Naomba ushauri juu ya dawa za kuongeza mwili

Naomba ushauri juu ya dawa za kuongeza mwili

Mwanangu me nakupa ushauri, ukitaka kunenepa jambo la kwanza ni Kula ule walau mara Tatu kwa siku tena ule haswa, kama unahisi huwezi kula nunua dawa za kuongeza hamu ya kula, sio unakula kwa mama ntilie hapana, pika mwenyewe nunua hata rice cooker tu, unajipikia wali mwenyewe mboga unaenda kununua nje,

na sio unakula maharage unaenda kununua hata kuku robo au nusu au mishikaki unakuja kula na wali, huku kila asubuhi unapiga push ups 50 tu kila siku mzee wiki mbili nyingi utaanza kuona mabadiliko, chengine stress achana nazo kabisa ukiona jambo linataka kukupa mawazo litupe kule hata utaona mabadiliko kabisa
 
Kadri siku zinavyoenda wembamba wangu unazidi kunipa stress nilifikiri nikiwa mbaba nitaongezeka mwili ila imekuwa kinyume kadri siku zinavyoenda ndio nazidi kupungua.

kila nikikutana na mtu tunayefahamiana swali la kwanza kuniuliza mbona umekonda sana unaumwa?

Kinachoniumiza siyo kukonda ni usoni maana angle za fuvu zimeanza kuonekana kuhusu minyoo najitahidi kula dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu ila bado.

Leo nimetumiwa nauli nirudi Mkoani sababu ya wembamba wangu eti maisha ya mjini yamenishinda.
Tafuta unga wa Muyoma na katigula changanya uwe unga mmoja
Chukua ulezi kilo mbili na mtama kilo moja saga
Tumia mchanganyiko wa dawa yako kuweka kwenye uji wa ulezi na mtama
Hii ni mujarrabu unanenepa fasta
 
Ngoja namimi nijaribu kutoa ushauri kuhusu kunenepa.

Kwanza kabisa unatakiwa ujue chakula si kitu pekee kutakachokufanya unenepe.

Unene ni matokeo ya afya ya mwili na afya ya akili.

Afya ya mwili ikiwa sawa na afya ya akili ikashake.
Basi unene uko mashakani.

Kwahyo pamoja na kuhakikisha unajiweka sawa kwa milo mbalimbali basi hakikisha na stress zote zimepunguzwa kwa kichwa kama si kuondolewa kabisa.

Unene pia ni masuala ya familia.
Kama kwenu kuna wanene basi nawewe utanenepa zingatia mlo kamili.

Kama kwenu hakuna historia ya unene.

SAHAU KUNENEPA😁😁.

WEwe sio LEONARDO KWELI😁😁😁
 
BabaMorgan ukiachana na sababu zingine zote kuwa mwembamba ni ishu ya vinasaba (genetics) so unakuta wewe unakuwa na High or fast metabolism ambapo chakula unachokula chote kinatumika hakuna kinachohifadhiwa na ili unenepe sharti kiasi fulani cha chakula unachokula kihifadhiwe.

Kwanini unazidi kupungua?
• kama hauna shida yoyote ya kiafya basi ni ishu ya appetite watu wembamba wanakawaida ya akila kidogo tu ameshiba so kama wewe huwa unakula milo mitatu kwa siku maana yake chakula unachokula hakikidhi matumizi ya mwili so mwili unaenda kuchukua kile kidogo kilichohifadhiwa ili kufidia kilichopelea ( Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho. Note:Haihusiani)

Sasa unawezaje kuongezeka uzito au kunenepa wewe kama mtu mwembamba?
• Usile ile milo mitatu mikubwa (Breakfast, Lunch & Dinner) bali kula milo midogo midogo lakini mingi, kwa siku kula mara sita na zaidi isiwe chini ya hapo yaani we kula kula tu over time mwili utaongezeka wenyewe.
• Kumbuka ni ishu ya genetics so sikushauri uharibu hela kwenye virutubisho, vidonge na vitu kama hivo unless unataka tu kuweka watu mjini
 
Kuna vitu hujaweka sawa ili tukushauri vizuri,
1.Je unategemea kimaisha yani unakazi yako unaingiza kipato cha kutosha mahitaji
2.Je una familia?
** hata ukiwa na hela kama Elon musk ukiwa na stress lazima huta nenepa kamwe.
Unene ni afya ya akili kwa 80% na chakula kwa 20%
 
Ndiyo😂😂😂. Kumbe bhana ukinenepa na ngozi inanawiri. Kipindi mwembaba nilikuwa napaka mafuta ya bei na ngozi haing’ai kumbe uchawi ni kula vizuri bhana😂😂. Siku hizi wamebaki kuniuliza pia najipaka mafuta gani kumbe najipaka mafuta wanayopaka watoto wangu .
Nina kabinti kangu kembamba mno..kumbe kuna siku katanenepa nimeshachoka kuhangaika nae..kula yake ni tabu..ila huwa haugui hata mwaka mzima..
 
Tafuta unga wa Muyoma na katigula changanya uwe unga mmoja
Chukua ulezi kilo mbili na mtama kilo moja saga
Tumia mchanganyiko wa dawa yako kuweka kwenye uji wa ulezi na mtama
Hii ni mujarrabu unanenepa fasta
Ila watu mnapenda kuficha mambo sasa muyoma katigula ndo nini..hapo unataka ufwatwe pm..
 
Ngoja nisome na mimi, wahanga ni wengi.

Mimi Suruali ni 31, mpk sio poa.
Japo mimi nipo stable, sishuki wala kupanda, nimezoeleka kwa mwili huu tangu tuu nilipoanza Advance.

Hii imekuja kuathiriwa zaidi ni ulaji wangu, pact moja ya karanga na Soda Nashiba kabisaaa, kuna mtu kaniambia hata kula yangu ya haraka haraka yaweza kua sababu,
Ni kweli hua nakula haraka na pia ni nadra sana nikala huku nimekaa, kwa ufupi Sijawahi Kua serious na chakula.

Mtaani wananiita Magrili, yaani kwenye dirisha la grili napenya vzr kabisa, mguu wangu na Square pipe ya grill havitofautiani sana,
Dr. Kanishauri nipunguze(suala la kuacha nilimuambia asiliwaze) nyeto. Ila nimeacha, ngoja nione, Nisipo nenepa narudi.
Sema leo nitashtua kimoja kujipongeza kwa kuacha.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Una mpa mashart Dr. Kwa Afya yako? Na alijuaje? Au unaonesha kwa nje kama ni mzee wa kukaba nyoka?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Una mpa mashart Dr. Kwa Afya yako? Na alijuaje? Au unaonesha kwa nje kama ni mzee wa kukaba nyoka?
Ni Classmate wangu Advance, Ananijua na yeye mwenyewe ni bingwa, Alishaweka record siku ya Necta hata mimi siwezi ivunja, kwahio nammudu.
 
Ngoja nisome na mimi, wahanga ni wengi.

Mimi Suruali ni 31, mpk sio poa.
Japo mimi nipo stable, sishuki wala kupanda, nimezoeleka kwa mwili huu tangu tuu nilipoanza Advance.

Hii imekuja kuathiriwa zaidi ni ulaji wangu, pact moja ya karanga na Soda Nashiba kabisaaa, kuna mtu kaniambia hata kula yangu ya haraka haraka yaweza kua sababu,
Ni kweli hua nakula haraka na pia ni nadra sana nikala huku nimekaa, kwa ufupi Sijawahi Kua serious na chakula.

Mtaani wananiita Magrili, yaani kwenye dirisha la grili napenya vzr kabisa, mguu wangu na Square pipe ya grill havitofautiani sana,
Dr. Kanishauri nipunguze(suala la kuacha nilimuambia asiliwaze) nyeto. Ila nimeacha, ngoja nione, Nisipo nenepa narudi.
Sema leo nitashtua kimoja kujipongeza kwa kuacha.
[emoji2] kichwa chako. Nasema kama nilivyosema nilipomalza kucheka. Mwanzon umenitia simanz kidg kisha tena ukalabua.

Me mwenyewe nimesikia hawa wa Herbs wanatoa hiyo suppliment.
 
Uwe unafanya vipimo vya afya mara kwa mara. Kuna maradhi yakiwa mwilini hata ule vipi haunenepi ni kukonda tu.

Sema hamna mtu mwembamba kuna siku utanenepa tu. Mimi nilikuwa mwembambaa hadi sio poa ila nilivyoanza kufumuka hata niliosoma nao chuo wananiulizaga nimechoma sindano au vipi maana sikuwa na dalili ya kupata mwili siku moja
Sasaaaa,,,...wewe ni wa kikeee tatizo
 
Back
Top Bottom