Chris Lukosi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 4,581
- 2,937
Ndugu zanguni,
Sasa mwaka 2013 ndio unakatika na ni masaa machache tu kabla hatujaingia mwaka mpya 2014
Ningependa kutumia fursa hii kuwashukuru wale wote walionisapoti mwaka huu 2013 bila kusahau wagonga like na wale walioniwezesha kulitumia jukwaa hili kutoa maoni yangu.
Nawashukuru sana bodi nzima ya Jamii forums kwa kutuwezesha sisi watanzania wadogo kwa wakubwa, walio ndani na walio nje, chadema kwa ccm na wengineo kuweza kupata fursa ya kutoa maoni yao juu ya siasa za nchi yetu. Mungu awabariki na kuwaongezea busara za kuzuia machafuko na mupate uwezo wa kujua na kufuta thread yoyote itakayoleta madhara kwa jamii kwani sasa JF ni kubwa mno na ninaamini hata viongozi wetu hutembelea sana hapa.
Pia nawaomba wale wote niliowakwaza kutokana na coments zangu hapa jukwaani kwani najua kabisa kuwa coments zangu zinaweza kuwa nzuri kwa kambi yangu lakini zikawa mwiba mchungu upande wa pili. Naomba mnisamehe kwani bila kuelezana ukweli hatutafika.
Mimi pia nawasamehe wale wote hata walioniita mwizi wa rambi rambi nilizotoa mfukoni mwangu kujazia kidogo walichotoa akina chadema UK.
Baada ya hayo yote naomba niwatakie heri ya mwaka mpya 2014.
Namuomba Mwenyezi Mungu alijalie taifa letu amani kipindi hiki kijacho ambapo tutakuwa tunaingia kwenye katiba mpya
Namuomba Mwenyezi Mungu amzidishie hekima Rais wetu na bunge la katiba waweze kutuletea katiba itakayomnufaisha kila mwananchi bila kubagua Chama au dini.
Namshukuru sana Rais wetu kwa kutuletea katiba mpya
Ndugu zanguni, pia nningeomba viongozi wengine wa kisiasa waige mfano wa waheshimiwa Anna Tibaijuka, Mmwigulu Nchebma, Dr Wilbroad Slaa , Zitto Kabwe , Hamis Kigwangala na wengineo kwa kuamua kujumuika nasi kwenye jukwaa la siasa kuchangia hoja na kubadilishana mawazo kwani naamini kuwa hapa pamoja na kuwa kuna mbulumundu wengi lakini pia kumejaa great thinkers ambao mawazo yao yakisikilizwa yanaweza kusaidia katika kurekebisha pale panapopwaya nchini
MUNGU AWABARIKI WOTE
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU TUEPUSHE NA MACHAFUKO NA UENDELEE KUTUJALIA UWEZO WA KUVUMBUA RASILIMALI ZAETU KAMA MAFUTA NK 2014
ASANTENI.
Chris Lukosi.... kalenga - Iringa