Naomba mshahara wa Rais upandishwe uwe kama zamani

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Kwanza napenda kumpongeza mama yetu mpendwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya.

Kitu kingine ningeomba sana mshahara wa Rais upandishwe tena uwe angalau kama enzi ya Rais Kikwete.

Magufuli alijishushia mshahara lakini lazima tujiulize, je alikuwa anauhutaji? Kwa kuanza tu mpwa wake ndiye aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya fedha.

Pili, kampuni ya Mayanga Construction ni ya mtu ambaye alioa naye nyumba moja na ndiyo iliyopewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Chato. Lazima pia ikumbukwe zabuni ya hiyo tenda haikutangazwa kwenye vyombo vya habari na wala pesa ya mradi kuidhinishwa na bunge.

Kwa mfano tunapata Rais bilionea akajipunguzia mshahara, je hii ni haki kwa Rais ajaye? Kumbuka kwamba nimesema kuwa nafikiri Magufuli alikuwa hahitaji pesa za mshahara.
 
Sheria nzuri za mishahara ni kuwa hutakiwa kupangwa kabla mtu hajaingia kwenye kiti. Najua wakati mshahara wa Rais wa Marekani ulipoandishwa kutoka dola laki mbili kuwa laki nne ilikuwa ni wakati wa rais clintoni, lakini yeye aliendelea na ule mshahara wa laki mbili hadi Bush alipoingia ndipo akaanza kupokea laki nne.

Ukiruhusu mtu aliyeko madarakani apandishiwe mshahara, unaweza kuruhusu mtu mwingine akingia madarakani na kubadilisha mshahara wake kuwa kama robo ya bajeti ya serikali.

Swala hili niliwahi kulialamikia zamani sana hapa JF takriban miaka kumi iliyopita pale wabunge wetu walipojipangia mishahara na posho kubwa halafu kweli ikawa hivyo.
 
Unaacha kufikiria vitu vya maana unafikiria mshahara wa mtu ambaye hajakuomba hata pesa ya vocha, wakati kuna wastaafu wanadai mafao yao, kuna watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara, kuna vijana tele hawana ajira, upatikanaji wa umeme tu umekua tatizo tunakatiwa kila muda tena bila taarifa, n.k,

Halafu unakuja kupandisha mabega hapa, "Naomba mshahara wa Rais upandishwe kama zamani"
 
sheria nzuri za mishahara ni kuwa hutakiwa kupangwa kabla mtu hajaingia kwenye kiti. Najua wakati mshahara wa rais wa marekani ulipoandishwa kutoka dola laki mbili kuwa laki nne ilikuwa ni wakati wa rais clintoni, lakini yeye aliendelea na ule mshahara wa laki mbili hadi Bush alipoingia ndipo akaanza kupokea laki nne...
Umeongea vizuri lakini kumbuka rais aliyepita alijipunguzia mwenyewe akiwa madarakani. Kwa mfano tunapata rais bilionea akajipunguzia mshahara, je hii ni haki kwa rais ajaye? Kumbuka nimesema kuwa nafikiri Magufuli alikuwa hahitaji pesa za mshahara.
 
.
salehjembefacts-20210406-0001.jpg
 
Yaani watu hatujapandishwa mshahara tangu enzi za Kikwete wewe unamfanyia kampeni Rais kuongezwa mshahara...
 
Unaacha kufikiria vitu vya maana unafikiria mshahara wa mtu ambaye hajakuomba hata pesa ya vocha, wakati kuna wastaafu wanadai mafao yao, kuna watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara, kuna vijana tele hawana ajira, upatikanaji wa umeme tu umekua tatizo tunakatiwa kila muda tena bila taarifa, n.k,

Halafu unakuja kupandisha mabega hapa, "Naomba mshahara wa Rais upandishwe kama zamani"
Watu wa namna hiyo mawazo yao huwa yanatikea kwa nyuma na sio mbele,
Maisha yao ninkujipendwkeza kwa vitu visivyowapa faida yoyote.
Raisi akupandishiwa mshahara yeye atapata faida gani?
 
Kwanza napenda kumpongeza mama yetu mpendwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya.

Kitu kingine ningeomba sana mshahara wa Rais upandishwe tena uwe angalau kama enzi ya Rais Kikwete.

Magufuli alijishushia mshahara lakini lazima tujiulize, je alikuwa anauhutaji? Kwa kuanza tu mpwa wake ndiye aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya fedha.

Pili, kampuni ya Mayanga Construction ni ya mtu ambaye alioa naye nyumba moja na ndiyo iliyopewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Chato. Lazima pia ikumbukwe zabuni ya hiyo tenda haikutangazwa kwenye vyombo vya habari na wala pesa ya mradi kuidhinishwa na bunge.

Kwa mfano tunapata Rais bilionea akajipunguzia mshahara, je hii ni haki kwa Rais ajaye? Kumbuka kwamba nimesema kuwa nafikiri Magufuli alikuwa hahitaji pesa za mshahara.
Another imbecile, Pima akili yako,
 
Mshahara haujawahi kupunguzwa, ni yeye alitamka kizalendo mshahara wake ukatwe (kama ni kweli ulikatwa) ila hakusema ndo mshahara wa Rais.

Ni kama Donald Trump alivyosema atachukua mshahara $1 (sina uhakika) kwa mwaka.

Ni yeye binafsi.
 
Aisee Mara ya mwisho ulionana na daktari lini? Nashauri ukalime akili yako, it possible una fuvu la fisi. Haitaji mshahara, kila kitu ni bure kwake all pay Inala tu benki plus maruprupu ya mikatabs. Ana mabillioni wewe kuku.
 
Huwa siwezi kujadili lolote na watu wa aina yako, ila kwa leo naweza kukupa ushauri wa bure ukufae maishani…. ilimradi usikaze fuvu.

Subiri shule zifunguliwe uwahi MEMKWA ujifunze japo kuandika, kwa busara nitakuvumilia hadi urudi kisha tutaona kama tutaweza kujadili lolote.

Until then, kwa sasa nachagua kukupuuza tu…. ukiitwa MPUMBAVU uwe unashukuru.
 
Back
Top Bottom