Naomba ushauri, kila nikipanga mipango haitimii

Melancholic

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,831
3,063
Habari za muda ndugu zangu.

Hope weekend yenu imekaa njema

Wacha nisipoteze muda niingie kwenye mada.

Mimi ni kijana ambae nimekuwa nikihangaika sana kwenye mambo yangu lakini huwa sifanikiwi inshort huwa nina mipango mizuri mno lakini haijawahi kufanikiwa, unaweza kuongea na mtu akakuahidi jambo fulani ila mwisho wa siku atakuja kukukataa tu.

Yaani Jambo nalianza vizuri but mwisho wa siku huwa ni kufeli tu mpaka huwa najiuliza huwa nina mkosi gani, hata kwenye mahusiano nimekuwa ni mtu wa kuhangaika tu. Maana sijawahi kutulia kwenye mahusiano na mtu hata kwa mwezi mmoja.

Kuna mtu akaja kunishauri niende kwa wataalamu basi nikaenda kwa mtaalamu mmoja akaniambia nyota yangu imechukuliwa ndio maana kila nalofanya haliendi.

Nikamuuliza bei akaniambia nimpe 120k, nikampa hiyo hela akanipa madawa nikaogea nikamaliza but sikuona mabadiliko mpaka sasa mambo yangu bado magumu halafu mara nyingi huwa ninasumbuliwa na ndoto za kuwa shuleni tena primary na classmate wangu niliomaliza nao kitambo kile. Sasa sijui nina shida gani ndugu zangu naombeni ushauri nini nifanye ili mipango yangu iweze kwenda maana naona kama nina nuksi.
 
Kuna mahala niliwahi kusoma "Ukiwa unaota upo shuleni na ili hali ulishamaliza shule kitambo sana, kuna asilimia kubwa ya kiashiria cha kurudishwa nyuma katika mambo yako unayofanya hasa ya kimaendeleo". Kurudishwa huko nyuma kunachagizwa hasa na nguvu za giza, kila la kheri mkuu!!
 
Kuna mahala niliwahi kusoma "Ukiwa unaota upo shuleni na ili hali ulishamaliza shule kitambo sana,kuna asilimia kubwa ya kiashiria cha kurudishwa nyuma katika mambo yako unayofanya hasa ya kimaendeleo". Kurudishwa uko nyuma kuna chagizwa hasa na nguvu za giza, kila la kheri mkuu!!
Ahsante mkuu
 
Nakuja mkuu
 
Na hata mi niliwahi kusikia hivyo mara nyingi
 
Waganga matapeli tu mkuu, we focus na mambo zako ipo siku utatoboa.
Ukienda kwa mganga uwa shida haziishi ukimaliza kufungua nyota utaambiwa jiranj anakuroga,
Hata mimi nilikuwa mzito sana kwenda kweli hawa watu hawafai
 
Back
Top Bottom