Naomba Mnishauri nilime zao gani

browwn

Member
Apr 25, 2017
35
27
Habari za kutwa ndugu zangu..
Mimi nikijana niliemaliza chuo na sina ajira, nmejichanga kwa muda sasa, nimepata million 3, sasa nataka kuingia kwenye kilimo ninaishi mkoa wa Mbeya.

Nmefanya kautafiti kidogo nikaona kuna eneo wanafanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya, ila nashindwa kuamua nilime zao gani iliangalau nikuze mtaji wangu kwakiasi kikubwa kidogo, binafsi nikaona bora nilime Viazi au Mahindi..

VIAZI
Kwa utafiti wangu mdogo nmeskia hekari moja ya viazi inatoa gunia 70-90 na mara ya mwisho gunia 1 nliskia linauzwa 62,000/= Mbeya.

MAHINDI
Pia hekari moja ya Mahindi inatoa gunia hadi 30 kama kila hatua ikifanywa kwa usahihi bei kwa gunia bado sijaifahamu.

Sasa nawakaribisha ndugu zangu wana Jf mnishauri nilime nini kwa mtaji huo, inaweza ikawa ni kati ya mazao nliyoyataja au zao lingine linaloweza kunipa faida nzuri kwa kuuza ndani ya Mby au hata nje...
Pia naomba kujua naweza lima hekari ngapi kwa zao husika na kwa hako kamtaji kidogo...

natanguliza shukurani kwa ushauri wako
 
Bangi inalipa sana sema jpm analeta wivu tu
Avatar yako jamaa yako huyo anatumiaga naye mmea? Mambo yake ya kifyokonoko sana huyo dogo.Aliwahi kuajiri mzinga kumtuliza mjomba wake kwa kupishana naye kwenye ushauri.Nasita kukubaliana na ushauri wako pia kwa jamaa.
 
Mi nakushauri ulime mpunga una soko sana hasa ukizingatia mchele wa mbeya huwa ni mzuri na bei yake huwa ya kuridhisha.
 
Angalia wakati wa mavuno je supply ya hilo zao unalotaka itakuaje sokoni,ikiwa ni hafifu lima zao hilo.
 
Mi nakushauri ulime mpunga una soko sana hasa ukizingatia mchele wa mbeya huwa ni mzuri na bei yake huwa ya kuridhisha.
Ubarikiwe ndugu..wasiwasi wangu juu ya mpunga ni naskia unahitaji uangalizi wakaribu sana..hasa ukizingatia kuna wale ndege...so itabidi nimuweke mtu kwa kazi hio na mtaji huo ni kidogo..

Pia vipi naweza lima hekari ngapi kwa mtaji huo ndugu
 
Habari za kutwa ndugu zangu..
Mimi nikijana niliemaliza chuo na sina ajira, nmejichanga kwa muda sasa, nimepata million 3, sasa nataka kuingia kwenye kilimo ninaishi mkoa wa Mbeya.

Nmefanya kautafiti kidogo nikaona kuna eneo wanafanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya, ila nashindwa kuamua nilime zao gani iliangalau nikuze mtaji wangu kwakiasi kikubwa kidogo, binafsi nikaona bora nilime Viazi au Mahindi..

VIAZI
Kwa utafiti wangu mdogo nmeskia hekari moja ya viazi inatoa gunia 70-90 na mara ya mwisho gunia 1 nliskia linauzwa 62,000/= Mbeya.

MAHINDI
Pia hekari moja ya Mahindi inatoa gunia hadi 30 kama kila hatua ikifanywa kwa usahihi bei kwa gunia bado sijaifahamu.

