Naomba Munitambue JF

Naomba Munitambue JF

Kalamunzu

Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
5
Reaction score
2
...Jina langu (la kalamu) naitwa Kalamunzu dia Zinguku. Nimezaliwa mwaka 1938, tarehe 2 mwezi wa sita (Juni) katika kisiwa cha Bermuda (kwenye pembetatu). Si kawaida sana kwa sisi watu wa Bermuda kujitambulisha kwa maija ya kalamu, isipokuwa kwa vile tumekuwa tukiandamwa sana na mfumo wa kifisadi hata kutishia maisha yetu; ndio maana tunalazimika kutumia majina ya kalamu ili kuficha utambulisho wetu halisi.

Nimemaliza masomo ya udaktari wa falsafa katika elimu jumla (general knowledge) na kubobea katika elimu nafsi na siasa-uchumi. Najishighulisha na kazi za kilimo cha matikiti maji (water melons) katika viunga vya mji mkuu wa Bermuda. Nina uwezo wa kuzungumza lugha tano (5) za kujifunza: Kiswahili, Kifaranza, Kingazija, Kiarabu, na Kiajemi. Vilevile, lugha ya mama ni ki-Bermuda.

Naomba ushirikiano wenu wanaJF.
 
Kalamunzu nimekutambua tayari na nimekupenda ghafla,,karibu sana
 
Intro yako nimeipenda, karibu tushee uzoefu
 
ingia ndani mkuu,hii ndo JF kipimo cha uvumilivu
 
Naitwa venance kiloti nimwana harakati mdogo naepinga ufisadi naomba mnitambue
 
Mambo vp mko poa wana JF, MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA AU NI UMASIKINI KWA KILA MTANZANIA? Tujitume ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom