Naomba ushauri, kila nikipanga mipango haitimii

Kuna mahala niliwahi kusoma "Ukiwa unaota upo shuleni na ili hali ulishamaliza shule kitambo sana, kuna asilimia kubwa ya kiashiria cha kurudishwa nyuma katika mambo yako unayofanya hasa ya kimaendeleo". Kurudishwa huko nyuma kunachagizwa hasa na nguvu za giza, kila la kheri mkuu!!
Naweza kuamini. Kila nikijaribu kuhusianisha matukio naona kuna uhusiano.
 
Kwenda kwa waganga ndo uliharibu kabisa, wangekuwa na uwezo huo watz wasingekuwa fukara.Kuota unasoma shule ya msingi ni kurudishwa nyuma kimaisha.Ulipoenda kwa mganga kakuongezea majini ya mikosi utabadili waganga hadi ukome na solution hamna.
 
Mi naona kawaida tu kwakweli, I just thank God....
Ila huwa natamani kuelewa maana ya hii ndoto, kuota mara kwa mara nipo shule.
Manake akili yako kuna jambo inalihangaikia bado halijakamilika, kama hivyo unatafuta suluhisho la matatizo yako, usijali pambana ipp siku utavuka hicho kikwazo na utasahau hizo ndoto
 
Shida uliyonayo ni ya kiroho zaidi kwani hiyo kuota upo shule ya msingi ni stagnation kama walivyosema.Kwenda Kwa sangoma ni kosa jingine kwani hujatibiwa umeongezewa matatizo kwani jini au pepo hamtoi mwenzie. Chanzo Cha tatizo ni vitu mchanganyiko unahitaji upate madhabahu yenye nguvu na uweze kuamini na kuuacha uchafu unaoufanya ili upate deliverance.Angalizo maombi ya Kiislam hayatakusadia.
Acha kudanganya watu,Mzee wa upako mwenyewe amefundishwa na muislam,marehemu sheikh YAHYA mtabiri wa nyota.Wewe ni ZUZU
 
Daah ata mm hua naota sana kijijini kwetu sjui ttzo ni nn jaman yani haipiti sku mbili
 
Mi naona kawaida tu kwakweli, I just thank God.

Ila huwa natamani kuelewa maana ya hii ndoto, kuota mara kwa mara nipo shule.
Uliwahi kusoma shule? Kama ulipitia shule basi siyo ajabu. Ni wengi tu huwa tunaota mambo yaliyotokea nyuma. Inategemea na state of mind uliyonayo.
 
Habari za muda ndugu zangu.

Hope weekend yenu imekaa njema

Wacha nisipoteze muda niingie kwenye mada.

Mimi ni kijana ambae nimekuwa nikihangaika sana kwenye mambo yangu lakini huwa sifanikiwi inshort huwa nina mipango mizuri mno lakini haijawahi kufanikiwa, unaweza kuongea na mtu akakuahidi jambo fulani ila mwisho wa siku atakuja kukukataa tu.

Yaani Jambo nalianza vizuri but mwisho wa siku huwa ni kufeli tu mpaka huwa najiuliza huwa nina mkosi gani, hata kwenye mahusiano nimekuwa ni mtu wa kuhangaika tu. Maana sijawahi kutulia kwenye mahusiano na mtu hata kwa mwezi mmoja.

Kuna mtu akaja kunishauri niende kwa wataalamu basi nikaenda kwa mtaalamu mmoja akaniambia nyota yangu imechukuliwa ndio maana kila nalofanya haliendi.

Nikamuuliza bei akaniambia nimpe 120k, nikampa hiyo hela akanipa madawa nikaogea nikamaliza but sikuona mabadiliko mpaka sasa mambo yangu bado magumu halafu mara nyingi huwa ninasumbuliwa na ndoto za kuwa shuleni tena primary na classmate wangu niliomaliza nao kitambo kile. Sasa sijui nina shida gani ndugu zangu naombeni ushauri nini nifanye ili mipango yangu iweze kwenda maana naona kama nina nuksi.
Kupanga mipango ni kitu kimoja, na kuitekeleza ni kitu kingine. Kama ni kupanga tu basi nakuhakikishia kila binadamu anapanga lakini mipango inayofanikiwa mara nyingi ni michache. Halafu jambo jingine wewe unachanganya ''ndoto za alinacha'' na kupanga mipango. Pia nimegundua ''mipango'' unayopanga wewe akili zako zinadhani ni mizuri kumbe siyo mizuri. Je, kuongea na mtu na akakuhaidi jambo ni kupanga mpango? You cant be serious! Yaani upange mipango kwa kutegemea msaada wa kuomba kutoka kwa mtu halafu asipokupa unasema mipango imeenda vibaya?
 
Back
Top Bottom