Naomba msaada kutafsiri 'Humanism'

mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Yupo fulani aliyewahi kusikia au kusoma juu ya ‘humanism’ au ‘humanistic teachings’ kwa kiingereza na anayejua kuitafsiri katika Kiswahili! “Mafundisho ya kibinadamu” haifiki! ‘Humanism’ inafundisha kwamba mtu alizaliwa kwa tabia mwema kabisa na inawapaswa jamii kuitunza na kuisaidia ile tabia nzuri ipate nafasi kusitawi. Mimi sikubali na mafundisho haya lakini ninatafuta tafsiri nzuri kama ipo kwa Kiswahili! Au je, ni lazima kutumia neno lile lile kwa Kiswahili pia??? Mimi ni mwingereza anayeishi hapa Uingereza. Ninajaribu kujifunza Kiswahili basi naomba ukijibu, tumie Kiswahili kisicho ngumu sana, yaani, maneno yaliyo rahisi kuelewa! Asanteeni sana!
 
Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,384
2,000
Yupo fulani aliyewahi kusikia au kusoma juu ya ‘humanism' au ‘humanistic teachings' kwa kiingereza na anayejua kuitafsiri katika Kiswahili! "Mafundisho ya kibinadamu" haifiki! ‘Humanism' inafundisha kwamba mtu alizaliwa kwa tabia mwema kabisa na inawapaswa jamii kuitunza na kuisaidia ile tabia nzuri ipate nafasi kusitawi. Mimi sikubali na mafundisho haya lakini ninatafuta tafsiri nzuri kama ipo kwa Kiswahili! Au je, ni lazima kutumia neno lile lile kwa Kiswahili pia??? Mimi ni mwingereza anayeishi hapa Uingereza. Ninajaribu kujifunza Kiswahili basi naomba ukijibu, tumie Kiswahili kisicho ngumu sana, yaani, maneno yaliyo rahisi kuelewa! Asanteeni sana!

Mimi sijasoma hii taaluma ya "Humanism au Humanistic teaching" lakini kama mswahili nina uhakika kuwa maana ya hili neno Humanism ni UTU au moyo wa kupenda watu.
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Mimi sijasoma hii taaluma ya "Humanism au Humanistic teaching" lakini kama mswahili nina uhakika kuwa maana ya hili neno Humanism ni UTU au moyo wa kupenda watu.

Asante kwa jibu, lakini maana ya 'utu' kwa kingereza ni 'humanity' - ina maana tofauti kabisa. Pia maneno 'moyo wa kupenda watu' yanakosa maana ya 'humanism'. 'Humanism' lina maana maalum au maana ya pekee. Huwezi kubahatisha maana. Sijui kama bado hamna tafsiri ya neno au wazo hili lakini ninauliza tu. Asante tena!
 
Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,384
2,000
Yupo fulani aliyewahi kusikia au kusoma juu ya ‘humanism' au ‘humanistic teachings' kwa kiingereza na anayejua kuitafsiri katika Kiswahili! "Mafundisho ya kibinadamu" haifiki! ‘Humanism' inafundisha kwamba mtu alizaliwa kwa tabia mwema kabisa na inawapaswa jamii kuitunza na kuisaidia ile tabia nzuri ipate nafasi kusitawi. Mimi sikubali na mafundisho haya lakini ninatafuta tafsiri nzuri kama ipo kwa Kiswahili! Au je, ni lazima kutumia neno lile lile kwa Kiswahili pia??? Mimi ni mwingereza anayeishi hapa Uingereza. Ninajaribu kujifunza Kiswahili basi naomba ukijibu, tumie Kiswahili kisicho ngumu sana, yaani, maneno yaliyo rahisi kuelew...Asante kwa jibu, lakini maana ya 'utu' kwa kingereza ni 'humanity' - ina maana tofauti kabisa. Pia maneno 'moyo wa kupenda watu' yanakosa maana ya 'humanism'. 'Humanism' lina maana maalum au maana ya pekee. Huwezi kubahatisha maana. Sijui kama bado hamna tafsiri ya neno au wazo hili lakini ninauliza tu. Asante tena!

Mkuu, tofautisha kati ya Utu (Humanism) na Ubinaadam (Humanity). Sio kila binaadam ni mtu. Binaadam aliekuzwa kwenye mazingira ya kinyama hatakuwa na maadili mema kwa binaadam wenzake au hatakuwa na utu (au sio mtu). Sehemu ya makala yako hapo juu niliyoitilia rangi nyekundu inaeleza vizuri sana kuwa Humanism ni TABIA na sio UMBILE.

