Naomba ushauri wenu wana jf

kbz

Member
Jul 18, 2012
21
1
Poleni na majukumu yanayowakabili,

Mm ni msichana mwenye umri wa miaka 26,kwa mara ya kwanza najiunga na jf nikiomba ushauri wenu

Nina mpenzi wangu nampenda sana na hatuna mda mrefu, tuna miezi nane hatujawahi kufanya mapenzi ila tuna chati na kutembeleana, Ila kinachonitatiza yapata wiki sasa nikipiga cm hapokei wala sms hajibu,na hajanieleza chochote kama kapata mwingine au la sielewi nifanyeje kwa hili naomba ushauri wenu
 
actually use his friends to find out what goes on kwani huwezi jua chochote kwani yeye simu yake haipatikani
 
kama unasoma soma kwanza....masomo na mapenzi havichangamani,kuhusu kutopokea simu uwezi jua nini imetokea,kwani unakaa naye karibu? kwanini usimtembelee ujue tatizo lake nini...
 
Poleni na majukumu yanayowakabili,

Mm ni msichana mwenye umri wa miaka 26,kwa mara ya kwanza najiunga na jf nikiomba ushauri wenu

Nina mpenzi wangu nampenda sana na hatuna mda mrefu, tuna miezi nane hatujawahi kufanya mapenzi ila tuna chati na kutembeleana, Ila kinachonitatiza yapata wiki sasa nikipiga cm hapokei wala sms hajibu,na hajanieleza chochote kama kapata mwingine au la sielewi nifanyeje kwa hili naomba ushauri wenu
Chukua muda kwanza nawewe kaa kimya kama kweli naye anakupenda atakutafuta na kama anazuga hatakutafuta, take care.
 
pole sana csta ni vigumu kutoa hukumu ya kwa nini apokei cmu kwani hatujui tatizo lilompata fanya ufanyavyo ili ufahamu kwa nini imekuwa hivyo kwa sasa.
 
mfuatilie hata kwake kama unapafahamu, au tumia rafikii zake ili ujue kulikoni kabla ya kumtuhumu kwa kutopokea simu..ukimpata halafu haeleweki PIGA CHINI tena wala usiongee sana!
 
We bint we muda wote hujabanjuliwa kweli kuna vitu unavikosa sasa naomba kwanza
nikupongeze halafu.Acha kutoa hukumu bila vifungu kama dogo labda anaumwa au yuko
kwenye bad mood inaweza kutokea hiyo kitu.ila kama atakuzingua ucjali ma single tuko wengi humu jamii f.
nipm nitatue tatizo mi mwenyewe nishaumizwa mara mbili sitaki kuumizwa tena
 
Kwanza nakupongeza kwa kuwa na msimamo. Ila nataka nikwambie huyo atakuwa kashaingia mitini achana naye. Inawezekana kashindwa kukuomba TUNDA basi njia pekee akaona asipokee simu kama adhabu. Kwangu mimi namuona huyo kijana ana mambo ya kizamani. Wapenzi wanaojitambua huwa wanakutana wanaelezana tatizo wanatafuta njia ya kulitatua sio stahili hiyo ya kutopokea simu. Mimi nakushauri kama kwake unakujua basi nenda ili ujue tatizo ni nini kama haukufahamu na haujui sehemu ya kumpata mpotezee, endelea na maisha yako kama vile hujawahi kukutana na mtu kama yeye.
 
Kwanza karibu sana majukwaani kwa mara ya kwanza.
Mtembelee kwenye makazi yake...huenda amepatwa na la kupatwa!...usije ukamhukumu bure, kumbe mwenzio yuko hoooi kitandani, akiwa anaumwa ugonjwa wa kukumisi wewe!

PakaJimmy huo ugonjwa wa kummiss mtu dalili zake ni zipi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom