Naomba Msaada: Ndoto hizi zimenitisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Msaada: Ndoto hizi zimenitisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hardwood, Jun 29, 2011.

 1. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  Heshima kwenu wote!!

  Nimeamua kuomba msaada humu jamvini baada ya kuota ndoto za ajabu kwa siku mbili mfululizo (juzi na jana) zote zikiwa zinahusu wanyama wa porini. Ndoto ya kwanza ilikuwa hivi: Nilijikuta niko juu ya mlima mrefu sana(ndivyo ndoto ilivyoanza hivyo) na ghafla nikawa na shauku ya kushuka mlima ule maana mazingira yale yalinitisha sana. Nilipoanza safari ya kushuka mlima ghafla nikakutana na wanyama wawili ambao ni Dubu na mwingine kama Mbwa mwitu wote wawili wakanivamia na nikaanza kupambana nao. Ghafla nikaanza kupaa kama ndege (huku mbawa zikiwa ni mikono yangu mwenyewe). Wale wanyama wiwili wakawa wanatafuta namna ya kunishusha chini huku wakitoa sauti za ukali sana. Kwa jinsi walivyokuwa wanapigana vikumbo wao kwa wao, Dubu akakasirika na akamgh'ata Mbwa mwitu miguu ya nyuma na ndipo Mbwa mwitu akaishiwa nguvu na Dubu akapambana peke yake. Nikajikuta napaa kwa nguvu hadi kumwacha yule Dubu akiwa na hasira sana. Nikaendelea kushuka mlima na ghafla nikakutana na kundi la Tembo. Mtoto wa tembo akanifuata kwa shari nikamshika mkonga wake kumzuia asinizuru na ghafla akadondoka chini. Mama wa tembo akanifuata kwa hasira kali ajabu na ghafla nikaanza kupaa tena(mbawa zikiwa ni mikono yangu mwenyewe). Yule tembo akanyanyua mkonga wake juu kabisa hadi akanigusa nikiwa angani ingawa alishindwa kunishusha chini!!! Ugomvi ulikuwa wa kutisha sana na niliogopa sana. Baadaye nikajikuta napaa kwa kasi na kumwaccha Tembo yule na ule uwezo wa kupaa ukaniishia nikawa natembea kwa kwaida. Nikaendelea na safari hadi nikafika chini ya mlima bila ya kukutana na kizuizi kingine. Ndoto ikaishia hapo.

  Jana usiku nikaota ndoto nyingine: Nipo katikati ya pori nene lililojaa wanyama wakali. Ghaafla nikakutana na Simba na akanivamia nikaokota fimbo pembeni nikaanza kupambana nae hadi nikamuua!!! Ghafla nikaona kundi la Simba wanakuja kwa mbali na njia wanayoijia ndio hiyo hiyo ninayoiendea, nikjawa na woga sana lakini ghafla nikamuona mtu ninayemfahamu yupo pembeni ya njia ileile huku naye akiwatazama Simba wale wakija kwa mbali. Akanipa ushauri kwamba tujifiche nyuma ya kichaka kilicho karibu huenda tukapona. Sikuwa na shaka naye maana namfahamu vizuri nikakubali tukajificha nyuma ya kichaka kile. Wale simba walipita huku wakitoa mingurumo ya hasira kali sana. Baada ya muda kidogo nikiwa nimeshaachana na yule mtu nikaendelea na safari yangu ghafla nikaona kundi la tembo wengi sana wakija kwa njia ileile ninayoiendea!!! Nikaona mtu anapita na gari lenye sura ya nyumba, nikamwambia wewe huogopi kundi lile la tembo wanaokuja mbele yako? Akatazama mbele akawaona wale tembo naye akaogopa sana. Akasimamisha gari lake pembeni lakini akagoma kunipa hifadhi ili tembo wale wapite kwanza!!! Ndipo nikajificha chini ya gari yake pasipo yeye kujua hadi wale tembo walipopita....walikuwa tembo wengi sana sana!!! Ndipo nikaendelea na safari yangu nikafika kwenye kidaraja fulani ambacho ndicho kinachotenga pori hilo na kijiji fulani. Nikaingia ndani ya kijiji hicho na watu wa sehemu ile ni watu watulivu sana na wala sikuona shari yoyote baada ya hapo. Ndoto ya pili ikaishia hapo.


  My concern
  Kiimani (Be it Islam or Christian) ndoto yoyote ile ina maana yake. Kwahiyo jambo hili nimeliieta jamvini ili kuomba msaada wa possible interpretation ya ndoto hizo. Ningependa mtu akitafsiri ndoto hizo atoe clear framework kulingana na muongozo ya dini yake juu ya masuala ya ndoto(atoe reference ya kifungu husika kutoka kwenye maandiko matakatifu ya dini yake). Please wanajamvi nawasilisha for solution
  .
   
 2. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Bwana yu nawe. Majaribu yatajitokeza ofisini pako, yatakuwa ni makubwa sana. Utateseka. Lakini watesi wako watageukana na hakika utainuliwa juu na utayashinda
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  ndoto mbili hazina Tatizo zikifika tatu za aina hiyo nijulishe
   
 4. f

  fikiriakwanza Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndoto ni bayana,biblia imejaa ndoto kibao,farao aliota yusuph akatafsiri,mfalme wa babeli aliota juu ya sanamu yenye chuma,shaba,udongo etc,yusuph baba yake Yesu alioteshwa kuhusu Herode kumwangamiza mtoto hivyo akimbilie misri.Hivyo ndoto ni jambo halisi na la kweli,Babu Loliondo aliota na wengine wengi,Luther King etc.
  Tafsiri ya ndoto yako ni kuwa kuna mambo yatakukuta ktk njia zako i.e kazini,ktk biashara au kwenye familia yako ila utashinda.Yakupasa kukaa kwenye maombi ili Mungu akupe nguvu za kupitia katika vikwazo hivyo salama
   
 5. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Sijui unafanya kazi gani, inawezekana ukawa askari wa wanyama pori ndio maana ndoto hizi zinakuijia mara kwa mara, mimi sio mzoefu wa kutafsiri ndoto lakini mfano, mabawa ama tendo la kupaa hewani ni alama ya kuwa huru, simba na mbwa mwitu ni alama ya maadui, tena kama huyo mbwa mwitu ni mbaya sana. kwa maoni yangu ni kwamba hili ni kama onyo kwako kama walivyosema hapo wengine kwamba inawezekana ikawa ni kuhusu kazi , biashara , n.k
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,116
  Likes Received: 6,598
  Trophy Points: 280
  Anyway, unatakiwa kufanya maombi sana kwa imani yeyote ile omba sana ili kuvunja hiyo hali hiyo, kama vipi tafuta na wanajamvi kwa imani zao wafunge na kuomba kwa ajili yako.
   
 7. Beautiful Lady

  Beautiful Lady Senior Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utakutana na matatizo mbalimbali, na adui wengi katika maisha yako.lakini utawashinda wote na hata maadui watageuka na kushambuliana wao kwa wao.watu utakaotegemea wakusaidie hawatatoa msaada wowote. Lakini USIOGOPE maana utashinda.Mwombe Mungu atakutia nguvu na kukusaidia.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Maana yake utakumbana na matatizo makubwa hasa ofisini

  na matatizo hayo yaweza kuwa ya aina mbalimbali.....

  Cha kufanya ufanye maombi saana
   
 9. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hali ilivyo kutokana na ndoto hizo ni dhahiri kuna wakati mgumu unakuja kwako. Sina aya yeyote ya biblia kwa sasa lakini hilo halina ubishi kwamba utaingia katika mapambano. Cha kufurahisha ni kwamba mwisho wa yote utakuwa mshindi. Matatizo hata hivyo ni sehemu ya maisha. Wewe una bahati kwamba utapambana ukijua utakuwa mshindi. Inakuwa hatari sana pale unapoingia katika migogoro na matatizo ambayo hujui utatokea wapi. Hapo ndipo mashinikizo ya damu yanapoanzia na matatizo mengine ya kimwili kwa sababu ya hofu. Sina uhakika kama unaweza kuzuia hayo yasitokee ila kuomba na kufunga ni muhimu ili Mungu akutie nguvu.
   
 10. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ninao iwezo wa kutafsiri ndoto. Nlipozisoma nilikua na mswali ya kumuuliza alieotz hizo ndoto. Baadae mwisho akawa anahitaji ushahidi wa kile kitachotumiwa ushahidi wa tafsiri.
  Sasa nakushauri umuombe Mod aihamishe hii uzi yako aipeleke jukwaa la dini/imani. Ili nianze kuzitafsiri na members wengine waanze mjadala.
  Naamini wengi mtanishangaa kwanini sijazitafsiri.
  Ukweli ni ajili ya maelezo ya huyo alieota.
  Naamini pia nmefuata utaratibu wangu.
   
 11. D

  Danniair JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mfasiri wa ndoto mara nyingi ni mwotaji mwenyewe.
  1. Kilele /juu kabisa ni kufanikiwa sana, lakini hapa wewe unataka kushuka
  2. Kushuka chini /kuanguka ni kuporomoka/kuachana najambo fulani
  3. Dubu katika ndoto ni hali ya kutishia amani/ na ukiwa
  4. Tembo ukiwaogopa katika ndoto ni kuwa kuna tatizo kubwa sana unaloogopa kulikabili
  5, Kupaa, hapa kunategemea ulipaa kwa bila vikwazo au kwa vikwazo. Lakini kama unavyoonyesha ulikuwa na vikwazo ni hivi unajitahidi kuendelea bila kujali jambo linalokutafuna moyoni lakini jambo hilo linakuzuia.

  Tafsiri; hii inaweza kuwa kuna jambo ambalo ualijua wewe. Jambo hili linakukosesha amani sana unataka kuachana nalo lakini unakumbana na vikwazo vya kujishauri hivyo unashindwa kuachana nalo japo kwa kulitamka hadharani.
  Hakika utaanguka tu kwani umeshuka. Ila achana na hizi past memories kwa kuzitamka hadharani.

  Ushauri wangu kwako.kati ya saa10:33 -19:13 tarehe 30.7.2011 usifanye maombi ila baada ya hapohadi tarehe 1.7.2011 kabla ya saa 8:37 mchana fanya maombi yako ya kutubu mbele ya muumba wako huku uksisitiza neno :... naachilia hali fulani... initoke na kurudi huko ilikotoka mimi siitaki sana. kama useme kwa imani yako. In english we say like this, in the name of....i am letting go of to spirits this and this problem. and never come to me any more.
  Nimekushauri mda kwa sababu najua ndani mda niliokuonya ni mbaya wakati huu wa mwezi mfu.
   
 12. One and Only

  One and Only Senior Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mara nyingi tunasoma kwenye vitabu vitakatifu njinsi Mungu alivyoongea na wanadamu kwa njia ya ndoto, mitume, manabii, makuhani, wafalme na wengine wengi, katika ndoto zako Mungu anakuonyesha utakayopitia, unayo vita mbele yako na mapito magumu lakini Mungu atakushindia. Fanya maombi Mungu akutie nguvu, hekima, uvumilivu na akushindie maana yeye ni Mungu atushindiyae soma: mwanzo 15: 1-17, mwanzo 37: 5-11, mwanzo 40: 5-19, mwanzo 41: 1-40, soma hiyo mistari itakusaidia
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ndoto is nothing, just don't believe on it.
   
 14. networker

  networker JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  mbwa;simba niroho ya uzinzi ina kufukuzia
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hardwood, Vita imeanza juu yako kwenye ulimwengu usioonekana, utapigwa kila upande, kazi yako au biashara yako haiko salama, afya na ustawi wa familia na ndoa yako itayumba sana sana.
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Unatazama sana vipindi vya wanyama kwenye TV.

  Nyumba uliokaribishwa una wasiwasi nayo kuwa wako wanaekupenda na wasiokupenda.

  Ndoto zako hizo hazina tatizo wala hakuna matatizo yatayokukuta. Ni ndoto za shibe. Punguza kula.
   
 17. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ndoto zinajengwa na mawazo pia maisha yako. Mara nyingi zinakuwa hazina maana, ila kuna wakati zinaweza kuelekezwa kule ambako fikra zako zimetawala katika kipindi hiko.

  Kutokana na maelezo yako, inaelekea kuna mabadiliko, tetesi au vitu ambayo unavifikiria sana na ambavyo sometimes vinakupa hofu, but at the same time naona kama unapata faraja either kupitia imani yako au vinginevyo. Yaani unajipa moyo utafanikiwa.

  Mara nyingi imani zinatusaidia mambo ambayo kama binadamu yanatuchanganya, mambo yale ambayo hatujui mwisho wake, tunamwomba Mola atusaidie na tunapata faraja moyoni. Kwako kama unayo imani ya kutosha kupitia dini yako itakusaidia kuondokana na fikra za hofu hivyo basi ndoto kama hizi zitaisha.

  Kuna upande wa pili wa kitabibu. Ndoto zinaweza changiwa pia na afya yako. Mfano kama hufanyi mazoezi na unapata matatizo ya kupumua usiku unaweza kuota unakimbia halafu unaishiwa pumzi au vitu unakimbizwa na mnyama halafu unashindwa kukimbia. Hivyo ndugu usiache kuangalia mwenendo wa afya yako, angalia uzito. Fanya mazoezi ya kutosha kama shughuli zako muda mwingi ni za ofisini.

  I wish you all the best!
   
 18. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,133
  Likes Received: 7,380
  Trophy Points: 280
  Just ndoto tu mkuu, worry not.
  kutokana na kua mtu anaota karibia kila siku, zinahitajika ndoto nyingi sana kutosheleza binadamu tuliopo, basi ndo maana hata ukipata ndoto za ajabu au isiyo na maana ushistuke maana kuna uhaba wa ndoto
   
 19. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani kila mtu akileta ndoto zake hapa, JF itajaa in an hour!
  Mbona mi nishaota nimekufa several times?

  Wewe punguza uasi, fanya ibada... subiri kitakachotokea kabiriana nacho!
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,374
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  bahati nzuri yule mwehu sheikh yahaya hatunaye tena angekudanganya saana kuhusu ndoto yako ila uwe na imani kuwa ndoto mara nyingi huendana na kile unachokiwaza ila pia huko uswahilini kuna wanga ambao huja km ndoto unaamka umechoka sana kumbe walikubebesha mizigo mizito usiku kucha
   
Loading...