Naomba Msaada: Ndoto hizi zimenitisha

Naomba Msaada: Ndoto hizi zimenitisha

Jamani wana JF!Hatukatazi kutoa maoni yenu. Ndoto ni taaluma inayo ufafanuzi wake. Huyu jamaa ameomba maana ya hizo ndoto sasa kila mtu anatoa mtazamo wake kama si Great thinkers!Wenye hizi taaluma wanawaona lowest thinkers.Kama uliwahi kudanganywa ni wewe na huyo aliekutafsiria!!Mbaya zaidi hata alieota hizo ndoto hajasema kitu...anabaki njia panda hajui afuate maelezo ya nani? Maana ameuliza kwa yeyote ataemtafsiria hizo ndoto atoe ushahidi wake!Lazima tujifunze na kufanya uchunguzi ...si kuamka na kueleza vile unavyofikiri ...imeniumiza sana!.Kama ndio hivyo Mod aihamishie kule Jukwaa la Udaku.
 
Pole hakikisha unamuomba Mungu ulinzi kwa imani yako kabla hujalala, Kama ni mkristo omba maombi ya nguvu uifunike nyumba kwa damu ya Yesu, uombe Mungu akuondolee hizo ndoto za kuzimu za shetani na malaika wake, usihangaike kutafsiri ndoto hayo ni mambo ya waganga wa kienyeji na tafsiri za ndoto zitaanza kukutia hofu na utaishi kwa mashaka kwa kujua kile ulichotafsiriwa ni cha kweli ,utaacha kufanya mambo yako ya maana ukae kusubiri tafsiri ya ndoto itokee, pole sana.
 
Usitishwe na hiyo ndoto, kama wewe ni Mkristo "usitumie hata nguvu nyingi tamka tu kuwa kwa jina la yesu kama kuna ubaya hautakupata" inatosha!!!!!! kama ni wadini nyingine nafikiri lazima kuna namna ya kufanya. Usije ukashawishika kusikiliza tafsiri za kibinadamu kabisa, hayo mambo ya ndoto niya kawaida sana hivyo usitishwe wala usiogope. Kuna wakati mimi niliota kuwa nipo sekondari ambayo nilimaliza miaka ya tisini, niliota mara kadhaa kuwa nipo shuleni hapo, wakati shule imeshabadilishwa na kuwa kitu kingine, Ndugu yangu hiyo ndoto yako haina uhusiano kabisa na maisha yako, naamini uliota kwa mara ya pili kwa kuwa mara ya kwanza ilikutisha na kufanya iendelee kuwepo kwenye ubongo neno moja ninalokuambia ni hili "U S I O G O PE" Mwamini Mungu tuuuuuuuu!
 
Saa zingine ukiota ndoto kazi yako ni moja tu, zibomoe kwa Jina la Yesu Kristu, kama ni ndoto ya Mungu hata kama umeibomoa kwa Jina la Yesu Mungu atatafuta namna ya kuwasilisha ujumbe wake kwako, kama ni ya kishetani itapotea hapohapo na hazitarudi tena!
Wewe zikemee kwa Jina la Yesu hata kama umeota ndoto nzuri, kama ni cha Mungu itakuja tu vizuri kwako.
Usiogope kabisa, kuwa na amani moyoni mwako!
 
jamani kuna ndoto imenitaziza nimeota nimepeleka simu kucharge kila nikimdai ananyama hii ndotö nimeota leo ni mara ya tano msaada wenu wakubwa
 
Bwana yu nawe. Majaribu yatajitokeza ofisini pako, yatakuwa ni makubwa sana. Utateseka. Lakini watesi wako watageukana na hakika utainuliwa juu na utayashinda
nami nimeelewa hivyo, ukiwa juu, ukipaa ni uwezo wa wewe kushinda vita, kupigana na mnyama na kumshinda vilevile ni ushindi. Unaonekana uko juu ila una maadui wengi wanataka kukushusha chini, kwakweli upo ktk vita tena sio na mmoja, hivyo simama ingawa unaonekana utashinda ila simama ktk maombi.
 
Yaani kila mtu akileta ndoto zake hapa, JF itajaa in an hour!
Mbona mi nishaota nimekufa several times?

Wewe punguza uasi, fanya ibada... subiri kitakachotokea kabiriana nacho!
Sasa unataka kutuambia hutakufa?
 
pole hakikisha unamuomba mungu ulinzi kwa imani yako kabla hujalala, kama ni mkristo omba maombi ya nguvu uifunike nyumba kwa damu ya yesu, uombe mungu akuondolee hizo ndoto za kuzimu za shetani na malaika wake, usihangaike kutafsiri ndoto hayo ni mambo ya waganga wa kienyeji na tafsiri za ndoto zitaanza kukutia hofu na utaishi kwa mashaka kwa kujua kile ulichotafsiriwa ni cha kweli ,utaacha kufanya mambo yako ya maana ukae kusubiri tafsiri ya ndoto itokee, pole sana.

kama hujui ni bora kukaa kimya kuliko kumpotosha mwenzako kila ndoto ina maana na tafsiri yake toka enzi ya nabii musa acha unafiki wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom