Naomba Mnishauri nilime zao gani

Naomba Mnishauri nilime zao gani

HiZo takwimu ni fake ilo la kwanza price ya viazi imeshuka sn this year...pili mahindi hupati gunia hizo kwa eka ...nipo mbeya ...uyole hapa unapenda kulima nini wewe
pia naomba kufahamu maeneo wanayofanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya
 
mkubwa usijiulize mara nyingi nyingi lima mahindi mpunga una kazi nyingi gharama kibao mimi nina experince nao lima mahindi yanazaa sana kuliko mpunga alaf bei yake haina tofauti sana na mpunga hasa kipindi cha kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa nne, tumia mbegu bora cheki mbegu za kampuni ya pannar seeds au dekalb mimi mwezi wa 6 naenda kuvuna mpunga wangu naachana nao naangalia kilimo cha mahindi kwenye mpunga nitarudi ila si kwa miaka ya hivi karibuni. Mpunga wa kwenye miradi unalipa sana ila ujiandae sana kimfuko, huo ndo ushauri wangu from my perspective and meagre experience. Alaf jamani asilimia 80 ya Watanzania nasikia ni wakulima lakini mada za kilimo haichangiwi kabisa. Mimi naombeni uanzishwe uzi madhubuti kwa ajili ya mbegu bora tu za mazao ya chakula yani 1.Mahindi 2.Mpunga 3.Maharage 4.Nyanya 5.Viazi
 
Tikiti usijaribu lima mazao ya chakula Wabongo kula matunda si jambo la kawaida ni anasa kubwa matunda bongo hii huliwa na makundi maalum tu ya watu ukikuta mtu ana kawaida ya kula matunda ni either ana kipato kikubwa na cha uhakika au ni mgonjwa yuko kwenye dozi
 
Ushauri wangu ,kwa mtaji huo Mkubwa, nakushauri ulime matikiti lakini kwenye mikoa ya Pwani na Morogoro,. Kukodi shamba ekari 2 kwa maana ya mashimo 2000 Tsh.200,000,usafi was shamba na mashimo Tsh. 200,000 mbolea ya kuku viroba 100@100,000+70,000usafiri. Halafu nunuambegu 500gm @ 250,000 sumu ya wadudu ya Tsh.150,000 bomba kupulizia dawa ,@40,000 . Kisha tafuta vijana 2 was kukusaidia kazi na hili maana yake uwanunulie chakula cha kula miezi 2 na kuwapangia chumba ambayo haizidi Tsh.200,000 huku mshahara unalipa 150,000@kila mmoja lakini baada ya mavuno. Ilikurahisisha kazi nunua water pump na mpira was kumwagilia ambapo gharama haizidi 500,000 kisha weka gharama ya Lita 20 za petrol. Kisha wasiliana nami uone maajabu
 
Habari za kutwa ndugu zangu..
Mimi nikijana niliemaliza chuo na sina ajira, nmejichanga kwa muda sasa, nimepata million 3, sasa nataka kuingia kwenye kilimo ninaishi mkoa wa Mbeya.

Nmefanya kautafiti kidogo nikaona kuna eneo wanafanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya, ila nashindwa kuamua nilime zao gani iliangalau nikuze mtaji wangu kwakiasi kikubwa kidogo, binafsi nikaona bora nilime Viazi au Mahindi..

VIAZI
Kwa utafiti wangu mdogo nmeskia hekari moja ya viazi inatoa gunia 70-90 na mara ya mwisho gunia 1 nliskia linauzwa 62,000/= Mbeya.

MAHINDI
Pia hekari moja ya Mahindi inatoa gunia hadi 30 kama kila hatua ikifanywa kwa usahihi bei kwa gunia bado sijaifahamu.

Sasa nawakaribisha ndugu zangu wana Jf mnishauri nilime nini kwa mtaji huo, inaweza ikawa ni kati ya mazao nliyoyataja au zao lingine linaloweza kunipa faida nzuri kwa kuuza ndani ya Mby au hata nje...
Pia naomba kujua naweza lima hekari ngapi kwa zao husika na kwa hako kamtaji kidogo...

natanguliza shukurani kwa ushauri wako
Wakati niko chuo mwaka wa mwisho mimi na jamaa zangu kadhaa tukakubaliana tulime,tukalima viazi Iringa na ilikuwa hekari tatu hivi!!
Changamoto zilikuwa nyingi lakini tulijitahidi sana kupambana nazo,sasa swala likaja kwenye kuuza mzigo yaan wanunuzi shambani wanataka wanunue gunia kwa sh.25000-30000 tukaona hapa hasara tukakubaliana tulete Dar kuuza kisha tukafanya taratibu zote mzigo ukaja ila ile kuvunwa kupakiwa na kusafirishwa mpaka dar kwa hako ka kipindi baadhi vikawa vimeanza kunyauka na hata kuanza kama kutoa majimaji hivi. Mzigo ukafika sokoni mabibo hapo tukakuta kwa hyo cku gunia linakwenda kwa 55000/- basi zikauzwa kadhaa hapo siku ikaisha kesho yake bei ikashuka mpaka 45000-50000/- zikazuzwa kadhaa yaan mpaka gunia la mwisho linauzwa tuliuza kwa 30,000/= tulikuwa hasara sana sitakaa kusahau.
Ushauri wangu lima mazao ambayo yana tunzika mfano mahindi,maharage ama mchele n.k mazao kama hayo kwenye swala la "Price flactuation"hautaathirika sana kulinganisha na viazi.
 
Ahsante sana kwa ushauri ndugu Varius..nmekuelewa sana, pia naomba unifahamishe uliposema bei ya mpunga na mahindi hazitofautiani sana, vipi bei zake kila moja kwa gunia ni kiasi gani

Pili, naomba kufahamu uliposema mpunga unalipa sana kwenye miradi..

Natanguliza shukurani.
 
nashukuru sana
 
Ahsante kwa ushauri ndugu...
Ingawa kwa tikiti natakiwa kucheza sana na hali ya soko...
Ahsante
 
Wakati niko chuo mwaka wa mwisho mimi na jamaa zangu kadhaa tukakubaliana tulime,tukalima viazi Iringa na ilikuwa hekari tatu hivi!!
Changamoto zilikuwa nyingi lakini tulijitahidi sana kupambana nazo,sasa swala likaja kwenye kuuza mzigo yaan wanunuzi shambani wanataka wanunue gunia kwa sh.25000-30000 tukaona hapa hasara tukakubaliana tulete Dar kuuza kisha tukafanya taratibu zote mzigo ukaja ila ile kuvunwa kupakiwa na kusafirishwa mpaka dar kwa hako ka kipindi baadhi vikawa vimeanza kunyauka na hata kuanza kama kutoa majimaji hivi. Mzigo ukafika sokoni mabibo hapo tukakuta kwa hyo cku gunia linakwenda kwa 55000/- basi zikauzwa kadhaa hapo siku ikaisha kesho yake bei ikashuka mpaka 45000-50000/- zikazuzwa kadhaa yaan mpaka gunia la mwisho linauzwa tuliuza kwa 30,000/= tulikuwa hasara sana sitakaa kusahau.
Ushauri wangu lima mazao ambayo yana tunzika mfano mahindi,maharage ama mchele n.k mazao kama hayo kwenye swala la "Price flactuation"hautaathirika sana kulinganisha na viazi.
Duh, aise pole sana...
Ahsante kwa ushauri mzuri....ila nahisi kipindi mnavuna, viazi vilikua vingi sokoni ndio maana bei ilikua chini kiasi hicho...au changamoto yakushuka kwa bei unahisi ilichangiwa na nini hasa mkuu....
 
Ahsante sana kwa ushauri ndugu Varius..nmekuelewa sana, pia naomba unifahamishe uliposema bei ya mpunga na mahindi hazitofautiani sana, vipi bei zake kila moja kwa gunia ni kiasi gani

Pili, naomba kufahamu uliposema mpunga unalipa sana kwenye miradi..

Natanguliza shukurani.
Bei ya mahindi kuanzia kipindi cha mwezi wa 1 na kuendelea ni huwa linaanzia 15000 mpaka 25000 kutegemea na mikoa la mpunga nalo hucheza kuanzia 15000 mpaka 30000 kutegemea na mikoa pia lakini wewe ukiwa mkulima advantage ni kwamba mahindi huzaa sana kushinda mpunga na ishu nyingine ni kwamba mpunga una kazi nyingi sana lakini kwa mahindi ni kupanda,palizi mara mbili na kuweka mbolea
 
Duh, aise pole sana...
Ahsante kwa ushauri mzuri....ila nahisi kipindi mnavuna, viazi vilikua vingi sokoni ndio maana bei ilikua chini kiasi hicho...au changamoto yakushuka kwa bei unahisi ilichangiwa na nini hasa mkuu....
Mkuu brown hii ni changamoto ya kulima mazao ambayo yanaharibika huwezi kuhifadhi, unajua hata walanguzi wakiamua kusema gunia la viazi sh.5000 unajua unakosa jinsi kabisa ni lazima uuze rasmi hivyo vitakuozea ila kama unataka kulima mazao ambayo ni rahisi kuharibika basi ni lazima ulichunguze soko kwanza kisha ujitahidi sana kulima eneo kubwa kawa gharama ndogo hapo waweza ona faida mfano mzuri wale wakulima wakubwa wanaolima nyanya za msimu
 
