Naomba Mnishauri nilime zao gani

Naomba Mnishauri nilime zao gani

Haijawahi kutokea wakati wa mavuno bei kufika 110000/ ndo mwaka huu. Hiyo bei tuliizoea mwezi wa pili hadi watatu, mwaka Jana ilikomea 120000 lakin haikudumu sana ikashuka 100000_90000(ukiwa na mzigo mchache). Nna uhakika uvunaji ukichanganya inaweza ikashuka hadi 90000 kitu ambacho hakikuwa kawaida mana tulizoea wakat wa mavuno ni 50_55000
tuko pamoja mkuu tutachekiana kwa info zaidi
 
Mr Brown nakupa zoezi dogo tu kama kweli unataka kufanya kilimo. Kapunga si mbali na Mbeya mjini wikiendi hii fanya hima ufike huko kisha uende na maeneo mengine ambayo wanalima kwa kutegemea mvua tofauti kubwa utaiona vilevile utajifunza mawili matatu. Gunia inategemea, kuna magunia ya debe 6 debe 7 debe 8 debe 9 na debe 10. Mfano kwa Mbeya mara nyingi huwa wanatumia debe 6, dodoma debe 6,7 na 8 na Morogoro huwa wanaweka katika debe 6 hadi debe 10 kutokea hapo piga hesabu debe huwa ni kama kilo 18 mpaka 20 kutokana na mahindi yenyewe
Pamoja Mr Varius..

Natamani sana nitembelee maeneo hayo kwaajili ya kupata taarifa zaidi, na ninaimani ntafanya hvo soon

saizi nipo nje kidogo Mbeya
 
Mimi nalima mpunga kilimo cha umwagiliaji huku kwenye mashamba ya mwekezaji ya 'mbarali highlands estates' wilaya ya mbarali. Kilimo cha huku ni cha uhakika sana kuvuna ingawa kina gharama sana na inahitaji uangalizi wa karibu mno sio kulimia kwenye simu. Huku tunakodi tsh 275000/ kwa kila ekari na hapo unakuta shamba tayar limelimwa(limekatuliwa). Huku tunatumia sana mbolea na bila mbolea hupati kitu. Kwa hiyo mill 3 kwa huku unaweza kulima ekari 3 tu mkuu. Na hiyo ni nje ya hela ya kukodia. Ukilihudumia shamba vizuri kwa usimamizi mzuri kuanzia wakati wa kuandaa mbegu, kupanda (hapa muhimu sana), mbolea(muhimu sana), na kulinda ndege hadi kuvuna! Kwa kila ekari unaweza kupata gunia kuanzia 22_25. Ili kulima kitajiri na kila kitendo kufanywa kwa wakat sahihi basi kila ekari moja utatumia mill 1 maximum. Wasimamizi wapo wanapatikana kikubwa umpate anaeijua kazi ya kusimamia mpunga hasa ambaye hasubiri umwambie kitu, malipo ni makubaliano ingawa wengi wanapendelea kulipana kwa msimu na bei hutegemea ukubwa wa shamba. Kwa ekari 5 msimamizi wanarange kati ya laki 3_4 ila sana sana ni makubaliano. Soko LA mpunga lipo LA uhakika tu kikubwa ni uvumilivu tu wa kulisubiria soko lipande, miaka ya nyuma wakat wa mavuno kuna kipind bei hushuka adi hufikia tsh 50000 kwa gunia ila sasa iv I mean mwaka huu imefikia tsh 110000 na watu wanaendelea kuvuna ingawa bado hawajachanganya. Sasa iv wanavuna wale waliowahi kupanda tu. Wengine tunahesabu hadi kufikia mwezi wa sita katikati tuvune. Changamoto huku ipo kwenye upatikanaji wa mashamba tu. Wapo wale ambao wanakosa mashamba lakin wananunua kwa wale waliopata, that mtu kapata shamba ila uwezo wa kulilima hana au anapumzika kulima basi wew unalilinua kwake kwa kumpa hela ya kukodishia na 'cha juu', let say utampa ile 275000 ya kukodia shamba na kwa kila ekari unampa laki moja nyingine. Karibu Mbarali mkuu tulime.
Mkuu xplastaz nakushukuru sana...
Ningependa kufahamu hio 110,000/= ni bei ya Mbeya au Dsm...

Pili ningependa kufahamu huwa mna uza mpunga au mchele, kwamfano hio bei ni ya guniaa la mpunga au mchele?

Tatu naomba kufahamu ni mazao gani mengine yanayolimwa hapo Mbalali, na je kuna umwagiliaji wa uhakika katika mazao hayo mengine mbali na Mpunga
Nashukuru tena.
 
Nna ndoto kama zako, ntakuwa na mtaji wa millioni 4 niliwaza kulima mihogo mwezi wa 9 ili nivune mwezi wa tano kipindi cha mfungo panapo uzima, ntalima mihogo hekari 3 kwakuwa nna advantage ya kuwa na shamba sio la kukodi, pesa kiasi ntafanya ufugaji ili incase mambo yakiwa sawa mwaka ujao nnaamini ntakuwa na capital ya kutosha nifanye kilimo kwa kiwango kikubwa zaidi hasa mpunga na mihogo. Nna hofu ya kuingiza pesa yote sehemu moja kwa sasa cz mtaji ni wa manati aisee
 
Habari za kutwa ndugu zangu..
Mimi nikijana niliemaliza chuo na sina ajira, nmejichanga kwa muda sasa, nimepata million 3, sasa nataka kuingia kwenye kilimo ninaishi mkoa wa Mbeya.

Nmefanya kautafiti kidogo nikaona kuna eneo wanafanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya, ila nashindwa kuamua nilime zao gani iliangalau nikuze mtaji wangu kwakiasi kikubwa kidogo, binafsi nikaona bora nilime Viazi au Mahindi..

VIAZI
Kwa utafiti wangu mdogo nmeskia hekari moja ya viazi inatoa gunia 70-90 na mara ya mwisho gunia 1 nliskia linauzwa 62,000/= Mbeya.

MAHINDI
Pia hekari moja ya Mahindi inatoa gunia hadi 30 kama kila hatua ikifanywa kwa usahihi bei kwa gunia bado sijaifahamu.

Sasa nawakaribisha ndugu zangu wana Jf mnishauri nilime nini kwa mtaji huo, inaweza ikawa ni kati ya mazao nliyoyataja au zao lingine linaloweza kunipa faida nzuri kwa kuuza ndani ya Mby au hata nje...
Pia naomba kujua naweza lima hekari ngapi kwa zao husika na kwa hako kamtaji kidogo...

natanguliza shukurani kwa ushauri wako
Nakushauri pia pigia uzi wa kilimo cha mboga mboga hapo kwenye stick threads juu kabisa!! Utapa ujuzi pia!
 
Kuna mdau amekushauri Kulima mpunga ambapo naona ni ushauri mzuri. Uzuri wa mpunga hauna mahitaji mengi sana kama Mazao mengine. Ila sehemu utakayolima lazima iwe na maji ya uhakika. Swala la ndege inategemea na Eneo kwa mfano mie nimelima mambi nyuma ya igurusi msimu na tatizo la ndege sijalipata. Kwa kifupi hakuna utakachoamua kulima kitakuwa hakina changamoto, kila kitu kinachangamoto zake ni jinsi ya kujipanga kukabiliana nazo.
Ushauri wangu ukishaamua zao la kulima jaribu kulifanyia utafiti wake kwanza na usilewe na Yale mahesabu yetu juu juu ujione ushakuwa tajiri. Kuna changamoto nyingi ambapo usipojipanga utaamua. Ila ukifanya utafiti wako vizuri ukauliza na kwa watu waliolima jaribu kuanza na Eneo Dogo ili uweze kujifunza uzuri na changamoto za hicho kilimo. Mara nyingi msimu wa kwanza wa kilimo tunaita msimu wa kujifunza tu. Ili msimu wa pili uje ukiwa umeshajifunza vya kutosha.
Usikatishwe tamaa ndugu yangu inawezekana na changamoto kwenye Jambo lolote ni kawaida nikujipanga tu.
Ukipata wazo zao gani unataka kulima unaweza kuniambia kama nitakuwa na lolote la kukueleza nitakuambia Mimi napatikana Uyole.
 
Mimi nalima mpunga kilimo cha umwagiliaji huku kwenye mashamba ya mwekezaji ya 'mbarali highlands estates' wilaya ya mbarali. Kilimo cha huku ni cha uhakika sana kuvuna ingawa kina gharama sana na inahitaji uangalizi wa karibu mno sio kulimia kwenye simu. Huku tunakodi tsh 275000/ kwa kila ekari na hapo unakuta shamba tayar limelimwa(limekatuliwa). Huku tunatumia sana mbolea na bila mbolea hupati kitu. Kwa hiyo mill 3 kwa huku unaweza kulima ekari 3 tu mkuu. Na hiyo ni nje ya hela ya kukodia. Ukilihudumia shamba vizuri kwa usimamizi mzuri kuanzia wakati wa kuandaa mbegu, kupanda (hapa muhimu sana), mbolea(muhimu sana), na kulinda ndege hadi kuvuna! Kwa kila ekari unaweza kupata gunia kuanzia 22_25. Ili kulima kitajiri na kila kitendo kufanywa kwa wakat sahihi basi kila ekari moja utatumia mill 1 maximum. Wasimamizi wapo wanapatikana kikubwa umpate anaeijua kazi ya kusimamia mpunga hasa ambaye hasubiri umwambie kitu, malipo ni makubaliano ingawa wengi wanapendelea kulipana kwa msimu na bei hutegemea ukubwa wa shamba. Kwa ekari 5 msimamizi wanarange kati ya laki 3_4 ila sana sana ni makubaliano. Soko LA mpunga lipo LA uhakika tu kikubwa ni uvumilivu tu wa kulisubiria soko lipande, miaka ya nyuma wakat wa mavuno kuna kipind bei hushuka adi hufikia tsh 50000 kwa gunia ila sasa iv I mean mwaka huu imefikia tsh 110000 na watu wanaendelea kuvuna ingawa bado hawajachanganya. Sasa iv wanavuna wale waliowahi kupanda tu. Wengine tunahesabu hadi kufikia mwezi wa sita katikati tuvune. Changamoto huku ipo kwenye upatikanaji wa mashamba tu. Wapo wale ambao wanakosa mashamba lakin wananunua kwa wale waliopata, that mtu kapata shamba ila uwezo wa kulilima hana au anapumzika kulima basi wew unalilinua kwake kwa kumpa hela ya kukodishia na 'cha juu', let say utampa ile 275000 ya kukodia shamba na kwa kila ekari unampa laki moja nyingine. Karibu Mbarali mkuu tulime.

Mkuu ulichokiongea hapo juu hasahasa kwny gharama za ekari moja ni kweli kabisa. Na kwenye la mbolea nadhani unalifahamu Hilo kama usipotumia mbolea ya SA kwa mashamba ya highland estates mavuno yanakuwa madogo mno sababu Kubwa ikiwa eneo hili limekuwa na chumvi sana na siku hadi siku inazidi kuongezekA ndio maana kuna kuwa na ulazima wa kutumia mbolea ya SA. Ila bado wanalima na kupata mavuno Yao. Kwny maelezo yako hapo umenikumbusha baadhi ya vitu kwenye hayo mashamba
 
Tikiti usijaribu lima mazao ya chakula Wabongo kula matunda si jambo la kawaida ni anasa kubwa matunda bongo hii huliwa na makundi maalum tu ya watu ukikuta mtu ana kawaida ya kula matunda ni either ana kipato kikubwa na cha uhakika au ni mgonjwa yuko kwenye dozi
Daah umeongea ukweli mtupu, ila nimecheka sana jinsi ulivyowasilisha.
 
Mkuu ulichokiongea hapo juu hasahasa kwny gharama za ekari moja ni kweli kabisa. Na kwenye la mbolea nadhani unalifahamu Hilo kama usipotumia mbolea ya SA kwa mashamba ya highland estates mavuno yanakuwa madogo mno sababu Kubwa ikiwa eneo hili limekuwa na chumvi sana na siku hadi siku inazidi kuongezekA ndio maana kuna kuwa na ulazima wa kutumia mbolea ya SA. Ila bado wanalima na kupata mavuno Yao. Kwny maelezo yako hapo umenikumbusha baadhi ya vitu kwenye hayo mashamba
 
Mkuu xplastaz nakushukuru sana...
Ningependa kufahamu hio 110,000/= ni bei ya Mbeya au Dsm...

Pili ningependa kufahamu huwa mna uza mpunga au mchele, kwamfano hio bei ni ya guniaa la mpunga au mchele?

Tatu naomba kufahamu ni mazao gani mengine yanayolimwa hapo Mbalali, na je kuna umwagiliaji wa uhakika katika mazao hayo mengine mbali na Mpunga
Nashukuru tena.
Kwa sasa ni 100000 na hii ni bei ya huku mbeya nilipo, binafsi sijawah kufanya biashara ya mchele huwa nauza mpunga tu na hiyo bei ni kwa gunia LA mpunga sio mchele, huku mbarali mbali na kilimo cha mpunga pia kwa miaka ya hivi karibuni kilimo cha mabustani ya vitunguu, nyanya, matikiti, mboga mboga kimeshamiri kwel kuna sehemu panaitwa igawa kuna mashamba makubwa ya vitunguu eneo LA Igomelo. Kwa upande huo sijajua changamoto zao maana sijawah kulima mazao hayo kwa eneo hilo ambalo kwa huku ndo maarufu kwa kilimo hicho.
 
Mimi nalima mpunga kilimo cha umwagiliaji huku kwenye mashamba ya mwekezaji ya 'mbarali highlands estates' wilaya ya mbarali. Kilimo cha huku ni cha uhakika sana kuvuna ingawa kina gharama sana na inahitaji uangalizi wa karibu mno sio kulimia kwenye simu. Huku tunakodi tsh 275000/ kwa kila ekari na hapo unakuta shamba tayar limelimwa(limekatuliwa). Huku tunatumia sana mbolea na bila mbolea hupati kitu. Kwa hiyo mill 3 kwa huku unaweza kulima ekari 3 tu mkuu. Na hiyo ni nje ya hela ya kukodia. Ukilihudumia shamba vizuri kwa usimamizi mzuri kuanzia wakati wa kuandaa mbegu, kupanda (hapa muhimu sana), mbolea(muhimu sana), na kulinda ndege hadi kuvuna! Kwa kila ekari unaweza kupata gunia kuanzia 22_25. Ili kulima kitajiri na kila kitendo kufanywa kwa wakat sahihi basi kila ekari moja utatumia mill 1 maximum. Wasimamizi wapo wanapatikana kikubwa umpate anaeijua kazi ya kusimamia mpunga hasa ambaye hasubiri umwambie kitu, malipo ni makubaliano ingawa wengi wanapendelea kulipana kwa msimu na bei hutegemea ukubwa wa shamba. Kwa ekari 5 msimamizi wanarange kati ya laki 3_4 ila sana sana ni makubaliano. Soko LA mpunga lipo LA uhakika tu kikubwa ni uvumilivu tu wa kulisubiria soko lipande, miaka ya nyuma wakat wa mavuno kuna kipind bei hushuka adi hufikia tsh 50000 kwa gunia ila sasa iv I mean mwaka huu imefikia tsh 110000 na watu wanaendelea kuvuna ingawa bado hawajachanganya. Sasa iv wanavuna wale waliowahi kupanda tu. Wengine tunahesabu hadi kufikia mwezi wa sita katikati tuvune. Changamoto huku ipo kwenye upatikanaji wa mashamba tu. Wapo wale ambao wanakosa mashamba lakin wananunua kwa wale waliopata, that mtu kapata shamba ila uwezo wa kulilima hana au anapumzika kulima basi wew unalilinua kwake kwa kumpa hela ya kukodishia na 'cha juu', let say utampa ile 275000 ya kukodia shamba na kwa kila ekari unampa laki moja nyingine. Karibu Mbarali mkuu tulime.

kwanza kula senks kwa maneno ya busara {huu ndio tunauita u-great think sio kushauliana kulima bangi hapa} nimependa flow yako iko so nice.. pia unapenda ushirikiano thats very nice.. watu kama nyie na wengine wote walio toa +ve comments MUNGU huwa anawabariki kwa style ya mafanikio kwenye kazi za mikono yenu, nazan mtoa uzi atapata cha kufanya juu ya hili
 
Wote tunahangaika, kikubwa kupeana support kila mmoja kwa nafasi yake na uwezo wake. Tupo pamoja mkuu, big up
 
Back
Top Bottom