Naomba ushauri kwa mdogo wangu kuhusu ajira ya Tutorial Assistant

hooligan01

JF-Expert Member
Nov 21, 2013
662
523
Habarini ndugu zangu nilikuwanaomba ushauri kuna dogo langu anafundisha chuo kikuu cha Dar es Salaam kama Tutorial Assistant na kaitwa kufanya interview TRA kama Tutorial assistant.

Yuko anauliza je kuna umuhimu wa yeye kwenda TRA kufanya interview na akaachana na UDSM maana salary scale ya TRA ni nzuri na hajui kama kutakuwa na fursa mbalimbali kama allowances etc.

Nimeshindwa kumshauri moja kwa moja…naomba mawazo yenu wadau.

Ahsanteni.
 
Bila shaka yuko kwenye Payroll ya Government

For Tutorial Assistant ni kuwa ataenda kumasta mara moja

Even though hapo alipo ana free nyingi za kufanya private issue zake.

Okay let's say ameenda interview akapata baada ya muda mfupi wakaingiza waarabu, je ajira itakuwepo ?
 
Bila shaka yuko kwenye Payroll ya Government

For Tutorial Assistant ni kuwa ataenda kumasta mara moja

Even though hapo alipo ana free nyingi za kufanya private issue zake.

Okay let's say ameenda interview akapata baada ya muda mfupi wakaingiza waarabu, je ajira itakuwepo ?
Yes ana check number tayari ila kuna option ya yeye kuandika barua ya kuomba uhamisho…..hapo kwenye kumasta mara moja unamaanisha TRA??
 
Yes ana check number tayari ila kuna option ya yeye kuandika barua ya kuomba uhamisho…..hapo kwenye kumasta mara moja unamaanisha TRA?
Haiko hivyo. Kwa njia unayoisema, alitakiwa tangu wakati anaomba ajira huko TRA, barua yake ipitishwe na mkuu wake wa idara.

So long as ana cheki namba tayari, hawezi kwenda kupiga interview huko TRA kwa style hiyo, labda zingekua zimetangazwa zile nafasi za 'transfer'.

Dogo atulie tu, akapige masters yake aendelee na maisha hapo UDSM. Akituliza akili, aaze kuangalia namna ya kuanzisha a side hustle.
 
Aache tamaa! Akomae kwanza na hapo hapo! Mbona inawezekana kufanikiwa tuu. Kuna wengine hawajapata ajira bado asiwabanie nafasi.
Sasa mkuu hata atakapotoka ataacha gap la mtu mwingine kuajiriwa na hata akiamua apotezee, bado kuna mtu atakaepata na wengi watakaokosa.

Kiufupi kila mtu anacheza race yake na kama yeye anafikia hatua ya kuchagua ajira haimaanishi yupo responsible kwa wale wanaokosa. Kila mtu ashinde mechi zake
 
Back
Top Bottom