Naomba ushauri

herimimi

Member
Joined
Aug 4, 2011
Messages
62
Points
0

herimimi

Member
Joined Aug 4, 2011
62 0
mimi nimeoa jirani sana na nyumbani kwetu. tangu nimeoa sijawahi kulala ukweni kwa sababu ni mwendo wa dakika tu kutoka kwetu hadi ukweni. rafiiki yangu anasema kuwa kitendo cha kutolala na mke wangu kwao ni kutomtendea haki kwani yeye analala kwetu. anasema ni vizuri kwa mahusiano kulala ukweni na mkeo eti inakuongezea heshima toka kwa wazazi wa mke wako! mimi kweli sielewi lakini mke wangu anasapoti. naombeni ushauri wenu.
 
AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,239
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,239 1,500
Sijaelewa vizuri... inamaana wewe unakaa kwenu na mkeo ama hua manalala kwenu mkienda kutembea huko nyumbani?? Alafu mila ya makabila mengi ya hapa Tz sio heshima mwanaume kulala kwa wakwe na Mkewe labda in speacial cases.. mbona kitendawili... mbaya zaidi anaesema hivo na kukupa headache ni rafiki wala hata sio wakwe.... kuna nini hapa Herimini??
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,198
Points
2,000

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,198 2,000
Kulala ukweni ni heshima?
Mi mbado kusikia hii
Huyo rafiki yako anakupa ushauri wa giza tena hata sijjui kama anajua nini maana ya wakwe
Hakuna cha heshima wala nini we kaa kwako bana na ndo maana ukaoa. Ingekuwa heshima ungemuacha mkeo kwa wazazi wake ukiwa na hamu nae unaenda kwa wakwe unafanya unalotaka then unarudi kwako
 
herimimi

Member
Joined
Aug 4, 2011
Messages
62
Points
0

herimimi

Member
Joined Aug 4, 2011
62 0
Sijaelewa vizuri... inamaana wewe unakaa kwenu na mkeo ama hua manalala kwenu mkienda kutembea huko nyumbani?? Alafu mila ya makabila mengi ya hapa Tz sio heshima mwanaume kulala kwa wakwe na Mkewe labda in speacial cases.. mbona kitendawili... mbaya zaidi anaesema hivo na kukupa headache ni rafiki wala hata sio wakwe.... kuna nini hapa Herimini??

tunalala kwetu tukienda kuwasalimia wazazi wetu..naambiwa siku nyingine tulale ukweni!
 
AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,239
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,239 1,500
tunalala kwetu tukienda kuwasalimia wazazi wetu..naambiwa siku nyingine tulale ukweni!

Hapo nimekupata... sijui kwa mila zetu, kama mnaishi karibu ina maana hata mila zenu wewe na Mkeo za fanana.... Fuatilia na uliza wazee wako kama ni kweli hayo maneno (thou bado siamini)... Mimi kama mtoto wa kike naweza ona aibu saana kutoka chumbani na mume wangu hata kama hatujafanya kitu... alafu nagongana na wazazi asubuhi... Liangalie kwa umakini hili suala...
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,198
Points
2,000

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,198 2,000
Ashadii hapo ndio ninapoona kituko. Unaamka asubuhi na mkeo hata kama hamkufanya lolote unakutana na mama mkwe mlangoni au koridoni mnaangalianaje na wanafikiria nini vichwani mwao
Ahh hata kama ni mila hizo nyingine ni balaa bana
 
AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,239
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,239 1,500
Ashadii hapo ndio ninapoona kituko. Unaamka asubuhi na mkeo hata kama hamkufanya lolote unakutana na mama mkwe mlangoni au koridoni mnaangalianaje na wanafikiria nini vichwani mwao
Ahh hata kama ni mila hizo nyingine ni balaa bana

Hapa ndo unatamani hata uulize wife ana age gani... ili walau kuelewa, kweli katika mila zetu za ki Africa leo ndo kusikia... Wengine hata ukiwa na ujauzito tu unaona aibu kwenda home...
 
Lokissa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Messages
7,452
Points
2,000

Lokissa

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2010
7,452 2,000
haina haja kulala ukweli kama ni karibu, labda ingekuwa ni mkoa mwingine mbali na kwenu mmekwenda kusalimia sawa lakini hapo hapo karibu ulale kwao ili iweje? hata wazazi wako watakuona ze comedy. vitu vingine bwana usiishi kwa kuogopa watu bali we ishi kadiri unavoona inakufaa wewe lakini isiwe kinyume na morals, sasa kulala kwa wakwe ndio utawaongea heshima? maisha? sifa au?? we kidume bwana umeoa lala kwako.
 
Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,603
Points
2,000

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,603 2,000
mimi nimeoa jirani sana na nyumbani kwetu. tangu nimeoa sijawahi kulala ukweni kwa sababu ni mwendo wa dakika tu kutoka kwetu hadi ukweni. rafiiki yangu anasema kuwa kitendo cha kutolala na mke wangu kwao ni kutomtendea haki kwani yeye analala kwetu. anasema ni vizuri kwa mahusiano kulala ukweni na mkeo eti inakuongezea heshima toka kwa wazazi wa mke wako! mimi kweli sielewi lakini mke wangu anasapoti. naombeni ushauri wenu.
Mimi mila na desturi yangu hainiruhusu kwenda kulala kwa mama/baba mkwe. Na hili kwetu linaongeza sana heshima kwa wazazi wa mke. Hivyo nina zaidi ya miaka kumi kwenye ndoa na sijawahi kulala huko. Sana sana huwa niawatembelea na kuondoka.
 
Forum statistics

Threads 1,379,206
Members 525,346
Posts 33,737,906
Top