Naombeni msaada, Rafiki yangu anaangamia

Naombeni msaada, Rafiki yangu anaangamia

Huyo mke kwani ana documents zote za hayo mashamba na Mali ili aweze kuclaim zao?
Ndio maana hutakiwi kumuonesha kila kitu chako mke Kama kakukuta navyo.
Ndugu zako wanatosha kuwaonesha.

Mwenzenu mashamba yangu yote nimeandika jina la mama yangu.
Hata kama alishakufa lakini ndio hivyo tena.
Na hayajui hata yalipo Ila ndugu zangu wanayajua.
Na nilishawaambia, nikifa Mali zangu ni za wanangu popote walipo.
Kula gwala kwa kuwa Mwanaume badala ya Mvulana Mzee Baba
 
Umepotea ndugu... Hivi malalamiko yote ya ndugu kudhulumu mali za marehemu kaka yao hujasikia?
Hebu acha mawazo ya kuamini ndugu, watoto wako watateseka bro Ukitangulia mapema. Ungekuwa unaweza kuona usingeamini kinachotokea, hilo lenye jina la Mama yako warithi ni ndugu zako na sio watoto wako.

Utawadhulumu bure watoto wako kwa kujifanya unamficha mkeo.
Kaangalie mkanda wa "Moses" kwanza uliochezwa na Kanumba ndipo uje uaibike hapa.

NB:

Si kila Mwanamke ni Mke.
 
Sasa umeshakufa wakiamua wawapige chini watoto wako utawafanya nini?

Watoto wa mama yako ndugu zako wakisema Mali za mama yao unahisi wanao watapata urithi wao?

Umeandika kwa ujasiri ukajiona mjanja kumbe umepotea.....mzee ukishaoa na ukapata watoto no way out muamini tu mkeo muoneshe kila unachomiliki hata akiichoka ndoa akitaka mgawane mpe ni mama watoto wako pengine atakiendeleza ulichompa then watoto wako wakanufaika.

NB: Nenda kabadilishe hilo jina la marehemu mama yako mapema kabla hujafa hakuna ndugu atakayewapenda na kuwahudumia watoto wako 100% kukuzidi wewe na mkeo
Big No.
 
Ni bora Aandike majina ya watoto lkn sio ya ndugu... Akiondoka watawadhulumu tu.
 
Hapo ni busara tu itumike,cha kujifunza ukishakuwa na mali nyingi unatakiwa pia usiwe mwepesi wa kutoa talaka.....atakama utamfumania mwenzako tafuta njia nyingine hata ya kutokushirikiana naye tendo huku ukijua unafanya nini.Vinginevyo,kama una mali na unadai talaka uwe tayari kugawana mali,na kama una mali ila upande wa mwenzako ndio unadai talaka....unaweza kukataa au kama anataka aondoke,aondoke jinsi alivyo...ila wewe utabaki kusema bado unampenda; kwa sababu unajua kusudi lake ni kutaka mali tu.Inabidi utumie akili sana lasivyo uchumi wako utayumbishwa na kunyanyuka itachukua muda au usinyanyuke kabisa.
 
Kwani kaoa kwakupitia dini gani Aisee mzee dingi
 
Kaka ni kumwomba Mungu pekee akupe hekima la sivyo hizo hizo mali zako zitakutoa roho mapema kabisa.

Rejea visa vingi tu vilivyosababisha Wanaume wapoteze uhai sababu ya kukatalia kuachana na Wake zao akiwemo yule traffic police sajenti aliyeuwawa 2015 akacha Mkewe na watoto wawili...
 
Yameshatokea kwa Kaka zangu kibao, so usiniaminishe kwa mawazo yako ambavyo nimeshashuhudia mi mwenyewe binafsi.
Kumbe kwa kaka zako..... Ninachokisema kimenitokea mwenyewe.
Kaka zako na wake zao wa ndoa wamebahatika kupata watoto then mashemeji zako wakaanza kulilia mali bila kujali ustawi wa watoto zao ? Basi kaka zako walikutana na vyangudoa na kesi za ndugu kudhurumu mali za mayatima ni nyingi sana ukilinganisha na kesi za wamama walio ndani ya ndoa + watoto kuzitaka mali hizo kwa njia ovu ukizingatia mali ni za watoto wao.
 
Kaka ni kumwomba Mungu pekee akupe hekima la sivyo hizo hizo mali zako zitakutoa roho mapema kabisa.

Rejea visa vingi tu vilivyosababisha Wanaume wapoteze uhai sababu ya kukatalia kuachana na Wake zao akiwemo yule traffic police sajenti aliyeuwawa 2015 akacha Mkewe na watoto wawili...
Nakubaliana nawe;ila kabla hajafikia huko akutanishe wazee kwanza....au kama ni watu wa ibada waende wanakoabudu kutafuta usuluhisho (kiimani);kuachana ni mchakato
 
Ni bora Aandike majina ya watoto lkn sio ya ndugu... Akiondoka watawadhulumu tu.
Binadamu tumeumbwa na tamaa, mimi mwenyewe nitadokoa haswa nikijiona jua limeshaniwakia utosini 😂😂😂......... Unaanzaje kutumia jina marehemu mama yangu kwenye mambo yako utalipa tu. Chaguo ni moja tu unampa kisu mkeo ashike mpini ili awaangamize watoto wake kitu ambacho ni kigumu kutokea 98%
 
Juzi ofisini kwetu dada wakazi alikuwa anamali zake kabla ya kuoana na kilaza fulani baada ya mume wake kuwa na hawara nje akaenda akaomba talaka na mahakama ili muamuru yule mama wagawane mali zote pasu kwa pasu yule mama kagoma kuhangaika kwa muda mrefu ila hakushinda.
Kwa maana yule mama ndiye aliyekuwa na mali nyingi kushinda mumewe huyo basi wakauza kila kitu hadi nyumba wakagawana pasu kwa pasu hadi huruma ila kuna maujanja ya kufanikisha kesi hiyo ila kwangu mimi naogopa kusema hapa nisije nikaletewa noma .
Hii ya kugawana mali nusu kwa nusu huwa inatoka wapi au ni sheria ipi maana Law of marriage Act haijasema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom