Naomba Mnishauri nilime zao gani

Naomba Mnishauri nilime zao gani

Mwezi wa Ramadhani unaanza lini? Kama utapiga mahesabu ya mihogo, viazi vitamu na ndizi mzuzu kwa mwezi huo soko ni zuri sana.
 
Ubarikiwe ndugu..wasiwasi wangu juu ya mpunga ni naskia unahitaji uangalizi wakaribu sana..hasa ukizingatia kuna wale ndege...so itabidi nimuweke mtu kwa kazi hio na mtaji huo ni kidogo..

Pia vipi naweza lima hekari ngapi kwa mtaji huo ndugu
Kwa 3m Usangu unaweza kulima mpaka ekari sita, kuanzia kukodi shamba, kulima, mbolea, mbegu na palizi. Ila inabidi upate mtu mwaminifu. Na mavuno ni kuanzia gunia 15 kwa ekari kwenda juu
 
Habari za kutwa ndugu zangu..
Mimi nikijana niliemaliza chuo na sina ajira, nmejichanga kwa muda sasa, nimepata million 3, sasa nataka kuingia kwenye kilimo ninaishi mkoa wa Mbeya.

Nmefanya kautafiti kidogo nikaona kuna eneo wanafanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya, ila nashindwa kuamua nilime zao gani iliangalau nikuze mtaji wangu kwakiasi kikubwa kidogo, binafsi nikaona bora nilime Viazi au Mahindi..

VIAZI
Kwa utafiti wangu mdogo nmeskia hekari moja ya viazi inatoa gunia 70-90 na mara ya mwisho gunia 1 nliskia linauzwa 62,000/= Mbeya.

MAHINDI
Pia hekari moja ya Mahindi inatoa gunia hadi 30 kama kila hatua ikifanywa kwa usahihi bei kwa gunia bado sijaifahamu.

Sasa nawakaribisha ndugu zangu wana Jf mnishauri nilime nini kwa mtaji huo, inaweza ikawa ni kati ya mazao nliyoyataja au zao lingine linaloweza kunipa faida nzuri kwa kuuza ndani ya Mby au hata nje...
Pia naomba kujua naweza lima hekari ngapi kwa zao husika na kwa hako kamtaji kidogo...

natanguliza shukurani kwa ushauri wako
Nakushauri ulime majani ya mifugo haswa ya ngombe wa maziwa
 
Bei ya viazi inategemea na aina ya viazi unavyolima. Kwa sasa bei ya chini kabisa ni sh 50,000 kwa gunia likiwa shambani (kiazi aina ya Alika) na ya juu ni 75,000 (Tigo). Kila aina ya kiazi ina bei yake.
Ahsante ndugu Ako, vp Viazi vinaitaji mvua san?, na mtaji huo wa 3m unafaa kwa hekari ngapi rafiki..
Pia hekari moja inatoa gunia ngapi
 
Kwa 3m Usangu unaweza kulima mpaka ekari sita, kuanzia kukodi shamba, kulima, mbolea, mbegu na palizi. Ila inabidi upate mtu mwaminifu. Na mavuno ni kuanzia gunia 15 kwa ekari kwenda juu
Hapo ndio tatizo sasa..na huyo mtu sijui naweza kukubaliana nae nimlipe vipi..labda kwamba nimlipe baada ya kuvuna..na ni Tsh ngapi kwa msimu...cjui
 
Hapo ndio tatizo sasa..na huyo mtu sijui naweza kukubaliana nae nimlipe vipi..labda kwamba nimlipe baada ya kuvuna..na ni Tsh ngapi kwa msimu...cjui
Hiyo fedha inajumlisha na hela ya msimamizi. Mpunga sio gharama kama tunavyouwazia mchele. Nikisema msimamizi mzuri namaanisha asije akasema kaweka mbolea kumbe hola!! Manake ni component muhimu sana!!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Anhaa..ahsante ndugu Ako, mambo mengine yamuhimu kama kuweka mbolea n.k...nakuwepo mwenyewe.
Naomba nifahamishe bei ya mchele/mpunga kwa gunia ikoje...je, nauza mpunga au mchele?
Pia msimu wa kupanda mpunga ni upi...Nashkuru tena
 
Unaweza kuuza mpunga au ukakoboa uuze mchele. Bei inategemea na msimu, wakati wa mavuno inakuwa chini, lakini kama utavumilia huwa inapanda vizuri tu.
 
Ukiona vipi fanya mpango ufuge Hata kuku, mbuzi, au ng'ombe wa maziwa, kwa uzoefu Wangu kazi za Kulima huku unamtumia mtu hela kwa simu zinasumbua na usipokua makini utalizwa ,na unapotaka kilimo fanya tafiti za masoko uangalie bidhaa gani inakuaga adimu kuanzia miezi ya 7,8 nk usije ukaingia mkenge ulime mazao ambao wengi wamelima utapata hasara
 
Ahsante ndugu @saab, changamoto ya kufuga sina eneo la kufugia kwasababu naishi geto...labda niangalie hasa nitalima nini...
 
Kama eneo lina maji ya uhakika na uneza pata eneo km heka moja lima mahindi kwa lengo la kuuza mabichi inalipa, I have same plan niko mbeya pia!
 
Kama eneo lina maji ya uhakika na uneza pata eneo km heka moja lima mahindi kwa lengo la kuuza mabichi inalipa, I have same plan niko mbeya pia!
vp ndugu umefanya utafiti wowote kujua maeneo wanayofanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya?
 
HiZo takwimu ni fake ilo la kwanza price ya viazi imeshuka sn this year...pili mahindi hupati gunia hizo kwa eka ...nipo mbeya ...uyole hapa unapenda kulima nini wewe
 
Lima maharage ardhi ya mbeya ina rutuba sn hasa kwa kilimo cha maharage nimeshuhudia wakulim wakiweka mbolea ya DAp tu mpk kuvuna na wanavuna vzr tu naamini milion 3 itazaa pesa nyingi sn kwenye kilimo cha maharage
 
Lima mahindi,,usiangalie kwanza yanauzwaje maana mahindi hayajawah acha kununuliwa,ni chakula chetu kila siku so hayatakupa tabu sana,,hata ulimaji wake sio mgumu sana,,komaaa utafanikiwa ndugu nami nakuja mbeya nitafutie sehem wanayolima vitunguu nije nikae shamba kdgo
 
Kwa mtaji huo,, nakushauri ulime Tikitimaji. Inalipa sana, but yanahitaji umakini na uangalizi wa karibu
 
HiZo takwimu ni fake ilo la kwanza price ya viazi imeshuka sn this year...pili mahindi hupati gunia hizo kwa eka ...nipo mbeya ...uyole hapa unapenda kulima nini wewe
Ahsante mkuu...nilifikiria hasa nilime kiazi, labda naomba unifahamishe bei ya gunia la viazi nikiasi gani...
Pia naskia mahindi yakihudumiwa vizuri unaweza pata gunia hadi 30...
naomba ushauri wako mkuu
 
Back
Top Bottom