Naomba msaada juu ya jambo hili la ajabu ambalo limetuchanganya kama familia

Saidama

JF-Expert Member
Jun 10, 2022
500
944
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, ni jambo lililotushtua kama familia kutokana na uajabu wake.

Ipo hivi, siku ya juzi tar 19 majira ya saa sita kasoro usiku nikiwa nimelala fofofo, simu yangu ambayo ilikuwa kwenye 'vibration mode' ilikuwa ikiita.

Wife kwakuwa alikuwa bado hajalala akawa ananiamsha niipokee lakini kabla hajafanikiwa kuniamsha akashangazwa kuona namba iliyokuwa inanipigia ni namba yake mwenyewe ambayo anatumia kwenye simu yake na wakati huo simu yake akiwa nayo mkononi, cha kushangaza zaidi ni kuwa simu yake haikuwa na salio la kuweza kupiga wala kubeep na haikuwa inaonesha kama inapiga simu, lakini kwenye simu yangu inaonekana ni namba yake ndiyo inapiga, namba yake ambayo nimeisave vizuri kabisa.

Wife akaamua kupokea mwenyewe tu ili aone ni kitu gani. Hakukuwa na sauti yoyote iliyosikika na yeye pia hakuongea chochote. Akawa ameiskilizia mpaka sekunde ya 31 akakata.

Kwakuwa nilikuwa nimechoka sana wife hakutaka kuniamsha na badala yake akaja kunielezea kila kitu asubuhi ambapo iliingia habari nyingine ya kushangaza tena.

Mama yangu mzazi alimpigia simu wife kumuuliza kwanini alikuwa anampigia usiku wa manane, hii ikiwa na maana kuwa namba hii ya wife ilionekana ikimpigia mama yangu mzazi pia usiku ule ule hali ya kuwa haikuwa na salio na kwenye simu ya wife hakuna call history wala hakuna salio la kupiga wala kubeep.

Sasa kitu kinachochagiza wasiwasi kwenye hili ni kwamba namba hii anayotumia wife ni namba iliyokuwa ikitumiwa na marehemu bibi yangu mzaa mama kama namba ya akiba na ina usajili kamili wa marehemu bibi ambae alifariki mwaka jana.

Hapa ndo kidogo pamefanya tuwe na wasiwasi.


Mimi kichwani mpaka sasa nina maswali mawili, kwamba je inawezekana likawa ni swala la kimtandao? au ni jambo linalohusiana na mambo ya giza kutokana na kua namba hii ilikua ikitumiwa na marehemu bibi yangu?


Kiukweli nimeshindwa kabisa kuelewa mpaka sasa. Naombeni msaada wa mawazo yenu jamani kwa ambao huenda mnafahamu au mmewai kuona mambo kama haya.
 
Simu ya mkeo ni itel?

Muulize vizuri mkeo, inawezekana alikuwa anabonyeza bonyeza Simu usiku huo. Unaweza kuwa hauna Salio ila simu ikaita upande wa pili tena sometimes inaacha ujumbe fulani alikutafuta saa fulani.

Nakuona tu unaanza kuhusisha mambo ya sijui bibi marehemu! Acha kusumbua ubongo kwa mambo yasiyo na maana na yasiyokuwepo.

Nje ya mada mkuu, nakukumbusha tu kutumia namba ya mtu mwingine akiwa Hai au amekufa ni kosa kisheria!
 
network issues tu mzee, hakuna kingine zaid ya hicho, so relax.
Nimejitahidi sana kurelax na kulifkiria hili jambo kitalam lakini namna mama na wife walivyo ingiwa wasiwasi na kwa vitu wanavyowaza, nimejikuta nashindwa kulifkiria vizuri. Shukrani kwa comment yako
 
Simu ya mkeo ni itel?

Muulize vizuri mkeo, inawezekana alikuwa anabonyeza bonyeza Simu usiku huo. Unaweza kuwa hauna Salio ila simu ikaita upande wa pili tena sometimes inaacha ujumbe fulani alikutafuta saa fulani...
Simu ni tecno kiswaswadu. Ye anasema alikua anaskiliza redio, hakua anabonyeza bonyeza. Hili jambo wife alivyonieleza moja kwa moja nilianza kulifkria kwa upande wa matatizo ya mtandao ila alivyoanza kuleta habari za bibi na alivyoingiwa na wasiwasi, mama nae hivyo hivyo. Hapo wakawa wamenivuruga ndo sababi nikaona nililete hapa
 
Simu ni tecno kiswaswadu. Ye anasema alikua anaskiliza redio, hakua anabonyeza bonyeza. Hili jambo wife alivyonieleza moja kwa moja nilianza kulifkria kwa upande wa matatizo ya mtandao ila alivyoanza kuleta habari za bibi na alivyoingiwa na wasiwasi, mama nae hivyo hivyo. Hapo wakawa wamenivuruga ndo sababi nikaona nililete hapa
Nenda kwa Mwamposa 😒
 
Imetokeaje mkeo akarithi namba ya marehemu wakati hawana undugu?
Alikua na ukaribu sana na bibi halafu ye hana kitambilisho wala namba ya NIDA. Kwaio akawa ameichukua hii namba kutoka kwa bibi. Alianza kuitumia tangu bibi hajafariki
 
Hata kama ni uzembe mtupu kurithi namba isiyomhusu angetumia hata nida yako kisha mkaja kubadili mbeleni. Nina watu wa karibu waliokua karibu sana na mama zao ila hawajathubutu kurithi namba za wazazi wao
Alikua na ukaribu sana na bibi halafu ye hana kitambilisho wala namba ya NIDA. Kwaio akawa ameichukua hii namba kutoka kwa bibi. Alianza kuitumia tangu bibi hajafariki
 
Dogo unaliwa nyama leo'

1. Lazima alijarb kukupgia na akawa hajakupata so network ilipokaa sawa ujumbe ukakufikia.

2. Lazima mama yako alipigiwa na mkeo na akafuta call history kama ulisema. Nae ujumbe ukamfikia mtandao ulipotulia.

Endelea kuishi kwa utulivu mkuu, hakuna cha uchawi wala wanga.
 
Embu ngoja aje mshana,,,,,
Niko hapa nijuavyo mimi mtu akifa namba yake haipaswi kutumika na mwanafamilia yeyote tena! Hata mimi mtu akishakufa na nanba yake naifuta kwenye phone book yangu
Nina kisa kinachofanana na hicho kidogo..
Kuna bibi mmoja tulifahamiana katika mazingira ambayo nisingependa kuyaweka wazi hapa, nikawa na ukaribu naye kiasi cha kuniita mjukuu wake aliyepewa na Mungu .. Nikiri wazi alinisaidia kwa mengi sana na mimi pia hivyohivyo
Namba yake ya simu nimeikariri hata sasa! Lakini alipofariki 2012 niliifuta kwenye phone book yangu
Sasa mwezi uliopita ile namba ikanipigia.. Nikastuka sana lakini nikaipokea hakukuwa na majibu upande wa pili.. Nikiipiga ni kama inapokelewa lakini hakuna sauti.. Hiyo hali iliendelea karibia wiki nzima mpaka nilipoamua kuiblock
 
Back
Top Bottom