Naomba ushauri: Mke wangu alinificha kwamba ameathirika

KIXI

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
1,624
1,885
Nimeishi na muathilika ambaye ni mwenza wangu ambaye naweza kusema ni mke wangu sababu nimeishi naye zaidi ya mwaka mmoja lakini kwa muda huo wote alikuwa akinificha kuwa yeye ni muathilika alikuwa akinywa dawa kimya kimya bila mimi kujua na kutokana na nature ya kazi yangu ya kusafiri safiri ilikuwa ni kazi kugundua lakini kuna siku moja nilikuta kuna ARVS kwenye mkoba wake nilipomuuliza aliniambia ni vya mdogo wake ambaye alikwisha niambia zamani kuwa mdogo wake huyo ni muathilika na mdogo wake ni mapepe sana kwa hiyo huwa anakwenda kumchukulia dawa panapobidi hapo niliamini itakuwa kweli lakini wanasema hakuna siri ya milele

Sasa leo nimejisikia homa na dizziness asubuhi nikaisi labda uchovu tu but hadi mchana naona bado hali ile ile ikabidi niende hospital kucheki hali nilipoenda kupima nikaambiwa sina ugonjwa wowote wakanipa dawa ya kutuliza maumivu niliporudi home nikamwambia hali halisi ya hospital yaani nimepimwa nimeambiwa sina ugonjwa wakati mimi bado najisikia homa ndio ikabidi aniambie kwamba yeye ni muathilika wa ukimwi since akiwa mdogo hadi leo ana miaka 24 anatumia dawa

Kwa kweli baada ya kuniambia hivyo nilijihisi kuchanganyikiwa nikarudi tena kupima HIV lakini majibu ya hospital nikaambia mimi niko negative yaani sina maambukizi na ukizingatia tayali tuna mtoto mdogo ana mwezi mmoja hapa namfikiria sana mwanangu bado mdogo na hii situation iliyopo nashindwa nifanye maamuzi magumu sababu huyu mwenzangu alidhamilia kabisa kuniambukiza but Mungu amenilinda.
Hapa ntaka kila mtu ashike njia yake je nitakuwa nimekosea kwa hili???
 
1. Kama anatumia ARV's kwa namna sahihi basi mimi nashauri endelea kuishi nae (ikiwa unaona bado unampenda) ama kaeni chini ili mkubakiane kuanza kulana kwa kutumia Condoms.

2. Kama unahisi tayari amekukwaza na hauna hpendo nae tena (basi muache), lakini kaeni chini mzungumze namna nzuri ya kufanya malezi ya mtoto pasipo kuwaumiza ninyi kama wazazi na mtoto pia.

Amua na uchukue moja kati ya ushauri 1 au 2 kabla hauja chelewa, pia hakikisha haumpotezei mzazi manzio muda na pia epuka kujenga uadui ambao unaweza ukamtia kinyongo mama hata akafikia hatua mbaya na kumuadhiri mtoto ama yeye mwenyewe.
 
Nimekuelewa sana mkuu
Asante sana kwa ushauri mzuri
 
Nimeishi na muathilika ambaye ni mwenza wangu ambaye naweza kusema ni mke wangu sababu nimeishi naye zaidi ya mwaka mmoja lakini kwa muda huo wote alikuwa akinificha kuwa yeye ni muathilika alikuwa akinywa dawa kimya
Hapa ntaka kila mtu ashike njia yake je nitakuwa nimekosea kwa hili???
Komaa nae tu mkuu maana uwezo wa kumuacha huna, Malaria inaua kuliko Ukimwi.
 
Kama muathirika anatumia dozi vzr, viral load wanakuwa wako kidogo sana, na ia virusi wsnakuwa dormant, ni kama wanakuwa wamefubaa hivyo hata chances za kuambukiza zinakuwa ndogo sana, ndiyo maana hujaambukizwa..

Cha kufanya hapo kwa kuwa alikuficha, ina maana alifanya makusudi na najua alikuwa anawaza akilana na wewe kwa muda mrefu utaupata, na akasubiri mmezaa kabisa, ili apige ndege 2 kwa jiwe moja, basi hauna budi kuachana naye kabla majuto hayajawa makubwa, maana siku ukikutwa nao hamtakuwa sawa tena....

Mwambie akuambie status ya mtoto, kama anao ama laah. Kisha mumlee mtoto, ila nyie kila mtu achukue hamsini zake.

Kiufupi huyo ni muuaji, alikuwa anajijua ila akakuficha.
 
Nimeishi na muathilika ambaye ni mwenza wangu ambaye naweza kusema ni mke wangu sababu nimeishi naye zaidi ya mwaka mmoja lakini kwa muda huo wote alikuwa akinificha kuwa yeye ni muathilika alikuwa akinywa dawa kimya kimya bila mimi kujua na kutokana na nature ya kazi yangu ya kusafiri safiri ilikuwa ni kazi kugundua lakini kuna siku moja nilikuta kuna ARVS kwenye mkoba wake nilipomuuliza aliniambia ni vya mdogo wake ambaye alikwisha niambia zamani kuwa mdogo wake huyo ni muathilika na mdogo wake ni mapepe sana kwa hiyo huwa anakwenda kumchukulia dawa panapobidi hapo niliamini itakuwa kweli lakini wanasema hakuna siri ya milele

Sasa leo nimejisikia homa na dizziness asubuhi nikaisi labda uchovu tu but hadi mchana naona bado hali ile ile ikabidi niende hospital kucheki hali nilipoenda kupima nikaambiwa sina ugonjwa wowote wakanipa dawa ya kutuliza maumivu niliporudi home nikamwambia hali halisi ya hospital yaani nimepimwa nimeambiwa sina ugonjwa wakati mimi bado najisikia homa ndio ikabidi aniambie kwamba yeye ni muathilika wa ukimwi since akiwa mdogo hadi leo ana miaka 24 anatumia dawa

Kwa kweli baada ya kuniambia hivyo nilijihisi kuchanganyikiwa nikarudi tena kupima HIV lakini majibu ya hospital nikaambia mimi niko negative yaani sina maambukizi na ukizingatia tayali tuna mtoto mdogo ana mwezi mmoja hapa namfikiria sana mwanangu bado mdogo na hii situation iliyopo nashindwa nifanye maamuzi magumu sababu huyu mwenzangu alidhamilia kabisa kuniambukiza but Mungu amenilinda.
Hapa ntaka kila mtu ashike njia yake je nitakuwa nimekosea kwa hili???
Pole sana .
Ukiona yafaa naomba ukapime tena sehemu zingine walau mara mbili baada ya miezi mitatu .

Ukiwa negative basi usikilize moyo kumuacha shemeji au kibaki naye maana hata ukiwa naye kuupata labda utake ila kuna njia za wewe kuwa salama .

Pole sana na hongera
 
Kama muathirika anatumia dozi vzr, viral load wanakuwa wako kidogo sana, na ia virusi wsnakuwa dormant, ni kama wanakuwa wamefubaa hivyo hata chances za kuambukiza zinakuwa ndogo sana, ndiyo maana hujaambukizwa..

Cha kufanya hapo kwa kuwa alikuficha, ina maana alifanya makusudi na najua alikuwa anawaza akilana na wewe kwa muda mrefu utaupata, na akasubiri mmezaa kabisa, ili apige ndege 2 kwa jiwe moja, basi hauna budi kuachana naye kabla majuto hayajawa makubwa, maana siku ukikutwa nao hamtakuwa sawa tena....

Mwambie akuambie status ya mtoto, kama anao ama laah. Kisha mumlee mtoto, ila nyie kila mtu achukue hamsini zake.

Kiufupi huyo ni muuaji, alikuwa anajijua ila akakuficha.
Na leo alipoona ninaumwa but majibu ya hospital nikaambiwa sina ugonjwa ndio akajua tayali ameshaniambukiza ndio maana akafunguka.
Asante sana kwa ushauri wako
 
Back
Top Bottom