Nakushauri ulime majani ya mifugo haswa ya ngombe wa maziwa

Kuongolea kuhusu hilo, nilikuwa nafanya uchunguzi kuhusu mahindi.
Kuna video nikaona YouTube jamaa analima mahindi , halafu yakikomaa, kuna mashine inakuja inasaga mahindi na majani yake kuwa kama unga, halafu wanawapa ng'ombe.
 
Brown kilimo cha mpunga katika schemes za umwagiliaji unalipa sana sababu miundombinu ya mashamba ni mizuri na maji ni uhakika, mpunga ni zao linalohitaji sana maji katika kipindi cha kuanza kutunga mpunga, wakulima wenyewe wanaita kipindi cha mpunga kubeba mimba hivyo unakuta kama umelima kwa kutegemea mvua na mvua zikakoma au kupungua basi kipato chako cha magunia kinaweza athirika lakini kwenye schemes maji ni uhakika mashamba yako level nzuri na vifaa kama planters, powertiler,na combines huwa zinapatikana mfano mzuri ni huko mbeya kapunga rice
 
Habari za kutwa ndugu zangu..
Mimi nikijana niliemaliza chuo na sina ajira, nmejichanga kwa muda sasa, nimepata million 3, sasa nataka kuingia kwenye kilimo ninaishi mkoa wa Mbeya.

Nmefanya kautafiti kidogo nikaona kuna eneo wanafanya kilimo cha umwagiliaji ndani ya Mbeya, ila nashindwa kuamua nilime zao gani iliangalau nikuze mtaji wangu kwakiasi kikubwa kidogo, binafsi nikaona bora nilime Viazi au Mahindi..

VIAZI
Kwa utafiti wangu mdogo nmeskia hekari moja ya viazi inatoa gunia 70-90 na mara ya mwisho gunia 1 nliskia linauzwa 62,000/= Mbeya.

MAHINDI
Pia hekari moja ya Mahindi inatoa gunia hadi 30 kama kila hatua ikifanywa kwa usahihi bei kwa gunia bado sijaifahamu.

Sasa nawakaribisha ndugu zangu wana Jf mnishauri nilime nini kwa mtaji huo, inaweza ikawa ni kati ya mazao nliyoyataja au zao lingine linaloweza kunipa faida nzuri kwa kuuza ndani ya Mby au hata nje...
Pia naomba kujua naweza lima hekari ngapi kwa zao husika na kwa hako kamtaji kidogo...

natanguliza shukurani kwa ushauri wako
Milion 3 nyingi sanaa mkuu kama upo mbeya fanya hivi
Chukua laki tano nenda uyole uliza karoti zinapotoka watakuelekeza shamban wanauza 35000 hadi 37000 nampka uifikishe ilala sokoni ni 60000 mpka 65000.hukosi faida hapo na gharama ya usafiri kwa kiroba cha karoti haizidi 17000 mkuu.kuliko ukalime na kusubiri mavuno weka hela kwenye vitu unavyoviona tayari.
 
Mr.Brown kama mfuko una ruhusu sogea kapunga rice uwahi block yako mapema kilimo ni cha uhakika ila kama una mtaji huo uliosema hapo juu aanza kidogo na eka 5 mpaka 8 za mahindi tumia mbegu za kisasa piga mbolea ya kutosha kisha muombe sana Mungu alaf utuletee mrejesho na experience yako, mimi pia mwakani nitasonga kwenye mahindi nikivuna nitakuja tena kumwaga experince yangu sitaacha kufanya hivyo.
 
Milion 3 nyingi sanaa mkuu kama upo mbeya fanya hivi
Chukua laki tano nenda uyole uliza karoti zinapotoka watakuelekeza shamban wanauza 35000 hadi 37000 nampka uifikishe ilala sokoni ni 60000 mpka 65000.hukosi faida hapo na gharama ya usafiri kwa kiroba cha karoti haizidi 17000 mkuu.kuliko ukalime na kusubiri mavuno weka hela kwenye vitu unavyoviona tayari.
Huu pia ushauri mzuri kama ana nafasi lakini kwanini usimshauri apeleke mchele au maharage hizi mali kuoza hiz
 
Back
Top Bottom