Naomba ushauri wa kozi ya kujiendeleza

Habarini WanaJF

Natumaini hamjambo wote. Mimi nimesome Bachelor Degree in Biology lakini nimejaribu kutafuta kazi nakosa naambiwa coarse yangu ni general sana.

Nilikuwa naomba mwenye kujua kozi ambazo naweza kujiwndeleza ili niwe specific

Natanguliza shukrani
Ulitaka uwe ticha....

Course Iko general sana .....
 
Una umri gani
Ada unayo ya kujiendeleza
Ungeandika hata courses ambazo unahisi utazimudu na ni rahisi kuajiriwa ili wadau tuongezee tuu
 
Aliyekuambia ukasome VETA anakutakia mema sana, kama una mjua mtumie hata Vocha.

Mimi pia hapa nakushauri kitu, sahau kuhusu hiyo Bachelor yako, nenda zako VETA tafuta kozi yoyote ya ufundi inayoweza kukuajiri, soma. Ipo siku utakuja kunishukuru.
 
Kuna jambo natamani nikushauri ila silielewi vzr maana nliishia la tano sijafika huko vyuoni ila mwenye kulielewa vzr atanisaidia kuweka sawa🤔🤔 baada ya kupata degree yako unarudi tena chuo kusoma mwaka Moja mfano Kuna jamaa alisomaga animal science lkn baada ya mazingira kua magumu akarudi kusoma mwaka Moja akawa mwalimu wa biology

Sijui na-make sense 😁kama nimevurunda niambeni nifute haraka
 
Back
Top Bottom