Sasa nawakaribisha ndugu zangu wana Jf mnishauri nilime nini kwa mtaji huo, inaweza ikawa ni kati ya mazao nliyoyataja au zao lingine linaloweza kunipa faida nzuri kwa kuuza ndani ya Mby au hata nje...
Pia naomba kujua naweza lima hekari ngapi kwa zao husika na kwa hako kamtaji kidogo...

natanguliza shukurani kwa ushauri wako
chukua ushaur katika hii ndoto yangu

napenda sana kujihusisha na kilimo ila muda wangu nahisi bado,ila siku ya kulima ikifika nitalima zao ambalo litakuwa na sifa hizi
>liwe ni zao la muda mfupi
>sitalima kwa kutegemea mvua
>zao litakuwa ni chakula kwa binadamu maana soko kidogo litakuwa la uhakika kuliko ya biashara
>litakuwa ni zao ambalo govt intervation wakat wa scarcity wa hilo zao haitakuwa kubwa sana maana madhala yake huwa makubwa sana
>nitalima zao ambalo machoni mwa watu wengi litakuwa linaonekana kama la la kipuuzi na halina faida
 
Jamani watu ambao ni wazoefu na mkoa wa Mbeya naomba mmusaidie ndugu yetu kwa ushauri, JF ni nzuri sana lakini kwa mtindo huu wa kudissapoint mtu akiwa na shida ya ushauri sio jambo zuri kabisa.
Hapa kuna majukwaa ya jokes ambapo unaweza kwenda kuchangia mada za utani ila kwa jambo la maana ni vizuri kama unaushauri uweke wazi, pia kama hujisikii kushauri ni vyema kutosema chochote ili usimkatishe tamaa muhusika ambaye anahitaji ushauri.
 
chukua ushaur katika hii ndoto yangu

napenda sana kujihusisha na kilimo ila muda wangu nahisi bado,ila siku ya kulima ikifika nitalima zao ambalo litakuwa na sifa hizi
>liwe ni zao la muda mfupi
>sitalima kwa kutegemea mvua
>zao litakuwa ni chakula kwa binadamu maana soko kidogo litakuwa la uhakika kuliko ya biashara
>litakuwa ni zao ambalo govt intervation wakat wa scarcity wa hilo zao haitakuwa kubwa sana maana madhala yake huwa makubwa sana
>nitalima zao ambalo machoni mwa watu wengi litakuwa linaonekana kama la la kipuuzi na halina faida
Ni zao gani hilo mkuu,, ushaur wako kuhus hilo zao ndio anaouhitaj zaid mtoa mada…!!
 
Ahsanten ndugu zangu...
Bado naendelea kusoma mashauri yenu...nawapenda sana
 
chukua ushaur katika hii ndoto yangu

napenda sana kujihusisha na kilimo ila muda wangu nahisi bado,ila siku ya kulima ikifika nitalima zao ambalo litakuwa na sifa hizi
>liwe ni zao la muda mfupi
>sitalima kwa kutegemea mvua
>zao litakuwa ni chakula kwa binadamu maana soko kidogo litakuwa la uhakika kuliko ya biashara
>litakuwa ni zao ambalo govt intervation wakat wa scarcity wa hilo zao haitakuwa kubwa sana maana madhala yake huwa makubwa sana
>nitalima zao ambalo machoni mwa watu wengi litakuwa linaonekana kama la la kipuuzi na halina faida
Naipenda ndoto yako ndg Kimbauzi...tatizo ni zao lipi linajibu maswali hayo
 
Ubarikiwe ndugu..wasiwasi wangu juu ya mpunga ni naskia unahitaji uangalizi wakaribu sana..hasa ukizingatia kuna wale ndege...so itabidi nimuweke mtu kwa kazi hio na mtaji huo ni kidogo..

Pia vipi naweza lima hekari ngapi kwa mtaji huo ndugu
Kulikuwa kuna jamaa anitwa Kubota angeweza kukupa mchanganuo, mi nimeangalia upande wa soko, ila uwangalizi wa karibu unahitajika haswaa kuepuka hasara na matarajio yanayokinzana kama unalima kwa kutumia "simu" inahitaji upate mtu mwaminifu wa kusimamia huo mradi.
 
Viazi shambani bei hushuka mpaka 30,000
....
Bei ya viazi inategemea na aina ya viazi unavyolima. Kwa sasa bei ya chini kabisa ni sh 50,000 kwa gunia likiwa shambani (kiazi aina ya Alika) na ya juu ni 75,000 (Tigo). Kila aina ya kiazi ina bei yake.
 
Back
Top Bottom