gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Salaam,
Mara kadhaa nimekua nikikutana na mtindi ambao unagandishwa kwa njia za kawaida kabisa humu mitaani,naita njia za kawaida kwasababu mtindi huu hauhitaji mitambo kama mtindi wa viwandani mf tanga fresh ambao unakua na vihifadhi(kemikali) na michakato mengine yakiviwanda.
Japo mtindi huu unachakatwa kwa njia za kawaida lakini test yake ni nzuri mno pengine kuliko hata ule wa viwandani.
Licha ya uzuri wake lakini pia bei yake ni cheap kwani maandalizi yake hayatumii gharama kubwa kama ule unaotengezwa viwandani hivyo ni fursa nzuri kibiashara.
Nimejaribu kufuatilia namna unavyoandaliwa lakini watengenezaji wamekua wasiri kutoa hii elimu.
Kwa hatua za awali wanaanza kuchemsha maziwa na yakisha chemka huyaipua na kuyaweka kwenye vyombo vipana vya wazi na kisha kukoroga kuhakikisha hayaweki utandu(creem) kwa juu mpaka yatakapo poa.
Changamoto inaanza kuanzia hapo kwani ugandishaji hufanyika kwa vificho kwakujifungia ndani tena kwa usiri mkubwa.
Lakini nimepata fununu wakiwa ndani kuna kitu wanachanganya kinaitwa culture.
Kwa maelezo hayo naomba mwenye ufahamu na hili atusaidie,
Thanks.