Kwa hiyo jibu langu bado ni lile lile nililokupa mwanzo.

Magwiji wa lugha tafadhalini njooni mtusaidie.
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Asante rafiki! ‘Humanism' siyo neno tu bali ni filosofia maalum (ilitokea kama miaka 150 iliyopita). Kama usipowahi kusikia au kusoma nadhani ni ngumu kujaribu kutafsiri. Kiswahili changu labda hakifiki kueleza vizuri, lakini humanism inafundisha kwamba kila mtoto huzaliwa ‘mwema', kwa tabia mwema. Humanism haipokei, kwa mfano, mtoto anazaliwa na dhambi. Mtu anayefuata filosofia ya humanism anaitwa ‘humanist'. Humanists wanaamini hamna dhambi. Humanists wanaamini mtoto huzaliwa mwema. Najua yale maneno ‘utu' na ‘ubinadamu'. Utu hutafsiriwa na ‘human nature' au ‘humanity' (kama ulivyosema); na ‘ubinadamu' pia inaweza kutafsiriwa na ‘human nature' au ‘humanity' – inategemea na context (muktadha?). Najua maneno haya na maana yao, lakini natafuta tafsiri ya neno ‘humanism' kama filosofia. Samahani, lakini maana ya ‘humanism' siyo ‘tabia'. Tabia kwa kingereza ni '(human) nature'. Kwa mfano, humanism inasimama moja kwa moja dhidi ya Ukristo. Humanists wanasema hamna dhambi. Inafndisha kwamba huhitaji kufanya toba; huhitaji kusamehewa na dhambi zako; huhitaji kuokoa au kukombolewa. Hii ni ‘Humanism'. Kwa ujumla Humanism ni adui ya dini yote. Humanists wengi wanaamini kwamba dini ni hatari kwa jamii (society). Humanists wanasema hamna Mungu. Kwa kweli, rafiki, unijalie kusema naamini huwezi kutafsiri ‘humanism' isipokuwa umewahi kuyasoma au kuyasikia kuhusu FILOSOFIA YA HUMANISM. Humanism imeshaanza kueneza ulimwenguni na labda bado hamna tafsiri ya neno hili katika kila lugha, lakini nilitaka kujua kama ipo kwa Kiswahili. Asante tena!
 
Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,384
2,000
Mpendwa789, nimependa majibu yako. Mimi sio mwana-falsafa wa lugha/imani/dini kama wewe ingawaje nina Ph.D.(ya uhandisi - engineering). Naomba univumilie katika haya malumbano kwa sababu mimi pia ninajifunza kutoka kwako.

Awali ya yote nataka ujue kuwa mimi bado ninatafuta elimu zaidi kuhusu Mungu (Agnostic). Najua kuwa kuna kitu nisichokijua ambacho kinaweza kuwa MUNGU au la.

With this disclosure - sasa ngoja nidadavue makala yako hapa chini ili nione kama nimekuelewa vizuri. Dondoo zako nitakazozijibu zitapigiwa mstari, na maoni yangu yatakuwa kwenye bold-italics.Asante rafiki! ‘Humanism' siyo neno tu bali ni filosofia maalum (ilitokea kama miaka 150 iliyopita). Kama usipowahi kusikia au kusoma nadhani ni ngumu kujaribu kutafsiri. Kiswahili changu labda hakifiki kueleza vizuri, lakini humanism inafundisha kwamba kila mtoto huzaliwa ‘mwema', kwa tabia mwema.

Kwa maoni yangu hii ni common sense. Na katika kiswahili tunasema "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo". Ikimaanisha kuwa mtoto anapozaliwa anategemea sana malezi,matunzo na mafunzo ya wazazi na jamii.

Humanism haipokei, kwa mfano, mtoto anazaliwa na dhambi. Mtu anayefuata filosofia ya humanism anaitwa ‘humanist'. Humanists wanaamini hamna dhambi.

Ukishaingiza neno dhambi hapa unaingiza dini na mimi sikubaliani na kasumba (ideology) ya dini yoyote ile. Na hapa ndio sisi "binaadamu au watu" tunapokuwa wanafiki. Tunafikiria sisi ni viumbe mahsusi (special) sana. Kwa nini tusifikirie kuwa simba hazaliwi na dhambi. Akikuua na kukula sio dhambi bali anatekeleza matwakwa ya mungu tu?

