meghan markle
JF-Expert Member
- May 22, 2018
- 489
- 1,197
@Empress_sheila just so you know safari yako haitakua rahisi hata kidogo , as you can see comments nyingi za lawama, vitisho na kejeli lakini sauti ya Mungu ni kubwa kuliko yote hayo.Kwenye Biblia Yona aliitwa na Mungu akaokoe watu wa Ninawi lakini hakutaka kufuata sauti ya Mungu badala yake akapanda Meli kwenda Tarshishi ili asitii agizo lq Mungu lakini meli aliyopanda ilipata mawimbi sana hadi alipojitokeza akajisalimisha walivyomtupa baharini meli ikatulia na akamezwa na samaki akakaa kwa siku 3 tumboni kwa samaki akisali hadi samaki akamtapika kwenye ufukwe wa mji ule ule aliokua hautaki.....akafanya kazi aliyotumwa na kusudi la Mungu kikatimia.
Nimejikuta na relate habari yako na kisa cha Yona, inawezekana msukumo ulionao ni Mungu ameweka ndani yako ili akutumie kwa jambo fulani kudhihirisha ukuu wake, Inawezekana Mungu anataka akakutumie maisha yako yawe ushuhuda kwa wengine. Kuna maneno yanasema "God does not call the qualified but he qualifies the called " ....Mimi nakuombea kusudi la Mungu litimie kwako na akutumie vile anavyotaka.
Natamani sana sana uje utupe ushuhuda siku moja Empress_sheila
Kuna mwalimu wangu aliwahi kujenga hoja yake kuhusu utatu akasema.Inatosha, upo vizuri labda tu tuongeze kitu hapa ili kuelewana:
Ukisikia Mkristu anasema Yesu ni Mungu usidhani amemuondoa Mungu kwamba hayupo. Huku kuna fundisho la utatu, lakini huo utatu ni 'mmoja'. Akili yako ikiweza kuyachukulia haya ndio utaelewa kuwa wakristu pia tunamtambua Mungu mmoja na hakuna Mungu mwingine isipokuwa yeye.
Mfano familia fulani inamiliki gari moja.
Sentesi A. Tunalo gari jeusi, zuri linalotumia petroli na linakimbia kwa kasi sana.
Sentensi B. Tuna gari linalokimbia
Tunaruhusiwa kusema sentensi B na sentensi A ni moja. Tunaruhusiwa pia kusema sentensi B ni mwana wa sentensi A na wakati tulisha sema ni moja na hatujachanganyikiwa! Kosoa hii logic kwanza kama iko na makosa. Kama haifai niambie nitumie miduara[cocentric circles labda tutaelewana
Katika msingi wowote kama kwa jambo hilo unaweza kupata majibu zaidi ya mawili yanayotofautiana basi we nipe majibu yote tuNiamini au nisiamini kutokana na msingi upi?
Hongera..sikiliza sauti iliyo ndani yako..na uifwate..mimi ningekushauri ukipata muda nenda makanisa tofaut na Roma, naamin hutajuta..na utapata amani na kumjua Mungu wa kweli..mambo ya babu sijui bibi hakuwa hivi wewe haikuhusu..roho/spirit yako ndio itakayohukumiwa..sio maelezo ya babu yako..jamii na fanatics watakucheka na kukudharua..usife moyo..shetani yupo hivyo..acha watoto waende mafundishoMimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaid ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mktisto mama yangu ndiyo muislam, bahat mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielew kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasabu dini ya kiislam naijua nimesama madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zaman nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.
Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipend kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumban na natumia maji ya baraka wakat mwingi nahis kabisa yananisaidia, halaf nikiwa kanisani nina aman zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubir ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumban redio nasikiliza redio maria tu na naifurahia.
Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sahiv ndiyo nazid kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu nataman waanze mafundisho, au kuna sehem sijielewi?
Ndiyo bwana Aliwaambia maraika na shetwani wamsujudie Adam,shetwani akakataa na ndiyo kisa cha kulaniwa
Hivi unajua kani la Roma wewe?huu utumwa mbaya sanaHongera..sikiliza sauti iliyo ndani yako..na uifwate..mimi ningekushauri ukipata muda nenda makanisa tofaut na Roma, naamin hutajuta..na utapata amani na kumjua Mungu wa kweli..mambo ya babu sijui bibi hakuwa hivi wewe haikuhusu..roho/spirit yako ndio itakayohukumiwa..sio maelezo ya babu yako..jamii na fanatics watakucheka na kukudharua..usife moyo..shetani yupo hivyo..acha watoto waende mafundisho
Sawa na kupoteza na kupata,sasa wewe utashangilia kupoteza?Akislimu mkristu mnashangalia takbir ila akibadili muislamu kwenda ukristu inakuwa pepo baadhi yenu waislamu mna kazi sana
Wasiokuwa waisilamu hawatakwenda mbingu,huo ndiyo ukweli mchunguMkuu dini zote tunamuabudu Mungu na sio kwamba kwa sababu mtu ni dini flani basi ataenda mbinguni isipokuwa matendo yako yatakupeleka na uamini wako,dini zote zinahubiri mambo yaleyale hivyo kama una amani zaidi kwenye ukristo basi fata moyo wako.
