Naomba mnisaidie kupendekeza jina zuri na 'unique' la mtoto wa kiume wa Kiislam

Wanabodi salaam! Nimefanikiwa kupata mtoto wa kiume, sasa kwa jinsi nilivyokuwa na furaha na ujio wake natamani nimpe jina zuri na la kipekee. Najua humu ndan kuna wajuvi wengi so karibuni sana
Sadam au Osama
 
bwana ukasha alioa na pia aliolewa Huyu na akazaa watoto enzi za bwana mtume Muhammad s.a.w kisa chake mpaka akaolewa kinanifurahisha sanaaa
Alitaka kujua kati ya mwanaume na mwanamke nani anaskia raha wakati wa kugegedana akajikuta kabadilika mwanamke na akaolewa
 
Wanabodi salaam! Nimefanikiwa kupata mtoto wa kiume, sasa kwa jinsi nilivyokuwa na furaha na ujio wake natamani nimpe jina zuri na la kipekee. Najua humu ndan kuna wajuvi wengi so karibuni sana
"Mtanzania."
 
Wanabodi salaam! Nimefanikiwa kupata mtoto wa kiume, sasa kwa jinsi nilivyokuwa na furaha na ujio wake natamani nimpe jina zuri na la kipekee. Najua humu ndan kuna wajuvi wengi so karibuni sana
Majina mazuri na ya kipekee yote yametumika.

Anza na majina ya mitume,kisha ya maswahaba wa mtume kisha ya waja wema.
 
Kuna majina nimeyafikiria kama Aaban au Abiy pia naomba ushauri juu ya hayo majina hapo
Abiy maana yake "Baba yangu" kwahiyo halina maana kumuita mtoto.

Hili "Aaban" nahisi ulikusudia "Aabun" hili maana yake "Baba".

Shukrani.
 
Hakuna jina la Kiislam wala Kikristo- hayo majina ni ya watu waliokuwepo hata kabla us Qur'ani kuwepo.Mfano Abdalla lilikuwepo Mtume Mohamed hajazaliwa, hata jina Mohamed lilikuwepo kabla ya kuitwa kuwa Mtume Tusidanganyike tafuta jina zuri hata la lugha au Kiswahili. Huwi Mwislamu mzuri kwa kumpa mtoto wako jina la Kiarabu au lililoandikwa kwenye Qur 'an. Uislamu ni imani kwa mungu sio kwa jina.
Watu tubadilike kuanza kutumia majina yetu na bado tutakuwa waislamu wazuri.
Tuache kutawaliwa na utamaduni wa majina ya nje.
Wewe unafikiri jina ni nini? Jina ni neno lo lote unalotoa kwa mtu au kitu
Tafuta neno lo lote unalopenda mpe mtoto.
Mfano labda umepata jina Ahmad unalipenda tafuta maana yake kwa Kiswahili au lugha yako mpe mtoto wako. Akikua tutapata watu mashuhuri Kama waliomo humo kwenye vitabu au hapa duniani
Majina ya Kiislamu kijana,ndiyo maana Mtume wapo baadhi ya maswahaba wake aliwabadilisha majina.

Vile vile mtume ametuusia tuwape watoto wetu majina mazuri kama vile Abdullah,Abdulrahman. Tafuta kitabu kiitwacho "Tasmiyaat al Mawluud" cha sheikh Bakar Abuu Zayd ameelezea adabu za kuwapa watoto majina. Mambo msiyo kuwa na ujuzi nayo msiwe mnayaongelea.
 
Mpe jina la asili mkuu dini mfundishe muda umefika sasa waafrika tuzinduke tusiache kila kitu chetu kizuri tukafuata kuanzia tamaduni, mila , lugha, mavazi na majina ya waliotuletea dini. Wao hayo majina ni ya asili kabisa kama sisi tuliyo na ya asili na hayana uhusiano wowote na imani
Dina haina uafrika wala uarabu. Ukweli usemwe majina mengi ya waafrika hayana maana nzuri bali ya hovyo.
 
