Naomba niwaage

HAYA SAWA NDIYO
 
Mkuu Ushimen kama bado upogo naomba u LIKE uzi huu. Maana tangu Friday ulipotuaga hadi leo Tuesday upo kimya. Kama walau unapumua naomba u LIKE uzi huu mkuu. Pia nakutumia wimbo wenye ujumbe wa matumaini hivi punde.
 
Japo ulikuwa mtukanaji maahuhuri pole na Mungu akuponye ili tuwe pamoja tena ukiwa mtoto mpya usie mtukanaji
 
Naisi umekimbia amana wewe
 
Mkuu usiogope, najua ni changamoto ila inapitika, last two weeks nilikutana na mama mmoja wa tabata ambaye alikufa ghafla siku mbili baadae na ikaamuluwa mazishi yafanyike bila waombolezaji, baada siku chache nilipata dalili zote zinazotajwa, niliogopa sana moja kufa pili kuwaambukiza familia yangu, nilichoamua ni kujipa self isolation, nimejifungia chumbani natumia herbals pia navuta bangi to get self centred.
Chukua tahadhari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu una shida gani??
 
Ukifa mungu akupokee vyema.Ila tunaamini mungu hatokuacha uangamie atakuponya tuna utarudiku kujumuika nasi.Ondoa hofu kwani hofu ndio husababisha vifo vingi kuliko korona.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wakuu..... hata sasa niseme naendelea vizuri sana, na Mungu amenisimamia katika hili.
Asante kwa MAOMBI yenu yalio niinuwa.
Asante kwa michango na PM zenu zilizo nifariji na kunitia moyo.
Asante kwa comments zenu zilizo nijenga na kunitoa hofu pakubwa.
Asante kwa kuniweka mawazoni mwenu na kunijulia hali, najivunia zaidi nikisema mnanijali sana.
Asante kwa msaada wote ule mliotoa kwa ushauri na pia member ulie nitumia dawa.
Asante kwa kujumuika nami kimawazo na kiroho.
Asante kwa urafiki wenu.
Asante kwa upendo wenu.
ASANTE, ASANTE, ASANTE tena nasema ASANTE.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…