Naomba ushauri juu ya dawa za kuongeza mwili

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,050
10,495
Kadri siku zinavyoenda wembamba wangu unazidi kunipa stress nilifikiri nikiwa mbaba nitaongezeka mwili ila imekuwa kinyume kadri siku zinavyoenda ndio nazidi kupungua.

kila nikikutana na mtu tunayefahamiana swali la kwanza kuniuliza mbona umekonda sana unaumwa?

Kinachoniumiza siyo kukonda ni usoni maana angle za fuvu zimeanza kuonekana kuhusu minyoo najitahidi kula dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu ila bado.

Leo nimetumiwa nauli nirudi Mkoani sababu ya wembamba wangu eti maisha ya mjini yamenishinda.
 
Uwe unafanya vipimo vya afya mara kwa mara. Kuna maradhi yakiwa mwilini hata ule vipi haunenepi ni kukonda tu.

Sema hamna mtu mwembamba kuna siku utanenepa tu. Mimi nilikuwa mwembambaa hadi sio poa ila nilivyoanza kufumuka hata niliosoma nao chuo wananiulizaga nimechoma sindano au vipi maana sikuwa na dalili ya kupata mwili siku moja
 
Ngoja nisome na mimi, wahanga ni wengi.

Mimi Suruali ni 31, mpk sio poa.
Japo mimi nipo stable, sishuki wala kupanda, nimezoeleka kwa mwili huu tangu tuu nilipoanza Advance.

Hii imekuja kuathiriwa zaidi ni ulaji wangu, pact moja ya karanga na Soda Nashiba kabisaaa, kuna mtu kaniambia hata kula yangu ya haraka haraka yaweza kua sababu,
Ni kweli hua nakula haraka na pia ni nadra sana nikala huku nimekaa, kwa ufupi Sijawahi Kua serious na chakula.

Mtaani wananiita Magrili, yaani kwenye dirisha la grili napenya vzr kabisa, mguu wangu na Square pipe ya grill havitofautiani sana,
Dr. Kanishauri nipunguze(suala la kuacha nilimuambia asiliwaze) nyeto. Ila nimeacha, ngoja nione, Nisipo nenepa narudi.
Sema leo nitashtua kimoja kujipongeza kwa kuacha.
 
Back
Top Bottom