Hiyo Afrika unayoizungumzia Afrika gani?ya kaskazini au kusini?Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu, na Mungu huyo anaetafutwa hapatikani pasipo kuwa na Imani. Na ukumbuke Imani ilikuwepo hata kabla Dini hazijatufikia huku Africa,
Unaweza umiza kichwa kufikiria kuhusu Dini lakini ujue wazi kuwa ndani ya dini pia kuna madhehebu ambayo kwa namna moja au nyingine yanapingana yenyewe kwa yenyewe ingawa yapo kwenye dini moja.
Hivyo utajikuta upo kwenye kibarua kingine cha kuuliza dhehebu lipi ni sahihi. (Wala huwezi kupata jibu)
Nachotaka kusema ni kuwa jambo kuu na lililo kubwa la kulizingatia ni Imani wala sio Dini.
Chagua pale roho yako inapenda then endelea kuijenga imani yako kupitia hapo
Ukitaka watu wakuambie nini ufanye utaishi maisha ya kinafiki kuwafurahisha watu huku wewe hauna amani ya moyo hata chembe.
Sijui kama nimeeleweka
Ulipoandika kuruan tu nikajua unaongopa,siyo muislam..ni qur'aanNani kakuambia sina hela?
Ninae jamaa tumekutana mazingira ya kazi kama unavyojua Watanzania hatuulizani haya mambo ya dini au kabila nilikuwa nasikia wanamuita Dennis na mimi nikawa namuita hivyo hivyo kumbe jina lake ni Jamal na nililijua hili kupitia kitambulisho chake.Familia yeyote, ikisikia Baba dini hii Mama dini hii, tegemea kupata watoto wasio kuwa na msimamo na dini yeyote.
Maana tangu kuzaliwa kwao kutoka kwa wazazi wasioujua Msikiti wala Kanisa, hawana mafundisho yanahusu dini.
Hivyo alieleta mada hii hapa ni zao la ndoa ya kwa mkuu wa Wilaya. Tena afadhari huyu anaetafuta dini akiwa mtu mzima na Watoto wake, naamini hajui kitabu chochote siyo Bibilia wala Qurani.
Mwenye kujua chochote hawezi kuja kuuliza wapi pa kwenda hapa JF.
Africa yetu waswahiliHiyo Afrika unayoizungumzia Afrika gani?ya kaskazini au kusini?
Ndiyo kuna sehemu hujielewi.Mimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaid ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mktisto mama yangu ndiyo muislam, bahat mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielew kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasabu dini ya kiislam naijua nimesama madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zaman nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.
Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipend kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumban na natumia maji ya baraka wakat mwingi nahis kabisa yananisaidia, halaf nikiwa kanisani nina aman zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubir ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumban redio nasikiliza redio maria tu na naifurahia.
Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sahiv ndiyo nazid kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu nataman waanze mafundisho, au kuna sehem sijielewi?
Ukiona jibu hili unatoa ujue huna pakupumulia. Update yourself before the hour comesHebu pumzika dada huendi popote na hamna aliyeenda akarudi ebooh
Umeona hasira tu hapo, mche AllahNinachopinga mimi ni kutishwa kupigwa mkwara kuhusu ukafiri sijui nini! Nimekuja kuomba ushauri wala sina shari na mtu sasa kwanini unijie na hasira? Lakini coment zote nazielewa na nachanganya na zangu! Aman!!
Ndiyo maana nakwambia wewe siyo muislam na hukuwahi kuwa muislam, kama ingekuwa muislam hungesema muislam anawezaje kuwa kafiri?Usije kwa mkwara mkuu! Nimekuja hapa kuomba ushauri pengine usome tena uelewe! Niko njia panda, hata wewe unayejiita muislam unaweza kuwa kafiri vilevile nadhani unajua kama kwel unaujua huo uislam, sitak kubishana na wewe badala yake kutokana na nilichohadithia hapo nishauri tu,
Wewe siulisema unaijua Qur'an sasa mbona unaanza tena kusema unasali kule unakoielewa lugha?.Huwa naumia roho yangu nikiona mikwara ya kutishana badala ya kuelimishana! Nimezaliwa kwenyw uislam lakini nimekua nawaza ukiristo sijapenda hivyo yaan sijawaza kubadilika ila mabadiliko yamenipenda na kule nimekuta hakuna kutishana bali kuna kuelimishana na kuhubiriwa kwa lugha ninayoielewa kiswahili, ninaomba na kusali ninachokielewa! Kwahiyo mkuu usinitishe hakuna aliyekufa akafufuka akaeleza aliyoyakuta huko! Hata yesu sijui kama alisema kwa mungu kukoje au unielekeze
Kwani wewe ulishakuta muislam anagalagazwa na mapepo au ulishawahi kukuta kwenye mihadhara ya waislamu watu wanashikwa mapepo.Ukristo ni ukafiri? Acha upopoma ww shwain. Hivi umewahi kutana na mganga mkristo? au jini la kikristo?
Jibu hayo maswali mawili nijue una upopoma kiasi gani.