Naomba uzoefu wa eliyewahi kutumia Toyota Noah generation ya 2008

tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
3,245
7,115
Habari ya majukumu wadau. Nimejaribu kutafuta humu taarifa kuhusu Toyota Noah generation ya 2008 sijaweza kupata.

Naomba mwenye uzoefu wa hili gari anisaidie ili nifanye maamuzi. Nahitaji gari ya familia sasa nimepata machaguo mawili ambayo ni Toyota Noah na Toyota Alphard.

Taatifa za Toyota Allphard zipo baadhi japo kwa uchache ila angalau zitasaidia nikipata za Toyota Noah kabla sijafanya maamuzi.

Picha ya Toyota Noah generation ya 2008.

1000034687.jpg
1000034685.jpg
 
Mkuu
Alphard ina shida gani
Haina shida ya kiufundi,shida ni unatakiwa uwe na kibunda sana kuirun,kwani inakula sana wese,ukitaka ambayo haili wese uipate hybrid,ambayo nayo bei yake imechangamka sana,hz za kawaida nyingi ni 6 cylinder na bei sio kubwa ila utatoboka kwenye wese
 
Hii kitu sijui km ni tofauti. Mie Mkoani napata 11km per litre. Sioni km tatizo
 
Haina shida ya kiufundi,shida ni unatakiwa uwe na kibunda sana kuirun,kwani inakula sana wese,ukitaka ambayo haili wese uipate hybrid,ambayo nayo bei yake imechangamka sana,hz za kawaida nyingi ni 6 cylinder na bei sio kubwa ila utatoboka kwenye wese
Huifahamu hiyo gari, alphard nyingi unazoziona mtaani zinatumia engine ya 2az yenye 2360cc ambayo ni four cylinder, hiyo 6 ambayo ni MZ 3000cc Tanzania ni za kutafuta
Hiyo 2az ni engine nzuri hasa ukipata generation kuanzia 2005 ambayo ilifanyiwa maboresho, hiyo engine ya 2az inapatikana pia kwenye
-toyota harrier(Tako la nyani)
-toyota estima
-toyota vanguard
-toyota blade
-toyota Camry
-toyota matrix
-toyota corolla xrs
-toyota pontiac vibe
-toyota RAV4(2004-2013)
-toyota highlender
-toyota Ipsum
- Toyota avensis
-toyota velfire
-toyota mark x Zeo
-toyota scion
Nk
Unaweza ukaona ni jinsi gani Toyota walivyoiamini hii engine hivyo Kwa KESI ya engine spare na ufundi popote unaweza kupata.
Sasa unapofananisha engine yenye zaidi ya 2000cc na yenye below 2000cc the unakuja kusema alphard inakula mafuta haupo sawa,
Technically
- Nunua kutokana na matumizi Yako. mfano je ni muda mwingi gari itakuwa full capacity, njia unazotegemea itakuwa inapita, operation cost, resale value nk
Kwa upeo wangu ningekushauri chukua alphard kwani hata confotability, stability, space, utility IPO juu ya Noah
Angalizo Kuna matoleo mengi ya alphard hivyo wakati wa kununua lazima ujue unanunua Nini
Mfano alphad AX ni tofauti alphard AS
Alphad AX na AXL Zina features tofauti
Usije ukapanda alphad Alcantara version ukafikiri na wewe ukijiagizia TU na Yako utaikuta alcantara.
Kikubwa kabla hujaagiza fahamu unahitaji nini
 
Back
Top Bottom