Naomba msaada wa kutatua tatizo la rejeta kwenye Subaru Impreza

Jul 28, 2020
38
49
Wakuu nawasalimu pamoja na mko bize kufuatilia kesi mbali mbali zinazoendelea kwenye mahakama mbali mbali naomba ushauri wenu kwa wazoefu ninatumia subaru impreza kwenye mizunguko yangu ila hivi karibuni imekuwa na tatizo kwenye rejeta maana kila nikienda kwenye mizunguko lazima nikute imekausha maji.

Hivyo nina kazi ya kujaza karibu kila siku na nimeshaenda kwa mafundi walisema inavuja wakaziba ila tatizo likaendelea bado nikarudi tena wakaitoa wakadai waisafishe lakini tatizo bado lipo nimeamua sasa niwe najaza maji tu naingia mtaani naomba msaada wenu wajuzi wa haya mambo.
 
Kwanza uko wapi?
Pili kama unaweza badilisha hiyo rejeta kabisa,kama uko dar unaweza kunicheki nikupe msaada
 
Umejaribu kucheck mfuniko wa rejeta kama vile vipira vipo vizuri (raba seal hazijakauka au kuharibika)?

Jaribu kubadili mfuniko kama hujafanya hivyo...
 
Wakuu nawasalimu pamoja na mko bize kufuatilia kesi mbali mbali zinazoendelea kwenye mahakama mbali mbali naomba ushauri wenu kwa wazoefu ninatumia subaru...

Kuna waarabu Wapo Ilala hapo, naamini Ni namba Moja Kwa issue na wana spare zote, watakuwa na connection na mafundi wazuri wa Subaru!

Nakuhakikishia Hakuna Fundi anayesema hajui Tanzania, jitahidi kukutana na mtu Mwenye uzoefu na gari Hilo Hilo
 
nashukuru mkuu maana hata hao niliwapelekea walichukua siku nzima wakasema tatizo limeisha ila mambo yako vile vile
 
Wakuu nawasalimu pamoja na mko bize kufuatilia kesi mbali mbali zinazoendelea kwenye mahakama mbali mbali naomba ushauri wenu kwa wazoefu ninatumia subaru impreza kwenye mizunguko yangu ila hivi karibuni imekuwa na tatizo kwenye rejeta maana kila nikienda kwenye mizunguko lazima nikute imekausha maji hivyo nina kazi ya kujaza karibu kila siku na nimeshaenda kwa mafundi walisema inavuja wakaziba ila tatizo likaendelea bado nikarudi tena wakaitoa wakadai waisafishe lakini tatizo bado lipo nimeamua sasa niwe najaza maji tu naingia mtaani naomba msaada wenu wajuzi wa haya mambo
Wacheki hao jamaa, ni wataalamu wa mambo ya rejeta wako Buguruni Malapa. Wanasafisha, wanamodify na pia wanaunda! Mimi walinisaidia.
 
Kwa uzoefu hio gari itakua inapoteza maji pia mkuu kwenye radiator ya gari hautakiwi kuweka maji wewe weka coolant..ukiendekeza kuweka maji inakuja kuota kutu kwenye oil cooler na mbeleni huko block inaliwa na kutu...mara nyingi kama umetatua tatizo la radiator bado gari inaendelea jaribu kuangalia kwenye cylinder head unaweza kuta inatakiwa ipigwe pasi. .
 
nashukuru sana mkuu
 
Back
Top Bottom