majina mazuri ya mababu zenu, walio waleta dunian, hamuyataki, mmekazana na majina ya jamii za mbali ambazo hata dini zao haziwatambui..shame on you, mambo mengine mnayafanya baht mbaya kwakujua ama kutokujua, effects zake ni kwa watoto hao, wanakosa baraka za maisha sabbu ya imani,

wanakosa baraka sabbu ya kuwapa utambulisho feki, ambao wamiliki wa huo utambulisho kiroho hawawatambui, nishasemaga hapa, Mungu mgeni hawez kukubariki kama wew upo nje ya jamii na tamaduni ya wahasisi wa iyo imani, nikatolea mfano kwa wakikristo, kuna hao mayahud mnaosema wamebarikiwa baraka toka kwa ibrahimu, na ili uwe sehem ya baraka izo lzma uwe muisrael, au ufanye jambo fulan fulan ndpo utazpata, ukikosea utaangaika kuwa fukara kama hawa walokole mitaani na hutopata kitu, maana umeingilia imani ya tamaduni ilyo nje yako, na hutambulik.

niliongelea pia hata kwa islamic ni hivyo hivyo, yaan ukitaka uwe recognized na hiyo iman, unakuta mtu kabadirishiwa mpak jina lake na kupewa jina la watu wa uko uarabuni kuonesha kuwa kwa uhalisia wako, hutambuliki mpka ufanye mambo fulan fulan ndpo miungu ya jamii hiyo itakukubali.

nachotaka kusema ni kuwa, jmn tupende vya kwetu, utumwa ulikwisha, izo imani za kuiga iga si nzur hata ushahid upo, ni bora ukampa mtoto hata jina la lolote lenye asili ya afrika(black people) ama jina la kiswahili ambalo unajua maana yake, nikwambie tu ukweli kila jina lina maana yake kwa kugha yake tuu FULL STOP, ndiomaana majina ya wahindi,wachina na wakorea hutoona yakibadirishwa sabb ya lugha ili kuendana na maana ya jamii fulan lkn yanaweza kutafsiliwa yanamaanisha nini kwa lugha ya sehem husika lkn si kubadirishwa, ndiomaana hutoona jina la Muhammad likiitwa kwa kingereza wala lugha yyte, zaid ya asili yake.

tabia ya kubadir majina kulingana na eneo, wanayo watu wa magharib na USA napo walianza kufanya il kuficha na kubadiri uhusika wa historia za jamii fulani.

wote mnaobeza haya mambo, mjue mnamkosea Muumba kwa kuikataa asili yenu na kukumbatia upumbv wa ugeni ambao hata hauna maana.

ukwel mchungu huu ushaur ukiuzingatia nakuhakikishia uyo mtoto wako atakuja kuwa mtu muhimu sana kwenye jamii, lkn ukipenda kuiga iga, ndyo hayo mnapata watot wenye tabia za akina, aisha, john mkabaji, muhamed mbakaji, musa mpiga ramli, yoshua mla wake za watu, ibrahimu tapeli, grace malaya, khareem mwizi, alhaji jambazi, Aziza tapel wa waume zawatu, magret mtoa mimba, na takataka znginezo,

we niletee jinalolote lenye asili ya hao watu nami nikuletee maana yake kulngana na wahasisi wa hayo majina.

kuweni wazalendo, utumwa wa akili ushafika mwisho, kama wao hawawez tumia jina la babu yako, why ww utumie yakwao??

ukweli mchunguView attachment 1970337
Hiki kituko kingine,jf kuna watu wajinga sijapata kuona sehemu nyingine yoyote.
 
Imam Malik jina lake kamili anaitwa Abdullah-Malik ibn Anas kumuita malik ni mazoea ila ni makosa Malik ni miongoni mwa majina ya mwenyezi Mungu maana yake ni (mmiliki) kwakua yeye ndo mmiliki wa kila kitu ila kwa binadam ni lazima iongezewe Abdul maana ya Abdul ni (mja/kiumbe) kwahiyo AbdulMaliQ maana yake (mja wa mmiliki)
Imam Malik jina lake ni hilo hilo Malik, Abdullah hapo umechanganya, hiyo ilikuwa ni kun-ya yake ambayo ni Abu Abdillah yaani Baba Abdillah. Hivyo jina lake hasa ni Malik na Abu Abdillah ilikuwa ni Kun-ya yake.
 
Wanabodi salaam! Nimefanikiwa kupata mtoto wa kiume, sasa kwa jinsi nilivyokuwa na furaha na ujio wake natamani nimpe jina zuri na la kipekee. Najua humu ndan kuna wajuvi wengi so karibuni sana
Mpe jina AZHAR.
Hii ina maan ya nyota ing'aayo angani, mzuri na mwenyekupendwa.
 
Back
Top Bottom