Naomba ushauri kuhusu dini

Amen! Maneno yako yamenifariji hasa
 
Kwa mujibu wa UISLAM Hadi hapo ulipo ww sio muislam
 
Katika msingi wowote kama kwa jambo hilo unaweza kupata majibu zaidi ya mawili yanayotofautiana basi we nipe majibu yote tu
MIMI SIAMINI JIWE KAMA NI KIUMBE HAI NA WALA SIAMINI KAMA JIWE NI KIUMBE MFU.SABABU MIMI SINA ELIMU JUU YA JIWE.
 
MIMI SIAMINI JIWE KAMA NI KIUMBE HAI NA WALA SIAMINI KAMA JIWE NI KIUMBE MFU.SABABU MIMI SINA ELIMU JUU YA JIWE.
Naomba utambuzi wako katika dhana isiyo egemea kwenye imani

Jiwe ni koumbe hai au siyo?
 
Mambo ya umilikii. Oookay twende kazi. Nikujulishe kuna tofauti kidogo ya jinsi Mungu anavyochukuliwa baina ya hawa watu wawili:

Mmoja akasema kwamba Mungu ni kama baba yetu hivyo wote tulio chini yake ni wana wake, kuna wazaliwa wa kwanza wa pili mpaka wa elfu na wote ni wana wake na ana upendo kwao woote.

Mwingine akasema Mungu ni kama bwana wa watumwa kuna watumwa wa aina mbalimbali lakini wote sisi ni watumwa wake. Na kila mtumwa atapokea haki yake kulingana na utii wake.

Mimi nikiyatenda mapenzi ya baba yangu [huyu wa duniani]najua ninayatenda mapenzi yangu pia maana mapenzi yangu na mapenzi ya baba yangu ni 'moja'. Nikienda kufanya kazi shambani mwetu najifanyia kazi mimi, kwa kumfanyia kazi yeye. Sisi ni mmoja. In essence mimi pia ni mmiliki wa hilo shamba.
Ni tofauti kwa yule mfanyakazi niliye pamoja nami shambani yeye anafanya kilekile ninachokifanya mimi lakini sio chake, na anategemea mwishoni kulipwa ujira wake kwa haki.
 
Kaka mkubwa naomba tuwe logically consinstent, je unataka tutumie akili ama hautaki?

Na pia utuambie ni kwa nini hata katika Qur'ani kila mahala Mwenyezi Mungu anapotoa maagizo anasema 'Tumewaambia watu fulani....., Tutawalipia matendo mema.... Sio nimeagiza..., nitawalipia...? Unajua msione tu wa upande fulani hawatumii akili wakati hata upande uliopo unakubaliana na matumizi ya wingi kwa kimoja na ni sawa tu!
 
kimantiki inakataa sababu kikubwa hakiwezi kwa sawa na kidogo, yaani "Subset" haiwezi kuwa sawa na "Universal set" mpaka uanishe baadhi ya mambo na kuyatoa mengine.
Labda umenielewa zaidi ya nilichomaanisha; Kusema subset ni sawa na universal set ✅katika hili suala sio sawa na kusema universal set ni sawa na subset❌. Nisome kwa makini hapa.

Ni kwamba subset ni mmoja na universal set. Hakuna kilichopo kwenye subset kikakosa kwenye universal set. Subset ni mwana wa universal set. Ndio maana kwa sisi tulio wadogo sana kuliko subset, na zaidi wadoooogo kuliko universal set sana sana huwa mda mwingine tunarahisisha kusema subset ni universal set kwetu[for all intents and purpose in our finite word]. Lakini hata siku moja hutatusikia tukisema universal set ni subset. Na muda wote tunaaffirm kuwa universal set ni mmoja tu na hakuna mwingine.

By the way bro umenisaidia kuniletea hii concept ya set nayo ni njema maana nilitak kuitumia pia pale niliposema. 'Au tutumie cocentric circles?'. Thanks✌
 
Nilipouona huu mfano wako ndio Nimekumbuka hii, yaani najiuliza kama sisi watu wazima umeona huwenda hatuja uelewa huo mfano wako, sijui watoto wenu huwa mnawaelewesha vipi?
Msonjo na KING KIGODA kuna mambo mengi tu ambayo hayawapaswi watoto. Lakini ukishakuwa mtu mzima unapaswa kuyaelewa. Acha watoto wadogo wapewe maziwa sisi tule hadi makande.

