Naomba msaada wa makazi Dar es salaam

city center

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2018
Posts
212
Reaction score
271
Habari za muda huu mabibi na mabwana!

Natumai mu wazima wa afya

Samahani kama bandiko hili haliko sehemu sahihi

Mimi ni kijana wa kiume (miaka 29, sijaoa), mwenyeji wa mkoa wa Mwanza.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikitafuta ajira bila mafanikio lakini mwezi huu nimepata kibarua kidogo cha kunisogeza mbele, ndani ya jiji la Dar.

Wakuu,
Shida inakuja sasa sina uwezo wa haraka wa kulipia chumba kwa ajili ya makazi.

Hivyo basi,
Nipo hapa kuomba hifadhi ya muda kwa mtu atakaekuwa na uwezo niweze nifadhili nipate pa kukaa wakuu angalau kwa mwezi mmoja wakati nikingoja mshahara wa kwanza ili niweze kupanga.

Nipo tayari kuchangia kiasi cha pesa kwa ajili ya maji na umeme.


Taarifa zangu binafsi

Jinsi; Me, mrefu, mweusi

Asili: Mara (serengeti District)

Umri; 29 y.o, sijaoa

Kilevi: situmii kwa sasa, sio mtokaji sana





Samahani kama nitawakwaza kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mkuu umenihukumu sana

Nimetoa taarifa zaidi ili niweze kusaidiwa na kuondoa some doubts

Equation x alishajitoa kunisaidia lakini makazi yakawa mbali sana mpaka kufika city center (ama mikocheni ambako ofisi ipo)

Msaada wako bro kama inawezekana
Kimsingi unatafuta sugar mummy, maana sijaona swala la kuandika maumbile yako kama lengo ni hifadhi tu. Endelea kujiuza

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi ofisi waliyokupa Ajira hawakuzingatia wapi utaishi kwa wakati huo, na je huna Ndugu hata jamaa huko mjini Dar es Salaam,

Lakini pole sana Kamanda Maisha ni mkusanyiko wa matukio na ni safari pia usijali sana
 
Vipi ofisi waliyokupa Ajira hawakuzingatia wapi utaishi kwa wakati huo, na je huna Ndugu hata jamaa huko mjini Dar es Salaam,

Lakini pole sana Kamanda Maisha ni mkusanyiko wa matukio na ni safari pia usijali sana
Ndugu yangu ofisi za siku hata hazizingatii hasa dunia ya sasa nafasi moja ya kazi inagombaniwa na watu laki moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…