Naombeni msaada, Rafiki yangu anaangamia

Ushauri wangu ni huu
Kama ndoa hio haijawahi pitia sehemu yoyote ile kwa ajili ya usuluhisho..moja kwa moja ikaenda mahakamani haiwezwi kuvunjwa labda mahakama iamue kuwa separation lakini ndoa inaendelea kuwepo.

Kwa mujibu wa Law of marriage act Matrimonial properties ni mali ambazo zilipatikana kipindi mume na mke wanaishi pamoja, kama zilipatikana kabla haiwezi kuwa mali ya mume na mke itakuwa ni mali ya mtu 1. Japo ndani ya ndoa pia huwa kuna haki ya kila mtu kuwa na kitu cha peke yake ata kama wapo ndani ya ndoa.

Hakuna sheria ya 50 kwa 50 kwenye kugawana mali maana watu wengi sana wamekuwa wanaongea hili.

Sijaona ground nzuri ya uyo mwanamke kwenda mahakamani kudai taraka, asiongope ajipange vizuri atafuke wakili mzuri


Best lucky
 
Kaoa kwa kupitia dini gani?kama ni kwa Wakristo akatae kutoa taraka kama ni kwa Waislam kuna sheria anapewa 1 ya nne
Labda ungekiquote hapa hicho kifungu cha sharia maana nachelea ukachanganya na sharia ya mirathi Qur'an 4:12 inayoeleza mke kurithi robo ya mali ya marehem mumewe!

Ikumbukwe ndoa ktk uislam inaleta mambo makuu matatu tu ambayo ni;

1. Kuhalalisha tendo la ndoa
2. Kuhalalisha nasaba, na
3. Kuhalalisha mirathi

Wala haileti umiliki wa mali baina ya wenza/wanandoa hawa. Ispokuwa ktk kila jambo la kiuchumi wanalolifanya ni muhimu kila mmoja kujua sehem yake ktk chumo jumla.

Mfano, mke anapowekwa ktk duka la mumewe alilolikuta kwa ajili ya kuuza ni muhimu sana afaham/afahamishwe wazi kabla kwamba;

1. Anajitolea kama ihsani tu kwa maana bila malipo,
2. Anaajiriwa, au
3. Ni mwekezaji mwenza/mshirika (shareholder) na hisa yake ni sehem gani ya mali, kwa maana anakuwa mshirika kwa vile ushirika unaweza kuhusisha mshirika anayetoa utaalam tu (kama hivyo kukaa dukani na kuuza) na mwingine akatoa fedha.
 
OK Asante
 
Mali zangu alizonikuta nazo hata wakifaidi ndugu zangu haina shida.
Si ndugu zangu!!
Za watoto nawatafutia zao na ninaandika kila mmoja jina lake.
Mkuu, mnachosahau ni kuwa tupo kwenye zama za wanawake kutafuta kuchuma mali kupitia ndoa.
Kama una Mali zako binafsi unahitaji muda wa kumtrust unayedhani ni mwandani wako kabla hujakabidhi kila kitu.
Aafu, sio wote tuna mke mmoja mkuu.
 
Mfate Pm msaidie.Anatia huruma sana
 
Ndo maana Mimi namuelewa Sana jamaa aliyemchoma mkewe na gunia mbili za mkaa
 
Mkuu unaishi na mke au adui yako?
 
Msaidie baharia mama
The law says that married spouses must equally divide all of the property that the couple gained during marriage. It doesn't matter who paid for what, or whose name is on the deed for the property. Remember that the matrimonial home is divided equally even if someone owned it before the couple got married.
 
The law says that married spouses must equally divide all of the property that the couple gained during marriage. It doesn't matter who paid for what, or whose name is on the deed for the property. Remember that the matrimonial home is divided equally even if someone owned it before the couple got married
 
Hata hivyo tumesikia upande mmoja, hatujasikia upande wa dada
 
Agome kumpa talaka.....ila sheria zipo wazi.....amtafute mwanasheria atamsaidia......hilo sio tatizo kabisa...akomae....
 
hapana, kama una udhibitisho ulio dhabiti, hakika alizokukuta nazo hapati kabisa.......sheria iko vaisi vesa...
 
1. 50/50 sio automatic. Lazima anedai 50/50 aiobeshe mahakama mchango wake katika hizo mali "MACHUMO YA NDOA". Mali za urithi, mali personal, hususani ambazo spouse amezikuta, HAZIGAWANYWI.
2. Mahakama pia itaangalia Demeanor ya upande unaodai talaka au mgawanyo wa mali, akionesha UJINGA basi mahakama inaweza ikamuumizia hapo.

So, in summary:
- Contribution (proof)
- Demeanor.

Zipo decided cases Kwenye hili, unfortunately sipo nazo kwa hapa.
 
Pole yake mwamba.

Same story kuna jamaa alisomesha mke baadaye mke akapata kajamaa chuo akawa anakalisha kabisa.

Mume akamaindi mke akaenda mahakaman kudai talaka ili awe huru na kajamaa kake wakati huo mke alikuwa amepata ajira na amezaa mtoto mmoja kwa mumewe.


Mahakama haikuona sababu za msingi za kuachana mwisho ikaamua mali walizochuma pamoja zitakuwa za mtoto.


Mtoto ni wa kiume hataki kuishi na mama anahitaji baba.


Mke akaondoka zake kwa kajamaa kake.


MUME NA MKE ni WAZALIWA WA KUSINI MAshariki.


MUME JEURI NA ANAAPA HATAKUFA KWA PRESHA akaamuua aoe kusini kinda la 20yrs anatoka kitambi sasa.


MKE X ANAANZA KUTEMBEA KUWASABAHI MAJIRANI aishipo mume x.



Mama zetu usipowaelewa jua ndo umewaelwa.
 
Awe makini sana na kitu kinaitwa sheria na mahakama pale akifeli kidogo tu panga linatembea!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…