Humanists wanaamini mtoto huzaliwa mwema. Najua yale maneno ‘utu' na ‘ubinadamu'. Utu hutafsiriwa na ‘human nature' au ‘humanity' (kama ulivyosema); na ‘ubinadamu' pia inaweza kutafsiriwa na ‘human nature' au ‘humanity' – inategemea na context (muktadha?). Najua maneno haya na maana yao, lakini natafuta tafsiri ya neno ‘humanism' kama filosofia.

Hapa sasa najua tunazungumzia maswala ya imani au dini. Lakini kwako wewe mkuu kutuuliza tafsiri ya HUMANISM ni sawa na kutuuliza tukupe tafsiri (neno moja) ya haya maneno yafuatayo:

 • Catholicism, Lutheranism, Mormonism, Presbyterianism, Protestantism, Quakerism
 • Judaism
 • Islam
 • Hinduism
 • Buddhism
 • Confusianism
 • Taoism
 • Jainism
 • Sikhism
 • Shintoism
 • Rastafarianism
 • Zoroastianism
 • Etc.

Samahani, lakini maana ya ‘humanism' siyo ‘tabia'. Tabia kwa kingereza ni '(human) nature'. Kwa mfano, humanism inasimama moja kwa moja dhidi ya Ukristo. Humanists wanasema hamna dhambi. Inafndisha kwamba huhitaji kufanya toba; huhitaji kusamehewa na dhambi zako; huhitaji kuokoa au kukombolewa. Hii ni ‘Humanism'. Kwa ujumla Humanism ni adui ya dini yote. Humanists wengi wanaamini kwamba dini ni hatari kwa jamii (society). Humanists wanasema hamna Mungu.

Hapa nakubaliana na HUMANIST isipokuwa tu siwezi kufikia kiwango cha kusema hakuna MUNGU kwa sababu sijui (agnostic).

Kwa kweli, rafiki, unijalie kusema naamini huwezi kutafsiri ‘humanism' isipokuwa umewahi kuyasoma au kuyasikia kuhusu FILOSOFIA YA HUMANISM. Humanism imeshaanza kueneza ulimwenguni na labda bado hamna tafsiri ya neno hili katika kila lugha, lakini nilitaka kujua kama ipo kwa Kiswahili. Asante tena!

Nakubaliana nawe kuwa huwezi kutafsiri "humanism" kama ilivyo kuwa huwezi kutafsiri "zoroastrianism".

Kila la kheri na utafiti wako.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,569
2,000
Humanism kwa direct translation ni utu. Ila mara nyingine unaweza kutafsiri neno, ukashindwa kubakisha maana ile ile ya falsafa kama hiyo falsafa haipo katika hiyo lugha unayotafsiria. Tafsiri ni zaidi ya maneno, kwa sababu inawezekana kabisa kwa Waingereza waliosoma habari za enlightenment Humanism (utu) ni mwanadamu kujitegemea na kutoamini katika mungu, wakati katika utamaduni wa Kiswahili utu ni kuamini mungu na kufanya alichoagiza.

Kwa hiyo unakuta neno halitafsiriki. Ukiforce direct translation unaweza kupata maana tofauti. Kiingereza utubora ni kuamini mwanadamu anaweza kujitegemea bila kumtegemea mungu, Kiswahili utubora ni mwanadamu kuamini kwamba yeye ni mja wa mwenyezi mungu tu na bila mungu hawezi chochote.

Neno moja hilohilo, lina maana tofauti katika tamaduni mbili tofauti kwa sababu tamaduni mbili tofauti zina mielekeo tofauti kuhusu utu.

I subscribe to a lot of the ideals that are central to humanism, particular secular humanism. Case in point being the ability of human beings to be ethical and moral without needing religion or god.The lyrics of "The Beatles" song "Imagine" come to mind.

Writing of "secular humanism" implies there being a "non-secular humanism", in contrast to the idea posed above that humanism is necessarily opposed to religion. A good example of non-secular humanism is Christian Humanism, which emphasize the humanity of Jesus.

In many cases, Humanism (capital H) is taken to mean secular humanism ( as opposed to Christian Humanism for example). I believe this is the root of thinking that Humanism has no room for religion. Secular humanism has no room for religion, there are other "humanisms" that accommodate religion as pointed above.
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Asante Kifyatu! Mimi naitwa David! Ya kwanza kabisa siyo kusudi langu kujadiliana juu ya dini au humanism – hata kidogo. Nilijaribu kueleza maana ya ‘humanism' ili kusaidia tafsiri ya neon hili tu – siyo kuanzisha majadiliano. Sina nafasi sasa kufanya hivyo na nafikiri Kiswahili changu hakitafika kufanya hivyo! Nilipenda kujua tu kama tayari ipo tafsiri ya ‘Humanism' kama filosofia, na sawasawa na sentensi ya mwisho wako (Nakubaliana nawe kuwa huwezi kutafsiri "humanism" kama ilivyo kuwa huwezi kutafsiri "zoroastrianism".) pamoja na jibu la Kiranga, inaonekana wazi kwamba hamna tafsiri ya neno hili. Nitakuja Tanzania mwezi ujao nami nataka kufundisha kidogo juu ya ‘Humanism'. Sasa, kwa mfano, kama ningesema kwa watu, "Mafundisho ya utu yanaeneza ulimwenguni……..", nafikiri kwa ujumla watu hawataelewa vizuri au watachanganyika na maneno haya. Nafikiri ni lazima kutaja neno ‘humanism' kwanza ndipo kueleza kwa ufupi mawazo ya filosofia hiyo kabla ya kuendelea. Siyo ndiyo? Nafikiri sasa nilipata jibu juu ya swali langu na nakushukuru sana kwa mawasilano yako katika jambo hili! Pia nafurahi sana kwamba naweza kupata nafasi to practice Kiswahili na wengine!
Ninakutakia heri na Mwaka Mpya!
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Nakushukuru sana kwa jibu lako, Kiranga. Mimi naitwa David. Kama nimeelewa maneno yako vizuri, nakubali, yaani, inaonekana kwamba hamna tafsiri ambayo watu wataelewa mara moja (immediately) kama nikitumia neno hili kwa Kiswahili – ni lazima kueleza maana ya neno hili kwanza. Kwa mfano, kama ningesema kwa watu, "Mafundisho ya utu yanaeneza ulimwenguni……..", nafikiri kwa ujumla watu hawataelewa vizuri au watachanganyika na maneno haya. Siyo ndiyo? Pamoja na jibu la Kifyatu sasa nadhania nimepata jibu na swali yangu na nakushuru sana kwa msaada wako!
However, is there not a contradiction when you say, "Humanism kwa direct translation ni utu." and then, "Ukiforce direct translation unaweza kupata maana tofauti". Exactly! If I used the word ‘utu' in Tanzania when I want to talk about ‘Humanism', surely they will misunderstand me? I don't think ‘Humanism' can be translated ‘utu' for this reason. If I say to people in Tanzania, "Mafundisho ya Utu…." I think that most will not understand or be confused – as you yourself suggest later in your answer. I think the only solution is, or will be a transliteration of the word itself into Swahili – with the necessary explanation or not, depending who you are speaking to.
As I said to Kifyatu above, my intention is not to debate humanism versus religion, but I explained to him – in short – the idea of humanism in order to help with the translation of the word!
Though a lot could be said, in short you are quite right in what you say about humanism, secular or otherwise. However, two things about ‘Christian Humanism'. As an outlook it is certainly not as popular or as widely used (as a term) as it used to be – having, in part, being somewhat overtaken by liberation theology. Secondly, historically and nowadays, most if not all (evangelical) Christians have regarded and regard ‘Christian Humanism' as liberal theology – in other words, not Christian at all. Though others, of course, would disagree with this stance!
I have difficulty in translating the verb ‘to practice'. If I want to say, ‘I am glad to have the opportunity to practice Kiswahili.', Could I do better than to say, ‘Nafurahia nafasi kupata mazoezi ya kutumia Kiswahili.'??? I would like to use the verb form of ‘practice', however. Could you help me with this?
So you write English as a native speaker of the language. Do you live in East Africa or where did you pick up English so well – if I may ask? As I said, I am English and live in the UK.
(Oh! I have just noticed your caption at the bottom of your entry. Well, I suppose it well illustrates the intrinsic antipathy of humanistic thought to religion!)
Anyway, many thanks for your help in this matter! I believe I have received a full answer to my question and I am grateful to you and Kifyatu!
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,569
2,000
mpendwa789 naona tumeelewana haswa kuhusu humanism/ utu.

