Naomba msaada wa mawazo, mdogo wangu ni kichaa

Naomba msaada wa mawazo, mdogo wangu ni kichaa

Kuna maswali machache hapa

Kama alikua kipanga sana class basi amelogwa .....mpeleke kanisani kwenye maombi heavy.......au muone MSHANA JR

Hapo kwenu hamna mwenye utajiri wa fasta kwa siku hizi za karibuni?

Nadhani Kuombewa ni suluhisho sahihi.nimeshawahi kuwa na kicha kwen
Poleni ndugu watanzania na majukumu ya kila siku,poleni na tozo na maumivu ya kushikiliwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Nasisitiza Mbowe Siyo Gaidi...
Pole sana mkuu.Najua hali mnayoipitia.Nimeshawahi kulea kichaa kwenye familia yangu.Ni hivi,kama unadhani hicho kichaa ni cha kulogwa/nguvu za giza nenda kwenye maombi.ANGALIZO.ukienda kwenye maombi kunahitaji imani na uvumilivu.anaweza akafunguliwa siku hiyo hiyo au ikachukua muda kiasi,kwa sababu inaweza ikahitaji kushughulika na mizizi ya hilo tatizo, mfano.Maagano ya kifamilia (usiyoyajua) yakivunjwa hayo na kichaa kinaishia hapo.muwe wawazi kuwaeleza watumishi historia ya huyo kijana na familia yenu kwa ujumla.

Ila kama unadhani ni mambo ya kisaikolojia nenda mhimbili.

Musiende kwenye waganga wa kichawi/kienyeji.watawatapeli na kuwafarakanisha nyinyi kwa ninyi.pepo huwa hawezi kumtoa pepo mwenzie anachoweza kufanya ni kumtuliza tuu kwa muda

Kwa vyovyote vile mnahitaji kushikamana ili mmsaidie mwenzenu
 
Kalogwa,

Katupiwa jini.

Umekutana na tiba asili ambao ama ni matapeli au uwezo wao ni mdogo.

Kama upo mwanza nenda ukerewe huko utakutana na magwiji watamtibia
 
Mpeleke Kwa mbowe sio haidi........uko lazima atapata Tu Tiba sahihi...
 
POLE SANA. HUJASEMA YUKO MKOA GANI.
INAWEZEKANA AKAPONA KABISA KAMA MKIMUWAHISHA HOSPITALI YA MILEMBE .
KULE ATAPEWA TIBA NZURI TU NA ATAPONA.
NINANDUGU YANGU ISHAWAHI KUMTOKEA ALITIBIWA MILEMBE NA SASA YUKO POA
ANATUMIA DAWA NA KUFATA USHAURI WA MADAKTARI.
 
Kama uko Dar basi kuna Hospitali zenye vitengo vya kuhudumia watu wa namna hiyo hivyo atapata matibabu..kuna Muhimbili moja wapo..

Kubwa ni matibabu huku ukimtegemea sana Mungu atamponya..

Pole sana!!
Hapana mkuu.....unavo anza kusolve tatzo lazima ujue chanzo
 
Una uhakika hatumii kabisa bangi/madawa ya kulevya?
One of my close family member alishawai kukutwa na hiyo challenge katika umri huohuo was around 23 tukadhani ni psychological problems kumbe alianza kutumia hizo mambo kutokana na bad influence kutoka shule.
Yeye alikataa katakata kwamba hajawahi tumia lakini baada ya kuchunguza Sana tukagundua anatumia hizo vitu. Alipelekwa hospital na akawa anatumia dawa anarudi nyumbani anakuwa sawa kwa muda lakini akipata chance tu ya kwenda sehemu bila kuchunguza akirudi baada ya muda kuchanganyikiwa kunarudi, tukaja kugundua anakoenda anaenda kuchukua bangi na kuvuta kwa Siri.
Ilikuwa ngumu kumdhibiti ila tulifanikiwa mpaka akawa vizuri kabisa.
Kwaio chunguza vizuri makundi au marafiki zake, wanajua ila wanaogopa kusema.
Msimruhusu kutoka kwenda sehemu yoyote bila uangalizi akiwa anatumia dozi maana huko ndo anakoenda kuharibu dozi kwa kuingiza madawa mengine.
Ondoeni imani za kishirikina Kwanza pambaneni na kuhakikisha anapata dozi kwa muda unaopaswa na chakula Cha kutosha kulingana na ushauri wa wataalam
 
Pole sana sana kwa hii changamoto unayopitia.. Kuna mdau hapa nitamshirikisha kisha tuone namna ya kumsaidia mgonjwa.
Mkuu mshana mm pia Nina mdogo ana tatizo kama hilo tushampeleka sana muhimbili wanamlaza wiki akitoka wanampatia vidonge vya kutumia nyumban baada ya muda kidogo hali inarejea tena, imekuwa ndio kawaida sasa nyumban - muhimbili , msaada mkuu
 
Korogwe kuna hospital ya lutindi ina deal na mental case jaribu kwenda ni bora
 
Pole sana nje ya mada kwenye hiyo avatar huyo kaka namjua anaitwa kombo naye ni kichaa je ndio huyo mdogo wako
 
pole sana ndugu mm mwenyew mzee wangu anasumbuliwa na hali hii tangia 2009 tulimpeleka hospitali rufaa mbeya.alichomwa sindano ya usingiz alilala usingz kalibu siku mbili.baada ya hapo akawa vizuri tangia hapo anatumia dawa aina ya vidonge anatumia kila siku anapoenda kulala mpaka sasa yuko vzuri tu
 
Back
Top Bottom