Naombeni msaada kurudi bongo

Naombeni msaada kurudi bongo

duuu pole sana.
mini nina uzoefu. mtu yeyote akiondoka kwao muda mrefu bila kuja kusalimia mara kwa mara huwa hawawi na akili nzuri ktk masuala ya jamii. mara nyingi mtu kama huyo utakuta kafiwa na watu wake kibao, pengine hata wazazi. lkn yeye haji tu. hiyo inapelekea kuwa mtu wa tofauti sana, mwingine unakuta hata familia hana. anaanza kuwa mzigo kwa wengine.

kwa habari ya huyu ndugu inabidi aendelee kukusanya nguvu. aone akifika miaka 55 atakuwa na kiasi gani. lkn kwa kiasi cha pesa alicho nacho ni kidogo. kwa wengine ni mshahara wao wa mwezi huo. isitoshe gharama za maisha ziko juu. endelea kudunduliza mpaka at lease 20+k $. hapo unaweza fanya kitu.
Uko sahihi mkuu na reference ni Dr. Shika
 
Mbula bora ubaki huko huko ukifa utaletwa kwa gharama za serikal ukija huku huku tuu kwa kina choendelea hautakaa hata wiki utajiua hata nyerere mwenyewe akifufuka ghafla ayakute haya ya tz atatamani arudi alikotoka
 
Hiyo hela akija nayo huku lazma ailipie kodi maana hii serikal nayo bhana..
Yani USD 1800 Zinakupa jeuri ya kutamka Kwa majivuno kiasi cha kujigamba hivyo? Bora ubakie hukohuko mkuu, hiyo pesa haitoshi kabisa kufanya hayo unayo dream ! Utakuja kujuta bure
 
Sikati vitunguu wala maboxi. Naendesha mabasi ya mjini. Kama UDA ya zamani.
Mzee wangu tulia huko huko,sikushauri urudi bongo na pesa km hiyo,piga kazi huko,jipange taratibu,hiyo pesa uliyonayo kwa msafiri kama wewe itakuishia ndani ya wiki 2
 
Sawa mkuu.sisi tupo bongo land.wengine tuna umri kama wa kwako.tunajiandaa ku staafu.wahuni walishapitisha sheria ya hovyo ya mafao ya uzeeni.tunajianda kula 25% ya pension.haitoshi hata mboga.tuna hali ngumu.malalamiko kila kona lakini watawala wameweka pamba.hawaelewi.pambana tu ughaibuni...

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo pesa ni nyingi sana mbona we kila siku hakikisha unabet tu na kucheza tatu mzuka na biko ukija bongo lazima utoboe.
 
miaka yote hiyo mkuu hujatoboa tuu au hata kuoa huyo demu wa kighaibuni? binasfi sijakuamini bado.
 
Kwanini watu ambao hamjawahi hata kwenda Namibia au Sri Lanka ndiyo mnajibu sana tena kwa hasira? Nani amewaambia maisha ni kufanya saving tuu bila ya kuishi? Mbona wazungu wengi hawana savings kabisa bank?

My weekly revenue and expenditure hii hii hapa.

Mshahara 500

Nyumba (3 bedroom) -115
Income Tax and social security -80
Energy Bill -22
Kula vizuri, family of 4 (siyo kula grain na mahindi) -80
Pocket money watoto wawili -30
Nauli za shule watoto wawili -18
Leisure club (swimming, hunting, etc) watoto wawili -20
Car Insurance -30
Car Fuel -35
Home broadband and Cable TV package -6
Mobile phone (parents) -12
One weekend meal out -50

Saving 2

Hapo bado kwenda sinema
Bado kupeleka watoto Disney Land

Sasa watu ambao wamishindwa kusafiri hata kwenda Msumbiji wanaleta hasira bure humu.
Mkuu nikushauri!! Kwanza kabisa weka mpango mkakati wa miaka hta 7, pia kwenye leisure baadhi zicancel ili uweze kusave hela ya kutosha

Ndani ya huo mpango hakikisha ndani ya miaka miwili uwe ushakuja bongo na kufanya survey uone km kuna possibility ya kuweza kurudi na kuishi vizuri. Then baada ya hpo rudi ughaibuni na kujipanga jinsi gani utarudi bongo na kuishi moja kwa moja

Hakikisha unajenga nyumba kbsa ya kuishi ili ukirudi bongo usihangaike na kodi.

Baada ya hpo utafute ni namna gani unaweza jitengenezea kipato kwa ajili ya kula na gharama ndogo ndogo za kila siku

Njia mojawapo unaweza itumia ni kununua shamba hta la ekari 10 na kupanda miti ya matunda yaani food forest ambapo pia utaandaa bustani za mboga mboga ....mpaka hpo utakuwa tayari na makazi na food security

Then baada ya hpo unaweza fanya vitu vikubwa zaidi kutokana na malengo yako

Kwa msaada zaidi njoo pm
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Hiyo hela itume kwenye namba hii 255 863 020 litatokea jina tea tootere.
 
Hello Thad, nakuona upo poa, usimdanganye huyo jamaa atakuja kukulaumu, hapa bongo hapafai kwa sasa
Sasa kama ka-make dola 1800 tu kwa miaka 26 aliyokaa ughaibuni si bora tu arudi bongo ambapo hata mpigadebe tu anadunduliza mpaka ananunua kiwanja na kujenga nyumba.
 
Uko sahihi mkuu na reference ni Dr. Shika

Ahaaa haaa haaa
unapotea home pia unasoma mno, lkn cha kushangaza bado unakuwa mzigo kwa wengine badala ya kuwa mtatuzi wa changamoto za JAMII.
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Pole sana kaka, Jinsi ya kuishi mjini utakaporudi toka ughaibuni, kama unaweza kufika bongo kwa hizo dola usd1800 tu bila kuweka nauli, unaweza kufanya hivi, dola 300 unapanga chumba kwa miezi 10, dola 500 unaweza kwenda kuungana na wadalali wa samaki feri, unaamka asubuhi unalangua samaki kwenye mnada unakomaa na wanunuzi wa reja reja, saa sita ushamaliza na umepata faida kama dola 80 hivi dola 20 weka akiba, 60 fanya matumizi mengine, ukifanya hivyo kwa miaka miwili, oa mama njasilia mali asiyeogopa shombo jiunge naye katika biashara hiyo , ndani ya miaka mitano utazoea tu unaweza kuchagua bisahra nyingine kwa kuwa tayari utakuwa ushapata marafiki. hiyo usd 1000 iweke benk fixed usiitoe kwa miaka miwili maana hiyo ndiyo itakulinda kama kikinuka unatambaa tena kama kawa
 
Pole sana mkuu, hivi hiyo $1800 hata nauli inatosha kweli (inategemea upo ughaibuni gani). Ukija Bongo hiyo pesa hata kodi ya nyumba ya mwaka inaweza isikutoshe.
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Kuna kambi LA wazee Bukumbi wilayani misungwi mkoani.mwanza wanalala, wanakula "NJOO NYUMBANI KUMENOGA"
 
Back
Top Bottom