Kwa sababu unajifunza Kiswahili, itakuwa vyema nikiandika kiswahili. Nilikuwa na mfanya kazi mwenzangu wa kutoka Uskochi (Scotland), alikuwa anafanya kazi za mazingira Tanzania. Basi alilalamika sana kwamba Watanzania walikuwa hawampi nafasi ya kujifunza kiswahili kwa maana kila mara walipokutana naye waliongea kiingereza, labda na wao ndiyo ilikuwa nafasi yao ya kujinoa kiingereza.

Miaka kama kumi iliyopita nilitaka kufanya kazi na kikundi fulani kutafsiri kitabu cha Brian Greene "The Elegant Universe". Nikagundua, hususan kwa nyanja za sayansi zenye mambo mengi mapya kama katika unajimu, kiswahili si tu hakina maneno, bali hata dhana zenyewe ni ngeni. Kwa mfano, tuna sayari na nyota lakini sifahamu kama kuna neno la kiswahili asilia la kumaanisha "galaxy". Katika hili, sioni ubaya wa kutohoa kutoka kiingereza na kusema "galaksi". Hata kiingereza chenyewe kimenufaika sana na kutohoa kutoka kilatini, kigiriki na lugha nyingine. Hii ni tabia ya lugha, na kama wanazuoni wataona kuna maneno yanahitajika, ni wajibu kuongeza, kwani lugha hukua.

Pia, watu wa kawaida hawafahamu maneno mengi sana ya kiswahili ambayo hayatumiwi kila siku, hivyo mara nyingine tunaweza kufikiri kiswahili hakina maneno, kumbe yapo mengi sana na mengine hata katika kamusi hayapo, wanaongea watu wanaojua lahaja ya Pemba tu huko waliojikita katika uvuvi, au watu wa Barawa, na kadhalika. Nikisoma vitabu vya Shaaban Robert, muandishi mashuhuri wa kiswahili aliyeandika sana kabla ya uhuru wa Tanganyika, na malenga walioandika miaka ile - na hata washairi mashuhuri wa sasa- naona maneno mengi yametumika ambayo watu wa kawaida hawatayajua katika mazungumzo ya kila siku, au hata katika mhadhara wa chuo kikuu. Lakini hili ni suala lililo sehemu nyingi, wengi hawawezi kuwasiliana kwa kiingereza cha Michael Erick Dyson au Noam Chomsky katika mazungumzo ya kila siku. Hili si kwa kiswahili na kiingereza tu, mfalme Hirohito wa Japana alipomaliza kutoa hotuba yake ya kujisalimisha baada ya Japan kushindwa vita vikuu vya pili, Wajapan walianza kujiuliza "huyu mfalme hapa kasema nini?", kwa sababu alitumia kijapani cha hadhi ya juu sana. Inabidi tuepuke umwinyi katika mawasiliano kwa kutumia lugha sahihi lakini isiyowafungia wengine kuelewa. Kwa wapenda lugha hili linaweza kuwa gumu kwa sababu kutafuta urembo wa lugha kunaweza kumaanisha kuwafungia wengine wasielewe. Mimi pia nina tatizo hilo.

Kuhusu " ‘I am glad to have the opportunity to practice Kiswahili.' unaweza kusema " ‘Nafurahia kupata nafasi ya kujizoeza kutumia Kiswahili.'. "To practice" = " ku jizoeza".

Asante kwa kukisifu kiingereza changu, bado nina mengi ya kujifunza.Naishi Marekani, ila tangu mdogo nilipenda sana kusoma vitabu vya kiingereza ikiwa pamoja na kamusi za kiingereza kwa kiingereza na kiswahili kwa kiingereza ili kujenga msamiati. Nina mapenzi sana na lugha, sayansi na falsafa na mambo mengi niliyotaka kufahamu hayakuwa yameandikwa kiswahili, hivyo nilikuwa natumia muda mwingi sana kwenye maktaba za British Council, United States Information Services na Maktaba Kuu ya Taifa pamoja na za shule nilizosoma. Kama methali ya kiswahili inavyosema "mgaagaa na upwa hali wali mkavu" na mimi ingawa siwezi kujisema kama ni gwiji wa kiingereza, ila kupenda kusoma kumejenga msamiati na ujuzi wa kiingereza.

Karibu kutumia nafasi hii kujifunza lugha na mambo mengine ya utamaduni wa kiswahili na Afrika Mashariki.
 
Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,384
2,000
Asante Kifyatu! Mimi naitwa David! Ya kwanza kabisa siyo kusudi langu kujadiliana juu ya dini au humanism – hata kidogo. Nilijaribu kueleza maana ya ‘humanism' ili kusaidia tafsiri ya neon hili tu – siyo kuanzisha majadiliano. Sina nafasi sasa kufanya hivyo na nafikiri Kiswahili changu hakitafika kufanya hivyo! Nilipenda kujua tu kama tayari ipo tafsiri ya ‘Humanism' kama filosofia, na sawasawa na sentensi ya mwisho wako (Nakubaliana nawe kuwa huwezi kutafsiri "humanism" kama ilivyo kuwa huwezi kutafsiri "zoroastrianism".) pamoja na jibu la Kiranga, inaonekana wazi kwamba hamna tafsiri ya neno hili. Nitakuja Tanzania mwezi ujao nami nataka kufundisha kidogo juu ya ‘Humanism'. Sasa, kwa mfano, kama ningesema kwa watu, "Mafundisho ya utu yanaeneza ulimwenguni……..", nafikiri kwa ujumla watu hawataelewa vizuri au watachanganyika na maneno haya. Nafikiri ni lazima kutaja neno ‘humanism' kwanza ndipo kueleza kwa ufupi mawazo ya filosofia hiyo kabla ya kuendelea. Siyo ndiyo? Nafikiri sasa nilipata jibu juu ya swali langu na nakushukuru sana kwa mawasilano yako katika jambo hili! Pia nafurahi sana kwamba naweza kupata nafasi to practice Kiswahili na wengine!
Ninakutakia heri na Mwaka Mpya!

Karibu sana tanzania. Pia nikushukuru kwani na mimi nimejifunza.
 
May 13, 2013
7
45
Katika kufunuafunua kamusi, nimeona hivi:

Humanism = elimu ya ubinadamu (inayohusu binadamu kwanza na mahitaji yake kuliko misingi ya dini).

Sijui kama itakusaidia.
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Asante. Labda itasaidia wengine. Binafsi nimeshaelewa maana ya 'Humanism'. Swali langu lilihusu tafsiri ya neno/wazo hili tu na nilipata jibu sasa. Lakini ni kweli, 'humanism' inajishughulisha na mahitaji ya binadamu na jinsi ya kuyaondoa mahitaji haya - hiyo kwa ufupi tu, yapo mambo mengine mengi ambayo yanaweza kutajiwa juu ya humanism!
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
5,835
2,000
wenzangu wamesema mengi kuhusu hili neno humanism. napenda tu kusema kwamba kila lugha ina utamaduni wake. kwa hivo ili upate tafsiri sahihi ya neno fulani ambalo huwasilisaha wazo fulani ni lazima ujue utamaduni wa hiyo lgha. hakuna tafsri sahihi ya moja kwa ya neno hili kwa vile hailikuwa sehemu ya utamaduni wetu. kwa hiyo humanism si utu bali inahusu utu yaani maadili. linaelezea imani (belief) katika maadili (moral values) kwamba mfumo wa jamii unaofuata maadili ya ile jamii utatwa humanism kama vile ulivyo socialism. mfumo huu ulianzia ulaya katika kipind kilichoitwa Renaissance kama harakati (movement) na hatimaae ukawa ni ideology/philosophy ya wakati huo. wako wanataaluma (Intellectuals) ambao walitetea mfumo huu na hata kuna vitabu vya falsafa vinavyozungumzia humanism. watu wa baraza la kiswahili wanaweza kutafuta neno maalumu au likatoholewa tu na kuwa yumanizimu. itakuwa vigumu kusema mfumo wa ubinadamu.
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
mpendwa789 naona tumeelewana haswa kuhusu humanism/ utu.

Kwa sababu unajifunza Kiswahili, itakuwa vyema nikiandika kiswahili. Nilikuwa na mfanya kazi mwenzangu wa kutoka Uskochi (Scotland), alikuwa anafanya kazi za mazingira Tanzania. Basi alilalamika sana kwamba Watanzania walikuwa hawampi nafasi ya kujifunza kiswahili kwa maana kila mara walipokutana naye waliongea kiingereza, labda na wao ndiyo ilikuwa nafasi yao ya kujinoa kiingereza.

Miaka kama kumi iliyopita nilitaka kufanya kazi na kikundi fulani kutafsiri kitabu cha Brian Greene "The Elegant Universe". Nikagundua, hususan kwa nyanja za sayansi zenye mambo mengi mapya kama katika unajimu, kiswahili si tu hakina maneno, bali hata dhana zenyewe ni ngeni. Kwa mfano, tuna sayari na nyota lakini sifahamu kama kuna neno la kiswahili asilia la kumaanisha "galaxy". Katika hili, sioni ubaya wa kutohoa kutoka kiingereza na kusema "galaksi". Hata kiingereza chenyewe kimenufaika sana na kutohoa kutoka kilatini, kigiriki na lugha nyingine. Hii ni tabia ya lugha, na kama wanazuoni wataona kuna maneno yanahitajika, ni wajibu kuongeza, kwani lugha hukua.

Pia, watu wa kawaida hawafahamu maneno mengi sana ya kiswahili ambayo hayatumiwi kila siku, hivyo mara nyingine tunaweza kufikiri kiswahili hakina maneno, kumbe yapo mengi sana na mengine hata katika kamusi hayapo, wanaongea watu wanaojua lahaja ya Pemba tu huko waliojikita katika uvuvi, au watu wa Barawa, na kadhalika. Nikisoma vitabu vya Shaaban Robert, muandishi mashuhuri wa kiswahili aliyeandika sana kabla ya uhuru wa Tanganyika, na malenga walioandika miaka ile - na hata washairi mashuhuri wa sasa- naona maneno mengi yametumika ambayo watu wa kawaida hawatayajua katika mazungumzo ya kila siku, au hata katika mhadhara wa chuo kikuu. Lakini hili ni suala lililo sehemu nyingi, wengi hawawezi kuwasiliana kwa kiingereza cha Michael Erick Dyson au Noam Chomsky katika mazungumzo ya kila siku. Hili si kwa kiswahili na kiingereza tu, mfalme Hirohito wa Japana alipomaliza kutoa hotuba yake ya kujisalimisha baada ya Japan kushindwa vita vikuu vya pili, Wajapan walianza kujiuliza "huyu mfalme hapa kasema nini?", kwa sababu alitumia kijapani cha hadhi ya juu sana. Inabidi tuepuke umwinyi katika mawasiliano kwa kutumia lugha sahihi lakini isiyowafungia wengine kuelewa. Kwa wapenda lugha hili linaweza kuwa gumu kwa sababu kutafuta urembo wa lugha kunaweza kumaanisha kuwafungia wengine wasielewe. Mimi pia nina tatizo hilo.

Kuhusu " ‘I am glad to have the opportunity to practice Kiswahili.' unaweza kusema " ‘Nafurahia kupata nafasi ya kujizoeza kutumia Kiswahili.'. "To practice" = " ku jizoeza".

Asante kwa kukisifu kiingereza changu, bado nina mengi ya kujifunza.Naishi Marekani, ila tangu mdogo nilipenda sana kusoma vitabu vya kiingereza ikiwa pamoja na kamusi za kiingereza kwa kiingereza na kiswahili kwa kiingereza ili kujenga msamiati. Nina mapenzi sana na lugha, sayansi na falsafa na mambo mengi niliyotaka kufahamu hayakuwa yameandikwa kiswahili, hivyo nilikuwa natumia muda mwingi sana kwenye maktaba za British Council, United States Information Services na Maktaba Kuu ya Taifa pamoja na za shule nilizosoma. Kama methali ya kiswahili inavyosema "mgaagaa na upwa hali wali mkavu" na mimi ingawa siwezi kujisema kama ni gwiji wa kiingereza, ila kupenda kusoma kumejenga msamiati na ujuzi wa kiingereza.

Karibu kutumia nafasi hii kujifunza lugha na mambo mengine ya utamaduni wa kiswahili na Afrika Mashariki.