Mnaweza kuona hata wenyewe, ukweli wake pale ambapo kila maagizo yanapotoka kwa Mwenyezi Mungu yanakuja kwa wingi. Kwa nini msipinge hili?

Ndo maana nikasema tusimuweke Mungu kama 'concrete' being tumuache hivyohivyo kama Roho ama wazo 'abstract' being

Unajua katika mawazo hakunaga utofauti kama ni lengo moja? Nitatoa mfano.
Kama lengo ni kujenga bomu. Chochote kitakachowazwa kuhusiana na uelekeo wa kujenga bomu kinaangukia kwenye wazo lilelile moja. Ni wazo moja. Ila kikitokea kingine kikawazwa kikawa cha kubomoa huo mpango wa bomu ndio kitaitwa wazo tofauti wazo la pili. Ndio tutapata mawazo mawili 1. kujenga bomu 2. kuharibu/kutojenga bomu
 
Mkuu!Hivi hata kiswahili ni kigumu kwako?.Ni wapi andiko limeongelea kufa mwili?Na niwapi nimekuambia kuwa mimi mkristo?
Usipoelewa kinachoelezwa na mtu ni bora zaidi ukikaa kimya kuliko kujidharirisha hivi.
King usiogope sana kuitwa mkristo mbona kila mkristo wa kweli ni muislamu, na kila muislamu wa kweli ni mkristo!😂😂😂

Mkristo ni mfuasi wa alichofanya na kufundisha Kristo, alichofanya Kristo ni 'Kuwa mtii wa mapenzi ya Mungu' na mapenzi ya mungu ni haya 'Kutumia akili yote na moyo wote kumcha Mungu, na pia kumpenda jirani'
Muislamu ni mtii kwa Mungu -Mtii kwa Mungu anafuata anachoambiwa na Mungu either directly[Yesu, Muhamad na manabii wote waliopita automatically wanakuwa ni waislamu!] au kupitia kwa manabii na mitume wake. Katika dunia ya sasa muislamu ni mfuasi wa alichofundisha Mtume specifically, Mtume alifundisha 'Mungu ni mmoja mcheni yeye, mimi nayewaambieni haya ni mtume wake tu'. Kumcha Mungu ni kuyatenda mapenzi yake [utii]. Mapenzi yake ni yepi? Yapo unayojifunza katika Quran na yapo waliyofundisha manabii waliopita katika Kitabu. Na manabii wa kweli ikiwa wanawasilisha ile Kweli huwa hawapingani kamwe! Sasa huoni kama ukisoma Injil utafuata alichofundisha Kristu[aliyefundisha pia utii na upendo], and by definition YNWAM.... Mkristuu🤭
 
Naona umeandika maneno mengi, ila hujajibu hoja ya umiliki, umiliki wa jambo lazima liwe lako, hakuna niaba ya umiliki mpaka iwe miliki imehamishiwa kwako.

Kingine nafsi ndiyo inonyesha upweke wa mtu. Hakuja nafsi mbili tofauti zikawa moja, hata lugha hili jambo inalikataa.

Kingine Mungu si kama baaba yetu wala haiwezekani kuwa baba yetu, sababu kiuhalisia ubaba ni wa kinasaba na kimaana kadhalika.

Kingine matumizi ya tamko "kama" kuonyesha kutokuwa sawa hicho unachokilinganisha na kitu husika. Napata wasi wasi na ufahamu wako juu ya lugha.
 
Nitumie email yako PM nikutumie material ya kukusaidia kuamua!
 
Kaka mkubwa naomba tuwe logically consinstent, je unataka tutumie akili ama hautaki?
Akili lazima itumike ila haiwezi kutumika peke yake sababu ina ukomo.

Hili jambo halitaki akili kubwa ni uhalisia tu na matumizi sahihi ya lugha.

Sasa unaposema utumie akili halafu unapotosha maana yake akili haijakusaidia wewe.
Shida yenu siyo tu hamsomi bali hamtaki kusoma. Hili jambo katika lugha lipo sana hata katika lugha ya Kiswahili na Kiarabu lipo tangu zamani, ndiyo maana hata waarabu hawakugagaika nalo, namna ya wingi kuwasilisha maana ya umoja ni katika mlango wa kujifadhilisha (Jina la kujifadhilisha).

Leo hii mimi naweza kusema hivi "Viatu kama hivi tuna vaa watu kama sisi" haimaanisha hapo tuko wengi bali naonyesha upekee wa kiatu hicho.

