Naomba msaada wa mawazo, mdogo wangu ni kichaa

Mbwichichi

JF-Expert Member
Dec 19, 2018
267
1,331
Poleni ndugu watanzania na majukumu ya kila siku,poleni na tozo na maumivu ya kushikiliwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Nasisitiza Mbowe Siyo Gaidi.

Hongereni kwa kupokea chanjo ya corona, Mimi nimeshachanja.

Straight to the point,nina mdogo wangu wa miaka 25 sasa hivi,miaka mitano iliyopita akiwa kidato cha nne alianza kulalamika anasumbuliwa na kichwa na homa za mara kwa mara,hali hii ilikua inamtokea mara kwa mara na alianza kuongeaa maneno yasiyoeleweka kwa wakati fulani ila kuna wakati anakaa vizuri...ilipelekea hadi kushindwa kufanya vuzuri kwenye mtihani wake wa kidato cha nne pamoja na kwamba kabla alikua ni mwenye uwezo darasani kuliko wanafunzi wote.

Baada ya matokeo kuwa mabaya ni kaa alichanganyikiwa mazima sababu alikua haeleweki completely,kule kuumwa kichwa pamoja na kuweweseka kukawa sasa ni parmanent,ni akawa kama kichaa rasmi,tulijaribu tiba mbalimbali za asili na za kisasa llakini hii hali haijataka kmtoka hadi sasa naandika hivi tuko naye nyumbani,keshakua ni mchafu sana..analeta kila aina ya taka nyumbani na uzuri nyumbani anapakumbuka.

Kuna wakati mnaweza ongea naye ila kikimpanda basi anaharibu kila kitu,anazidi kukua sasa na keshaanza kuonyesha dallili za kutaka mapenzi toka kwa wanawake na hapa nyumbani tu watoto wa kike..hofu ni kwamba asije wabaka siku moja.

NAOMBA MSAADA KUNISHAURI NICHUKUE HATUA GANI?,ANAYEJUA TARATIBU ZA KUWASAIDIA HAWA ANISHAURI TAFADHALI,sababu roho inauma sana kumtelekeza mazima akawe wa mtaani sababu ni ndugu,lakini pia umri wake unasonga na mahitaji yake ya kimwili yanaweza kuleta madhara makubwa zaidi.

Nilisikia kuna vituo vya kuwalea,Milembe n.k...naombeni mwenye chochote cha kunishauri tafadhali,naumia sana.

Mbowe Siyo Gaidi.
 
Pole sana, kwanza usimuite mdogo wako kichaa.

Ni maradhi ya akili,

Je ana matibabu anaendelea nayo kama dawa za kumeza kila muda au wakati anakuwa hajisikii vizuri.

Najua umejaribu hospitali, lakini nakushauri urudi tena hospitali, na kama upo Dar es salaam, nenda Muhimbili, watakushauri kama anahitaji rufaa ya hospitali husika.

Usikate tamaa, inaweza kuwa ni ya muda tu, kwa sababu kwa vijana kuna wanaweza kupitia kitu inaiitwa schizophrenia inayoaanzia miaka ya 20 - 30
 
Poleni ndugu watanzania na majukumu ya kila siku,poleni na tozo na maumivu ya kushikiliwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Nasisitiza Mbowe Siyo Gaidi...
Pole sana na Mungua amjaalie apate afueni. Umesema hsptl mlikwenda lakini hujasema kama mlikwenda kitengo maalumu cha magonjwa ya akili. Kama hamjawaona wataalamu mabingwa wa kitengo hicho muwaone tafadhali.

Ni changamoto kidogo, wengi wetu huwa hatupendi kuwapeleka huko maana kama tatizo si kubwa, ni kama unamtosa nduguyo gerezani. Lakini kwa kesi yake, hunabudi kuwaona wataalamu wa akili. Kama upo Dar nenda Muhimbili. Wao watakuelekeza cha kufanya ,kama ni kesi ya Milembe ama la.
 
Poleni ndugu watanzania na majukumu ya kila siku,poleni na tozo na maumivu ya kushikiliwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Nasisitiza Mbowe Siyo Gaidi...
Anzia eneo ulipo kama kuna taasisi inaweza kumsaidia.
 
Haina haja ya kumpeleka milembe sababu kubwa ya yeye kia hivyo si madawa ya kulevya hivyo ni msongo wa mawazo na changamoto alizopitia kushindwa kuzihimili' kama uko dsm nenda muhimbili hospital wana kitengo kinacho husika na haya magonjwa' Binafsi nina ndugu yangu nae shida ilikua kama yake ila yeyeni wa kike' tulianzia mwananyamala pale wakamhamishia muhimbili akafanyiwa counseling pamoja na dawa akawa sawa kwa kiasi na bado ana dozi ya dawa anatumia asubuh na jion ingawa tunaomfahamu bado tunaona utofauti kiasi ila imemsaidia pia family kumjali na hizo dawa ndo inampa kupona haraka zaidi. In Time kila mtu anaweza kupatwa na hizi hali.
 
Back
Top Bottom