Naombeni msaada kurudi bongo

Ushauri wangu endelea kuzichanga mpaka ukifikisha miaka 65 ndio urudi , kwa umri huo unaweza kukubalika kwenye nyumba za wazee pugu au vingungutu . Hapo ndoto yako ya kulala na kuamka kunywa maziwa itakuwa imetimia , maana huko msosi bure tu.
 
Utafikia wapi? Huko Gonja ukute wazazi walishaenda njia ya wengi.
 
Bongo kuna wanawake wanaoa? Mbona vijana MMU wanalalamika saana?
Watakuwa wanakosea timing! Dogo Mmoja wa kitaaa anauza GAME pale Mlimani city, nilimuuliza why wanafunzi wa vyuo jirani wanajaa sana maeneo yale? Wana purchasing power ya kutosha pale? Akanambia wale boys na mabeg yao mgongoni wanawinda Majimama!
 
Hiyo 1800 bado hujatoa nauli ya kurudia...anyway, karibu tz omba omba siku hz hawabugudhiwi kiviiiile.
 
WÉ RUĐÏ ŢÙ ÙJÎÒÑÊÈ MWĔÑŸËWË
huto tunyodo twako twote tutaisha
 
Naomba nikubuku asee ukifika tu nakutambulisha kwa nabii ili nakupiga ndoa fasta ila ujiandae kufanya kazi ya Mungu. Ila mi Mzee wa miaka 48.
 
Sikati vitunguu wala maboxi. Naendesha mabasi ya mjini. Kama UDA ya zamani.
Sasa kazi unayo si uendelee na maisha maana kwa masharti yako utaishia kunywa sumu tu,

Eti sitaki kula nafaka, very pathetic.
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo.
Bora ubaki hukohuko dingi...maana huku Jiwe kawakazia raia hawahemi....
 
Labda bombardier likianza ruti za huko azamie kurudi nyumbani
 
Hutaki kula nafaka unataka chakula yaan wewe nenda tu mbinguni kunakufaa
 
Mkuu ongeza speed kuserch money angalau urudi hata na usd 10000 upate hata cha kujengea kibanda na mtaji wa kulimia tangawizi huko upareni
 
JF raha sana,

Chige, umenichelesha sana.

Mr experience you know!
Hahaha! Raha sana enzi hizo... enzi za Yahoo Messenger! Wanazengo wakikushtukia, si kelele hizo "...don't trust Mr. Experience, he's a Nigerian!" Halafu najiita Mr. Experience wakati ndo kwanza nimetoka chuo... sina cha kufanya zaidi ya kushinda kwenye PC!
 
Lemutuz mbona ana miaka around 56 mtoto wake alivujisha siri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…