Sasa kingine Mola ameshajipambanua juu ya umoja wake na kupwekeka kwake na matumizi hayo ya wingi ni kwa kujifadhilisha.
 
Kijana unafaa kupigwa makofi. Mwana hawezi kuwa sawa na baba au mama aliye mzaa, akili yako inafikiri kwa namna gani ?

Hata kihesabu subset hawezi kuwa sawa na universal set mpaka baadhi ya mambo yatoke na mengine yaingie. Kitendo cha wewe kukubali tu ya kuwa subset iko ndani ya universal set maana yake viwili hivi havifanani.

Sasa nakupa kazi, kaangalie kanuni ya Universala set kisha uje kuniambia ni wakati gani subset inakuwa sawa na universal set mathematically, kisha uje ujikosoe mwenyewe. Kuna muda mnatuchosha sana aisee kuwaelekeza.
 
Kingine Mungu si kama baaba yetu wala haiwezekani kuwa baba yetu, sababu kiuhalisia ubaba ni wa kinasaba na kimaana kadhalika.
Nalijua hili kaka, na nishagundua kuwa ni moja ya matatizo yetu makubwa baina yetu ni jinsi tunauchukuliaje kisura uhusiano baina ya mtu na Mungu, kiumbe na Mola. Na naomba usitake kuyumbisha hapa. Tunaposema Baba Yetu uliye mbinguni, hatuappeal kwamba tunahusiana naye kinasaba. La. Yeye ni baba wa kiroho na ndivyo ilivyo. Tulipoumbwa tuliumbwa kwa 'mfano' wake kiroho. Na ukikubali na kuamini basi unafanyika kuwa mwana wake kiroho, rohoniii heeh!
Kingine matumizi ya tamko "kama" kuonyesha kutokuwa sawa hicho unachokilinganisha na kitu husika. Napata wasi wasi na ufahamu wako juu ya lugha.
Itoshe labda kusema lugha haijitoshelezi hasa katika kubagua ya kiroho na ya kimaterial. Ila ukiwa na akili analojia nayo inasaidia
 
Naona umeandika maneno mengi, ila hujajibu hoja ya umiliki, umiliki wa jambo lazima liwe lako, hakuna niaba ya umiliki mpaka iwe miliki imehamishiwa kwako.
Wakristu tunao mfano wa mwana mpotevu usome utakusaidia. Na ufalme wa mbingu unafananishwa na namna hiyo, yule baba alisema 31 “Baba yake akamwambia, ‘Mwanangu, umekuwa nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako
 
Unaelewa nini pale nguzo ya Imani ya Dini yetu ya Kiislamu inapotaka kuviamini vitabu vya Mwenyezi Mungu?.
Pili mimi ntamuelewesha asiye Muislamu kwa njia atakayo ielewa kwa wepesi kwa kutumia mifano na njia alizo zoea.
Ningekuwa najadiliana na Muislamu mwenzangu,basi nisingetumia Injili bali ningetumia Qur'an,hadithi na sunna za mtume.

Nafikiri umenielewa.
 
Usikimbie hoja.

Hebu ingizia huo mfano wako wa gari linalomilikiwa na familia na hizo sifa zake, katika kufafanua utatu uone unavyojichanganya.
 
Hata kihesabu subset hawezi kuwa sawa na universal set mpaka baadhi ya mambo yatoke na mengine yaingie. Kitendo cha wewe kukubali tu ya kuwa subset iko ndani ya universal set maana yake viwili hivi havifanani.
Sawa nakubali havifanani vyote kama vyote. Havifanani. Ninakubali kimaterial kuwa 'Mwana hawezi kuwa sawa na baba au mama aliye mzaa' Ila kimalengo, kiabstract, kiroho, kilogic hilo lipo.

Na utofauti wake upo hivi tukiuangalia sisi tulio wadooogo sana. Ni kwamba kutokana na udogo wetu sisi tunamuona Mwana kama 'infinity' kwetu. Ila tena tukijaribu kumuimagine Baba basi tutasema yeye anakuwa 'infinity plus one' au hata 'infinity plus hundred' au potelea pote labda ni 'infinity plus infinity' au ngoja tuvuruge labda baba ni 'infinity plus infinity, infinitely'

Sasa kwa kuwa sisi ni wadogo, finite beings: infinity ya aina yoyote na ukubwa wowote makes no difference in our perception of infinity. Ndo maana unaona kama tunajichanganya. Subset kwetu ni infinity [kikwetu] japo tunatambua kuwa imo ndani ya universal set ambayo ni infinity infinity
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…