Kumbe! Niseme nini sasa? Nakushukuru kwa mawazo yako na kwa kuchukua muda kuandika mengi unipe nafasi kujizoeza Kiswahili na kujenga msamiati wangu! Asante! Nafurahi nilielewa inakaribia yote ila sikuweza kupata tafsiri kamusini ya maneno yafuatayo: hususan, nyanja na kutohoa. Pia asante sana kwa tafsiri ya ‘to practice'. Nakubali na uliyoyaandika juu ya tabia ya lugha. Tatizo langu sasa ni jambo hili ya kwamba kuna na maneno mengi ya Kiswahili ya kisasa yanayotokeza karibu kila siku! Mwanzoni nilinunua vitabu ‘Tujifunze Lugha Yetu' ili niweze kujifunze Kiswahili kwa urahisi hatua kwa hatua. Vitabu hivi vilinisaidia sana, lakini ninaposoma jamiiforums au Facebook natambua ya kwamba kazi yangu ya kujenga msamiati wangu inaongezeka sana tena sana! Mimi napenda kujifunza Kiswahili kwa sababu napenda nchi na hasa watu wa Tanzania. Ndiyo, labda tunaweza kuwasiliana mara nyingine. Ningefurahi sana! Best wishes,
David
 
mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
wenzangu wamesema mengi kuhusu hili neno humanism. napenda tu kusema kwamba kila lugha ina utamaduni wake. kwa hivo ili upate tafsiri sahihi ya neno fulani ambalo huwasilisaha wazo fulani ni lazima ujue utamaduni wa hiyo lgha. hakuna tafsri sahihi ya moja kwa ya neno hili kwa vile hailikuwa sehemu ya utamaduni wetu. kwa hiyo humanism si utu bali inahusu utu yaani maadili. linaelezea imani (belief) katika maadili (moral values) kwamba mfumo wa jamii unaofuata maadili ya ile jamii utatwa humanism kama vile ulivyo socialism. mfumo huu ulianzia ulaya katika kipind kilichoitwa Renaissance kama harakati (movement) na hatimaae ukawa ni ideology/philosophy ya wakati huo. wako wanataaluma (Intellectuals) ambao walitetea mfumo huu na hata kuna vitabu vya falsafa vinavyozungumzia humanism. watu wa baraza la kiswahili wanaweza kutafuta neno maalumu au likatoholewa tu na kuwa yumanizimu. itakuwa vigumu kusema mfumo wa ubinadamu.

Naamini yote uliyoyaandika ni kweli (kama nilielewa mawazo yako – Kiswahili changu ni limited!). Kwa hiyo mimi binafsi nilitaka kujua juu ya tafsiri ya neno/ideology hili tu – siyo kuingia katika ufananuzi mrefu wa mfumo huu. Lakini nafikiri ulieleza tatizo ambalo tunalikuta na jambo hili vizuri sana.
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
5,835
2,000
Naamini yote uliyoyaandika ni kweli (kama nilielewa mawazo yako – Kiswahili changu ni limited!). Kwa hiyo mimi binafsi nilitaka kujua juu ya tafsiri ya neno/ideology hili tu – siyo kuingia katika ufananuzi mrefu wa mfumo huu. Lakini nafikiri ulieleza tatizo ambalo tunalikuta na jambo hili vizuri sana.
nimekuelewa ideology kwa kiswahili ni itikadi kama ile ya chama, nchi n.k. kuhusu masuala ya msingi kama siasa uchumi nk.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,569
2,000
Kumbe! Niseme nini sasa? Nakushukuru kwa mawazo yako na kwa kuchukua muda kuandika mengi unipe nafasi kujizoeza Kiswahili na kujenga msamiati wangu! Asante! Nafurahi nilielewa inakaribia yote ila sikuweza kupata tafsiri kamusini ya maneno yafuatayo: hususan, nyanja na kutohoa. Pia asante sana kwa tafsiri ya ‘to practice'. Nakubali na uliyoyaandika juu ya tabia ya lugha. Tatizo langu sasa ni jambo hili ya kwamba kuna na maneno mengi ya Kiswahili ya kisasa yanayotokeza karibu kila siku! Mwanzoni nilinunua vitabu ‘Tujifunze Lugha Yetu' ili niweze kujifunze Kiswahili kwa urahisi hatua kwa hatua. Vitabu hivi vilinisaidia sana, lakini ninaposoma jamiiforums au Facebook natambua ya kwamba kazi yangu ya kujenga msamiati wangu inaongezeka sana tena sana! Mimi napenda kujifunza Kiswahili kwa sababu napenda nchi na hasa watu wa Tanzania. Ndiyo, labda tunaweza kuwasiliana mara nyingine. Ningefurahi sana! Best wishes,
David

David,

Hususan = particularly
Nyanja = fields, the singular is uwanja
Tohoa = transliterate (as in adapting a word from one language to another, changing minimal phonetics)

Natumaini utaweza kuongeza msamiati japo kidogo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom