Naomba ushauri tafadhali

YESU YESU YESU

KABIDHI MAISHA YAKO NA FAMILIA YAKO KWA YESU.

OKOKA UANZE KUFURAHIA MAISHA.
 
Kuwa na Imani thabit na usiwe mtu wa kujaribu kila aina ya mambo

Mwamini Mungu wako sana na uswali na kumlilia sana Mungu
Kuna tatizo kwako ila hujasema upande wa familia yako wakoje
Je umeiliza nyumbani
 
Nimeuliza saaana bila kupata jibu la kueleweke. Baba na mama walishafariki kabla hata sijamaliza shule ya msingi, may be ningepata pa kuanzia
Kuwa na Imani thabit na usiwe mtu wa kujaribu kila aina ya mambo

Mwamini Mungu wako sana na uswali na kumlilia sana Mungu
Kuna tatizo kwako ila hujasema upande wa familia yako wakoje
Je umeiliza nyumbani
 
Salaaam.
Nimekuwa na changamoto katika maisha yangu na familia yangu.
1. Nilikuwa nimeowa mke wa kwanza 1996 na kubahati kuishi kwa miaka 9 ivi na kupata watoto 3. Lakini, ikaja changamoto mke akawa ananishutumu kuwa nawatuma watu wamzalilishe, akawa anakosa amani aliamini kuwa nawatuma watu wamchungulie Hadi chooni/bafuni na hata tunapolala. Nikamuacha kwa kuamini alikuwa analengo lake. Lakini baada ya kuachiwa Hali yake ikawa mbaya zaidi na kuwa mtu aliechanganyikiwa.

2. Nikaowa Tena 2003, lakini baada ya miaka Kama Saba Hali ya yule mke wa kwanza ikajitokeza kwa huyu na kupelekea kukosa Furaha ya ndoa. Amekuwa anasikia na kusema Mambo ambayo wengine tunashangaa tu na ngumu kuamini. Anaweza kuwa ndani lakini akakuambia watu wanamzomea au wanamtuka nje bila wengine kusikia
Mbaya zaidi kunasiku akaamka na kuniambia kuwa ameota kuwa na jitu kubwa na lilimwambia yeye ni mkubwa na aniambie nimwaache. Baada ya mwezi, anadai kuachwa. Naogopa kumwacha kwakuhofia lile la mke wa awali.
3. Wakati napambana na Hilo, mwaka juzi mtotowangu alitoka nyumbani nilikozaliwa na kuanguka na pikipiki na lakini hakuumia sehemu yoyote ile lakini alisema alishangaaa tu ameanguka na hakuwa anajielewa na kujikuta tu anaburuza pikipiki kwa mda mrefu na baada ya kupata fahamu akawasha na kurudi nyumbani anakoishi. Toka siku hiyo akawa anaongea Mambo ambayo ni ngumu kuelewa, atoki ndani mchana na kuchukia kuwa karibu na watu.
Naomba Allah akuongoze kunishauri Hilo maana linanikosesha amani. Naomba saana kwa Allah Ila nakosa maarifa ya kutafakari ndoto zangu.
Pole sana sana hii ina uhusiano mkubwa sana na ushirikina uliofanyiwa wewe kwa familia yako...
Je kuna mtu aliwahi kujiapiza kukufanyia mabaya?
Je kuna ndugu mlitofautiana mambo ya kifamilia?
Je kuna mwanamke ulishawahi kudate naye ukamuahidi ndoa na hukumuoa?

Tiba halisi ni pale utakapojua chanzo cha tatizo ama asili yake
 
Kwakweli ujanani ni mapito, nilikuwa na mahusiano mbalimbali lakini sikuahidi ndoa kwa vile nilikuwa na shule zaidi kupelekea kuchelewa kuowa. Nafahamu wengi walitamani niwaowe.

Sikuwai kugombana na mtu kufikia hatua ya kuwekeana vikwazo. Sio mgovi na muongeaji kitabia (mvivu wa kujibizana).

Sina ndugu nilietofautiana kifamilia labda Kama wivu na kijicho.
 
Pole sana sana hii ina uhusiano mkubwa sana na ushirikina uliofanyiwa wewe kwa familia yako...
Je kuna mtu aliwahi kujiapiza kukufanyia mabaya?
Je kuna ndugu mlitofautiana mambo ya kifamilia?
Je kuna mwanamke ulishawahi kudate naye ukamuahidi ndoa na hukumuoa?

Tiba halisi ni pale utakapojua chanzo cha tatizo ama asili yake
Bahati mbaya wazazi walishafariki kabla ya kumaliza shule ya msingi. Hata hivyo, nimewauliza Kaka na dada zangu, pia wajomba na mashangazi na wakubwa wa ukoo kupata histori yetu, bla kupata msingi wa matatizo yangu.

Dada yetu aliniambia nimezaliwa baada ya watoto Kama watatu kufariki wachanga na kupelekea maneno mengi Kati ya baba, mama na wazee wao na nikapewa jina la utoto Maneno
 
Vipi kuhusu mahusiano yako ya nyuma? Hujawahi kuharibu mahali?
 
Funguka kidogo mwisho ulikuwaje
Nilikwenda likizo home kabisa, kijijini, katika kaa yangu huko, nikalala nae na kurudi shule bila kujuwa Kama Ana ujauzito. Nilikaa mda mwingi kurudi huko na sikupata taarifa yoyote kuhusu Hilo. Ndugu zangu pia hawakunipa taarifa hiyo. Lakini baada ya mtoto kuzaliwa na kuendelea kukuwa DNN Za kienyeji zilithibiti kuwa ni wangu. Nilipomuuliza binti Kama Jambo Hilo ni sahihi alisema ndio na alitoa taarifa kwa dada mkubwa lakini dada zangu walilikataa.
Kaka alilifuatilia na mwisho kupewa mtoto.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom