Naombeni msaada kurudi bongo

Naombeni msaada kurudi bongo

Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu

HIYO $1800 HUKO INAFANYA NINI? NANI ALIYEKWAMBIA BONGO NI MSITUNI AMBAPO KUNA NYANI?
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
1800 na nauli humo humo bora ubaki hiyo million nne ndugu na unataka maisha ya juu
Utateseka huku
 
Japo ni Mzee Wangu ila 1800 unaomba ushauri kurudi bongo na unachagua maisha
Baki huko huko
 
Kama unarudi unarudi wakati mbaya kuna jamaa anaitwa Jei pm.Utakufa kwa stress aisee.Na je upo ugaibuni nchi gani?
 
Bora tu ubaki uolewe huko huko. Ukija bongo hata mwanaume wa kukuoa hutopata maana huku watakuchezea tu kama akina aunt shabani wanavyochezewa.mwishon watakuacha tu maana na umri nao umeenda.we miaka yote unamenya viazi na ndizi una akiba ya usd 1800?

Aiseee..... Wewe ulikuwa kilaza plus plus. Sasa uje bongo unadhani utapata mume kweli?komaa tu hivyo hivyo huko unaweza pata mume kikongqe mwenzio. By the way huku utatengwa pia.
 
Sorry mzee dereva nilitaka kukuambia tu kwa hela uliyonayo bongo hata hiyo nafaka hasa mchele hutakula utakula mihogo na maji kila siku mwisho wa siku utakuwa mnene Kama Kagame.
Huyu huyu PAKA tumjuaye ?
 
Dah ndugu yangu ni bora ukomae tu huko coz hyo pesa utaishia kwenye kilimo
 
Huyu bora arudi nyumbani tu na vile amekaa dunia ya kwanza amejifunza mengi akija kutumia kiakili anatoboza tu vzuri Bila shida yoyote kabisa. Kuliko aendelee kuishi kwa tabu
Sure!! Ile kanuni kwamba mjini shule inaweza kumsaidia! Sema dah! Sipati picha anadondoka home halafu ndugu wote wanajua jamaa kadondoka na "Boeing" huku wakiwa na matumaini kitu cha Range na BMW kinadondoka njia panda ya kwenda Zanzibar hivi punde kumbe!!

All in all, kurudi Bongo before it's too late ndo solution kwa sasa! Lakini ningekuwa mimi; ningepambana juani na mvuani... gizani hadi mwangani nipate angalau $5K za kufikia!
 
mimi siogopi maisha nyie vyura, acheni hasira zenu na kunitisha na maisha.
Mwezi February mwaka kesho narudi bongo na pesa hii hii na nitaishi tu.
Na pia mademu wenu nitawagonga.
 
Nyumbani ni nyumbani,kwani sisi tulizaliwa kutoka tumboni mwa mamazetu na pesa?pesa hutafutwa na muda hausimami,kwa uzoefu wangu na maisha ya viwanjani na umri uliokuwa nao nakushauri rudi home anza maisha mapya itawezekana,.kila la kheri.
 
Sikati vitunguu wala maboxi. Naendesha mabasi ya mjini. Kama UDA ya zamani.
Mkuu hata huko kuna aldhi utazikwa tu bola uwatumie kiasi ndugu zako tu. utadhalilika sana ukirudi kwa mtindo huo.
 
Back
Top Bottom