Naombeni msaada kuufahamu hiki kiitwacho Bitcoin?

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Wadau, nakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusisituza vijana kucheza Bitcoin. Kuna kampuni ya Bitcoin imeniimgiza huko. Na inanitaka nianze Kwa kuwekeza $200 kwamba nitavuna $360. Je Kuna ukweli wowote katika Bitcoin?
 
Pitia hapa
 
Ukiambiwa kucheza jua utaliwa, ingia ukiwa na maarifa na taarifa unaingia kuwekeza sio kucheza.
Sio kila mtu anaweza kuwekeza kwenye masoko ya kifedha na cryptos.
Halafu ukiona unaambiwa weka hiki utavuna hiki, kimbia kabisa maana haya mambo hayana guarantee ni prediction sasa mtu akikupa constant hiyo ni red flag.
Nimemaliza
 
FB_IMG_1709030122478.jpg
 
Naona comments zote zinanionya. Nakimbia na hivi punde wakaamua kunipigia kwa WhatsApp nikajibu, "call me later for now I'm busy some how" ili nije kwenu WAJUZI. Nawashukuru sana maana nilishachomoa $1000 niwekeze nivume $5000.
 
Achana na hizo Mambo ndugu,hakuna fixed amount of return kwenye uwekezaji wowote,Tena kuhusu cypto market usiseme,nakumbuka nilipokuwa chuo nilikutana na kampuni moja inaitwa bitclub advantage unawekeza kwa kiwango kulingana na uwezo wako,xo jamaa alieni introduce yeye aliweka palefu Mimi nikaweka kidogo,tumeenda na karibia kutoa hela Sasa 😆🤣🤣
Wakaanza kuleta sababu,kuwa ili kutoa inabidi ufanye upgrade ya kifurushi Mimi nikashtuka nikamuonya rafiki yangu hakusikia alipigwa km ngoma kwa kifupi unaenda kuibiwa kijinga Sana,km hautasikiliza watu
 
Wadau, nakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusisituza vijana kucheza Bitcoin. Kuna kampuni ya Bitcoin imeniimgiza huko. Na inanitaka nianze Kwa kuwekeza $200 kwamba nitavuna $360. Je Kuna ukweli wowote katika Bitcoin?
Hakuna utakachovuna labda wewe ndio utavunwa, wekeza pesa yako kwenye biashara zinazoeleweka
 
Wadau, nakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusisituza vijana kucheza Bitcoin. Kuna kampuni ya Bitcoin imeniimgiza huko. Na inanitaka nianze Kwa kuwekeza $200 kwamba nitavuna $360. Je Kuna ukweli wowote katika Bitcoin?

Utapigwa achana nao matapeli yamejaa huko!! Kuna kampuni kama safeland nk ni matapeli, utaliwa hela yako.
 
Wadau, nakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusisituza vijana kucheza Bitcoin. Kuna kampuni ya Bitcoin imeniimgiza huko. Na inanitaka nianze Kwa kuwekeza $200 kwamba nitavuna $360. Je Kuna ukweli wowote katika Bitcoin?
Hapo utaingizwa mkenge,

Tadadhali nenda jifunze cryptocurrencies kwa ujumla wake.

Bitcoin is real, na ni fedha kama fedha zingine, na sifa yake ni kupanda thaman ama kushuka thamani kulingana na wauzaji na wanunuzi sokoni.
Moja ya soko kubwa na maarufu ambalo unaweza trade ama kuexchange sarafu hzo ni Binance

Hizo zinajiita kampuni za uwekezaji, uwape hela then wanakulipa hela fixed (yaani unakuwa unapata ROI) mwisho wa siku ni kutapeliwa tu.
Yani hapo upo kwenye hatari ya kupoteza pesa zako.

Wanatumia hyo bitcoin kwa wasio waelewa wa sarafu hizo za kidigital kuibia watu.
 
Bitcoin haichezwi. Bali ni sarafu ya kidigitali. Hivi sasa thamani ya bitcoin moja ni usd 62000, hivyo basi ukisema ununue bitcoin sasa utakuwa umechelewa sana...

Bitcoin inanunuliwa kupitia kwenye sites/ apps kama vile Binance, na wallets nyingine ambazo unaweza kuuza na kununua bitcoin.

Bitcoin ni sarafu ya kidigitali ya kwanza lakini hivi sasa kuna sarafu za kidigitali zingine kama ethereum, solana n.k zipo zaidi ya 1000 ambazo bado zina thamani ndogo ambazo unaweza ukanunua zikiwa na thamani ndogo na kuziuza zikiwa na thamani kubwa.

Mfumo wa uwekezaji wa cryptocurrency ni sawa na mifumo mingine kama ya stocks sema ni risky sana kutokana wakati mwingine inaendeshwa na hisia za watu hivyo ni uwekezaji ambao unaweza ukakufanya kuwa milionea au ukakufilisi hivyo unahitaji kujifunza kwanza kabla hujaamua kuwekeza kwenue cryptocurrency..

Pia unashauriwa kuwekeza kiasi ambacho hata ukikipoteza hairokuuma yani mfano pesa ambayo ungenunua iphone au kitu cha luxury au kama unafanya kazi ya mshahara wa uhakika basi asilimia kidogo ya kipato chako ambacho labda ungetumia kwa starehe.

Hayo ni baadhi tu kuhusiana na cryptocurrency na bitcoin.
 
Back
Top Bottom