Whackiest
JF-Expert Member
- Sep 13, 2020
- 1,387
- 1,937
Leta chanya
Kama ameamua kuitumikia hiyo nafasi mwache aitumikie asiangalie hayo mengine c umeambiwa jamaa kaomba saana apate wakuzeeka nae! Ndo mungu akamuonyesha hivo...Leta chanya
Usije muua babu kwa presha bibi bomba wewe. 😀Aahahahahahahahaaaa mjukuu naweeeh, kama nawaona hapa wadao machokodoo na masikio popoo kusikia ntajibuje eeheheheheheheee
Acha niwarushe roho utamu 😛 😛
1. Hii habari ni ya kweli kabisaa mia ya mia, haina sukari wala ndimu ya nyongeza.
2. Naanzaje sasa kwa mfano, yule babu mwingine aahahahahahahaaa .......... tumeweka pozi tuuu 😀😀😉
Nisahihi kwa uonavy ww na mimi nilijion sahihi kwa uono wangu nilio jaliwa na sir GODKama ameamua kuitumikia hiyo nafasi mwache aitumikie asiangalie hayo mengine c umeambiwa jamaa kaomba saana apate wakuzeeka nae! Ndo mungu akamuonyesha hivo...
Il
Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Usije muua babu kwa presha bibi bomba wewe. 😀
Habari za jumapili,
Nahema kwanza maana.....! Maelezo marefu ila ntajitahidi kuyafupisha.
Jordan, mhusika leo ni Jordan. Huyu tulikuwa wote kombania moja 832kj Ruvu kwa miezi 3. Enzi zile jeshini ni lazima na unaenda kwa kipindi cha mwaka mmoja, na ndani ya mwaka mmoja unaweza ukahamishwa kutoka kikosi kimoja kwenda kingine kwa sababu kadha wa kadha.
Nakumbuka nilianzia makutupora na miezi mitatu ya mwisho nilimalizia hapo ruvu.
Jordan alikuwa sulule mwenzangu, alikuwa anapenda sana mziki kucheza na kuimba. Nakumbuka tukiwa tunakaribia kumaliza jeshi siku moja jioni alichukua mike na kuanza kuimba na akasema wimbo huu namuimbia sulule mwenzangu jina kapuni. Ila macho yote yalikuwa kwangu kipindi chote anaimba na kesho yake tukiwa tunachimba handaki aliniambia Kasie ule wimbo ni ombi langu kwako, niko tayari kutumika maisha yangu yote kwa ajili yako. Aidha tujaaliwe watoto ama tusijaliwe, wewe ndo chachu ya mimi kupambana kiume.
Nilikuwa nacheka tuu na kuchukulia mizaha hadi tukamaliza jeshi kila mtu akasambaratika kwake.
Jana sasa, nilikuwa na upako wa kwenda mziki, nikaenda mahala wanapiga live band na kuimba nyimbo zile za zamani. Nikawa kila wimbo nanyanyuka kucheza na nilikuwa pekeyangu, tabia mbaya na nzuri ya wanaume wa Dar wakimuona mwanamke yuko pekeyake basi wanajua ametega anatafuta kuvuliwa. Nikawa wengine nakubali kucheza nao wengine nakataa nacheza mwenyewe tuu.
Saa isiyo na jina nasikia sauti ya tofauti kwenye kipaza sauti kugeuka jukwaani ni Jordan looh..... ananiimbia..... huku akinitizama....
Naomba lao nipate nafasi ......
Niliishiwa stimu zote, nikajikuta nasimama sikucheza bali nilirudi kwenye kiti na kumuangalia mwanzo mwisho anavyoimba. Alipomaliza alikuja kukaa kwenye kiti changu, tukasalimiana nikamwambia naomba niondoke, akaniambia iwapo tuu utanikubalia ombi langu la kunipa nafasi kwenye moyo wako......
Jordan alioa akapata watoto 2, ambao saa hizi wote wako chuo ila mkewe alifariki baada ya kujifungua mtoto wake mdogo na tangu hapo alijikita kulea wanae hakuoa. Akaniambia watoto wake walipoingia chuo tuu akamuomba mungu ampe mwanamke wa kuzeeka nae. Ni mwezi sasa tangu aanze kuomba na jana kaonana na mimi, anaamini Mungu kamuonesha mimi ndo wa kuzeeka nae.....
Jordan, Jordan, Jordan.....
Ni kitambo kirefuu tangu tupotezane 832kj ruvu, Moyoni naumia eeehhhh...
Hata sielewi........... ila kama ni mpango wa Mungu, itakuwa tuu.
Kasinde Mahaba.
Woyooooo😂😂😂😂Muelekeo ndo unaelekea huko, tuombe uzima inshallah tutaanza kuzeeshana utasikia....
Jordan: Kasie naomba miwani yako nisome gazeti sijui miwani yangu nimeiweka wapi.
Kasie: Eeeh Jordan nawee haya chukua usiivunje tuu, sasa hapa nimekaa naona magoti yananiuma ngoja nikakutafutie miwani yako chumbani. Niazime mkongojo wako nideme nao maana magoti nayo yashakufa.
Kuzeeka pamoja raha sana aahahahahaaaa Jooorrrdaaaaaaannnnnnnn......!!!
Mkuu mwajuma huyu tuliekuwa tunamuimba kwenye machenja au yupiNami namtafuta Mwajuma tulipotezana 823KJ........