Naomba msaada kuhusu huyu mpenzi

Naomba msaada kuhusu huyu mpenzi

Sasa na ww nikwamba wanawake wameisha au uwezi kumface msichana na kumwambia au una shida gani????

Kashakwambia ana anae mpenda kama ww unavyo mpenda means akupendi ... sasa kwenda kumuomba asikuache sijui atatoa wapi upendo wa kukupa. Nyie ndo wale mnaombiwaga baby tujenge nyumba ya pili ili ukiniacha tugawane ..... Shtuka basi
 
Nashukuru kwa ushauri wako lakini leo kanambia atanifikiria sasa naogopa asije akakubali wakati nimeshachukua maamuzi magumu ambayo si sahihi!
 
Uuupsi kwa hiyo wewe unajpa moyo utakupenda ..worry out wait umeme gridi kuu ukikatika atakukuhitaji wewe jenereta

Kiukweli nikama usemavyo lakini kaniambia atanifikiria!
Ngoja tuone!
 
Wanawake wameisha?
Tafuta wako

Sasa si huyo jamani?
Kila mwanamke sikuhizi kashawahiwa,
Kuna wengine wanaoa lakini mwanamke anamwambia wazazi tu wamenilazimisha lakini mimi nilikua nina bwana wangu tayari!
 
Nashukuru kwa ushauri wako lakini leo kanambia atanifikiria sasa naogopa asije akakubali wakati nimeshachukua maamuzi magumu ambayo si sahihi!

Mapenzi yakufikiriwa umeyasikiaga wapi!!!
 
Sasa wewe mwezi mmoja tu unaanza kulialia kama umemjua miaka mitano iliyopita!! Alaf si amekwambia ukweli wewe unataka uendelee na nini!?
 
Kula mzigo

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Nilipewa namba ya msichana na rafiki yangu mmoja, nilichat nae kwa muda mrefu hadi tukawa wapenzi.

Kipindi cha karibuni nilimuuliza kiutani kama aliwahi kua na Boyfriend akawa hataki kunijibu, lakini niliamua kumsisitizia swali hilo hadi akaamua kuniambia kua ni kweli anae na akaniambia "NAOMBA TUACHANE".

Nilipomuuliza kwanini akanambia kwasababu kuna mtu ANAMPENDA kama vile mimi ninavyompenda yeye.

Nilichoamua kumuomba ni mimi kuonana na yeye ukichukulia ni kama mwezi mmoja tangu tufahamiane.

Kakubali tuonane kesho lakini nimebaki na mawazo ni vitu gani hasa natakiwa nivifanye;-

1)Kwasababu hatujawahi kuonana nianze kumtongoza upya?
2)Nianze kwa kumbembeleza asiniache?
3)Hakuna jipya litakalotokea bora nisiende nitazidi kuumia moyo tu!

Naombeni mnipe ushauri jamani nimechanganyikiwa!

Nyie wote mko darasa la ngapi???
 
utoto raha sana

kweli ndugu yangu unaonekana uko mpweke loh umenichekesha ile mbaya manake sikuamini nilichokuwa nakisoma, mtu ulikuwa hata kumuona hujamuona lakini ushahesabu ni mpenzi wako, mara anakwambia muachane yeye anampenzi wake bado unasisitiza ukamuone kwanza, haya mmeonana amekwambia atakufikria bado unasubiri mmh, haya kila la kheri
 
Sasa wewe mwezi mmoja tu unaanza kulialia kama umemjua miaka mitano iliyopita!! Alaf si amekwambia ukweli wewe unataka uendelee na nini!?

Nimeamini bana mimi fungu la kukosa!
Hata simu hapokei sms hajibu!
 
kweli ndugu yangu unaonekana uko mpweke loh umenichekesha ile mbaya manake sikuamini nilichokuwa nakisoma, mtu ulikuwa hata kumuona hujamuona lakini ushahesabu ni mpenzi wako, mara anakwambia muachane yeye anampenzi wake bado unasisitiza ukamuone kwanza, haya mmeonana amekwambia atakufikria bado unasubiri mmh, haya kila la kheri

Tatizo sijui ana nini! Tulichat sana tu tukakubaliana ghafla akabadilika na kusema kua naomba tuachane!
Ndio maana nikamuomba bora tuonane nikidhani huenda labda akabadili msimamo lakini naona kama nalazimisha sasa!
Kinachoniuma ni ile hela yng niliyomuhonga tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom