MR KUO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 2,399
- 3,250
Mwezi mmoja nyuma nilipatwa na hali ya kuumwa kwa, kuchoka mwili na homa ile ya watu wazima mwili hauchemki ila kwa mbali unajisikia hovyo, nikaenda maabala, nikapima mkojo, tyiphoid na malaria mara nyingi ndo magonjwa yanayonisumbua sana haya nikakutwa na typhoid na mkojo mchafu malaria haipo nikanunua dawa azuma nikameza dozi ikaisha nikajisikia kupona.
Ila baada ya wiki moja hali ikarudi, kuchoka na kujisikia hovyo, kukosa hamu ya kula n.k ikabidi niende maabala nyingine kupima vyote nikakutwa na malaria 10 pekee daah.nikashangaa haya maajabu. Isiwe kesi nikanunua dawa zile za 2000 nikameza hadi dozi ikaisha nikawa kama nimepona pia nikaendelea na shughuli zangu.
Sasa juzi hapa hali imerudi kama kawaida muda huu ninavyoandika hamu ya kula sina na mdomo ni mchungu balaa.
Naomba ushauri wako nini nifanyeje, dawa gani au vipimo gani nipime hadi nikae sawa.
Naomba msaada raia mwenzenu nikifa taifa linapoteza nguvu kazi na ninategemewa na watu sio chini ya watano.