Serikari imefanya msaada wangu kwa familia usiwe na matunda

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,714
Wakuu yaani naumia Sana tena Sana, kwa wale ambao wamekuwa wanafatilia baadhi ya nyuzi zangu mtagundua ni namna gani nilivojaribu kupambana mpaka hatua hii nilipo,

Kutoka kulalia mabox chini na wife mpaka kuununua kitanda na godoro ndani ya mwaka mmoja baada ya kutoka kijijini,

Mm kazi yangu ni fundi wa vifaa vya electronic hasa simu,radio,tv nk.

Sasa baada ya kupambana nikawa nimewakumbuka familia yangu huko kijijini ambao ni baba na mama na wadogo zangu wawili ambao wote wapo secondary, nikafanikiwa kuwatumia computer kwa ajili ya kurusha movie na nyimbo nk. Pale kijijini maana mazingira nilikuwa nayajua pia kipindi nipo kijijini niliwafundisha wadogo zangu kutumia computer,

Hivo wanafahamu tu vizuri, basi niliwatumia mwezi wa 12 tarehe 24 2023

Lengo langu ni ili waweze kununua madaftari na baadhi ya huduma ndogo ndogo za hapo nyumbani hata chakula pia, baada ya wiki moja nilimpigia simu na kumuuliza kuhusu kazi Kama inaenda poa, akanishukuru Sana na ndani ya wiki moja aliweza kusevu 18000 kwa kurusha movie na nyimbo tu kwani pale mtaani hakuna hiyo huduma zaidi ya yeye tu,

Basi Mimi nikafurahi pia wao wakafurahi,
Kwani walipata hela ya mtumizi ya shule bila shida,

Sasa kilichonifanya niandike huu uzi ni hiki hapa,

Hivi Sasa hii ni wiki ya tatu hakuna umeme kabisa pale kijijini, hii ni baada ya transformer kupata hitilafu kulitokea mvua ya radi ndo umeme ukakata,

Sasa hivi wananchi wameanza tu kununua sola kwa wenye uwezo hasa ukilinganisha sasa ni msimu wa kilimo, pesa huwa ni ngumu hasa kwa wakulima kwani hutegemea mavuno,

Je? Serikali au tanesco hawana vifaa vya akiba?

Au haijali tena wananchi wake?

Kama wapo kwenye mpango wa kufunga je? wanasubiria nini au wanawa cheleweshea nini kuwapa wanakijiji wale huduma ile muhimu kabisaa,

Kero yangu naomba isikilizwe, isipuzwe.
 
hali hiyo wanayopitia ndugu zako ndio tuliyonayo maelfu ya vijana tunaoendesha biashara zetu kwa kutegemea umeme,TUMEFUGA HASIRA NA CHUKI KALI DHIDI YA HII SERIKALI YA WANYANG'ANYI NA MAJIZI
 
hali hiyo wanayopitia ndugu zako ndio tuliyonayo maelfu ya vijana tunaoendesha biashara zetu kwa kutegemea umeme,TUMEFUGA HASIRA NA CHUKI KALI DHIDI YA HII SERIKALI YA WANYANG'ANYI NA MAJIZI
Huku nilipo toka jumapili ndo nimekuja kufanya kazi alhamisi kwani walikuwa wanauchukua saa12 asubuhi na kuurudisha saa2 usiku
 
Back
Top Bottom