Naombeni msaada wa haraka, NMB wamenikalia kooni

Hofu-less

JF-Expert Member
May 19, 2014
520
1,031
Wandugu poleni na majukumu, mwaka huu mwezi wa 2 nilienda kuwapelekea deni la loarn board walinunue na kwa kuwa nilikua na mkopo nao hao NMB wakanipigia mahesabu ya jumla kuwa pamoja na kununua hilo deni na kutoa deni lao watanipa jumla ya Tsh 5,660,000 nikasema poa tu kwakuwa nilikua na uhitaji sana, kufupisha stori ni kuwa jumla ya mkopo wote walinipa 17,400,000, sasa walipoingiza mimi nikakuta jumla ya 9,456,000 kwenye akaunti yangu.

Kwa haraka nilijua kuwa hiki ndicho kiasi changu nikatoa baadhi ya pesa na kuendelea kumalizia kibanda changu na kumaliza pesa yote. Sasa baada ya siku 10 afisa mikopo wa NMB akanipigia kuwa nirudishe mpunga wote yaani ile 9,456,000 maana lile deni la Loan Board halijalipwa bado.

Nikamuuliza kwanini hajalipa akasema mimi niliwahi kutoa pesa kabla hawajakata! Nikawapigia makao makuu, (audio clip ninazo) wakadai kuna makosa pande zote kwanza wao walitakiwa washikilie hiyo pesa kwanza mpaka miamala yote ifanyike, lakini pia walitakiwa ndani ya saa 72 kuwasiliana na mteja maana kumuachia mtu pesa zaidi ya wiki moja na kipindi hiki tunakijua ni mtihani, lakini pia wakasema nilifanya kosa la kutoa pesa ambayo ilizidi (kitu ambacho nilikubali) sasa jambo la ajabu wameniwekea credit -4,234,000 kwenye mshahara wangu na hivyo mshahara wangu wamezuia kwa ajili ya deni hilo.

Nimefanya njia zote ikiwemo kwenda tawini na kuongea nao, kuandika maelezo n.k lakini mpaka sasa wamegoma na option wananipa ni kurudisha pesa.

Nisaidieni wakubwa maana nimewaomba walau wakate kidogo kidogo pia wanagoma na sasa wanashikilia mshahara wote mpaka deni liishe ni zaidi ya miezi 8 na wote tunajua maisha ya mfanyakazi bila salary. Nisaidieni nifanyeje.

NB: Sipendi kuulizwa kwanini niliamua kutumia pesa zote.
 
Mkuu wewe si mwaminifu,sheria za kibenki zinasema ukikuta pesa imepungua au kuongozeka kwa account yako toa taarifa,nikuulize tu ungekuta mfano hakuna hata shilingi 50 elfu kwa account yako bila taarifa ungekaa kimya au ungeenda benki kuulizia?

Tena naona adhabu waliyokupa ni ndogo ulipaswa uwe sero.

Siku nyingine jifunze kuwa muaminifu na haya yote hayatakukukuta mkuu.
 
Back
Top Bottom