Naomba msaada wa kufika bungeni

Naomba msaada wa kufika bungeni

Tanzania haina bunge, lile ni kundi la makada wa CCM waliojipa madaraka kwa damu na bunduki October 29.

Wewe ni kijana mdogo jiepushe kuungana na wauaji.
 
Habari wana JamiiForums.

Nina ombi la dhati. Mimi ni kijana wa miaka 21 kutoka Tanzania, na moja ya ndoto zangu kubwa ni kupata nafasi ya kutembelea Bunge la Tanzania na kushuhudia kikao cha bunge nikiwa kwenye jukwaa la wageni.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya bunge kwa muda mrefu, na nina hamu kubwa ya kujifunza namna shughuli za kutunga sheria na uwakilishi zinavyofanyika kwa karibu.

Kama kuna Mbunge, mtumishi wa Bunge, au mtu yeyote mwenye uwezo wa kunielekeza au kunisaidia kupata kibali cha kutembelea bunge, nitashukuru sana. Itakuwa hatua kubwa kwangu kutimiza ndoto ambayo nimekuwa nayo kwa muda mrefu.

Asanteni sana kwa muda wenu na kwa msaada wowote mtakaoweza kunipa.
Kama unataka kwenda kuona jengo la bunge (kutembelea eneo la bunge) ni sawa, kesho napita Dar usiku nikitokea Kusini, ninaweza kukupa lifti, ila kama unaenda kuona utungaji wa sheria na uwakilishi, hilo nakushauri uachane nalo na sitakusaidia, kwani kwa sasa hatuna bunge (hatuna wawakilishi wa wananchi wala hatuna watunga sheria)..
 
Naunga mkono hoja miaka 21, joined 2019 ina maana alijiunga JF akiwa na miaka 15?, alafu huu uziumepangiliwa vizuri hivi hamna (xaxa), nukta zimekaa mahala pake.
Huyu anatuchora sio bure
Mimi nina mjukuu yupo grade 7 anatumia Jamii Forum kama guest tangu akiwa grade 5.
 
Habari wana JamiiForums.

Nina ombi la dhati. Mimi ni kijana wa miaka 21 kutoka Tanzania, na moja ya ndoto zangu kubwa ni kupata nafasi ya kutembelea Bunge la Tanzania na kushuhudia kikao cha bunge nikiwa kwenye jukwaa la wageni.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya bunge kwa muda mrefu, na nina hamu kubwa ya kujifunza namna shughuli za kutunga sheria na uwakilishi zinavyofanyika kwa karibu.

Kama kuna Mbunge, mtumishi wa Bunge, au mtu yeyote mwenye uwezo wa kunielekeza au kunisaidia kupata kibali cha kutembelea bunge, nitashukuru sana. Itakuwa hatua kubwa kwangu kutimiza ndoto ambayo nimekuwa nayo kwa muda mrefu.

Asanteni sana kwa muda wenu na kwa msaada wowote mtakaoweza kunipa.
Tafuta shamba ulime... Utanishukuru!
 
Kusoma na kuelewa limekuwa janga la kitaifa siku hizi.

Wabunge wote wana Ofisi majimboni na kunakuwepo Katibu wake hapo!!
Unaweza kupiga picha walahu ofisini kadhaa za wabunge mkoani kwenu?
 
Back
Top Bottom