Naomba maoni yenu kuhusu ajira kwa vijana nchini

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Nina wazo au proposal ambayo inahusu mradi mkakati mdogo utakaohusu kilimo na ufugaji kwa vijana waliohitimu vyuo nk.

Kama mnavyojua tatizo kwenye jamii ni fursa pia tena kubwa nimeandika proposal ambayo itakuwa inakusanya vijana kuanzia 50-100 kufanya kwa pamoja mradi wa kilimo na ufugaji.

Kilimo kitakuwa cha mazao yanayowahi kuvunwa na mazao biashara pia mboga mboga. Ufugaji ni wa Ndege na wanyama hii itakuwa kama backup wakati vijana wanasubiri kuvuna basi kuwe na ufugaji utakaokuwa unawaingizia kipato na kulipa kama ni mkopo wamechukua.

Mradi kama huu nimefikiria ufanyike kwa kila wilaya kisha kila kata.

Sasa naomba maoni yenu mi nilifikiria kwenda kuzungumza na mkurugenzi na mkuu wa wilaya niliyopo nione kama wanaweza kutoa ushirikiano.

Wilaya niliyopo ipo mkoa wa Kagera niliwahikutana na kiongozi mmoja wa kijiji akasema maeneo yapo unaweza omba ukafanya shughuri zako ukimaliza unarudisha yaani maeneo ya kijiji.

Pia nahitaji maoni je tunaweza kupata wapi connection ya kupata mkopo wa kuanzia na ndo maana nilitaka ends zungumza na mkurugenzi na mkuu wa mkoa si mnajua pia rais alisema kilimo kwa vijana ili kupunguza changamoto ya ajira.

Sasa naomba maoni yenu nianzie wapi.

Pili nataka vijana waliotayari kwa kushirikiana tupambane mpaka tufanikishe mradi wawe wilaya ya Biharamulo au katoro au mureba au bukoba ambao wanaweza pia kuwa na mawazo chanya tunafanyaje.

Tatu ambaye anajua tunaweza pata wapi connection ya kupata mahitaji ya mradi ikiwemo vifaa na pesa hata kama ni mkopo ikiwa mtoaji atakubaliana na proposal.

NB: mradi natamani uwe mfano kwa vijana wote nchini na uigwe.

Piga simu au tuma ujumbe hapa

0715774965.
 
Achana na maneno ya wanasiasa wewe, ninani atakupa MKOPO hauna dhamana yoyote hapa bongo? Toa kitu upate kitu ndo kauli mbiu ya Africa continent.
 
Tafuta kwanza dhamana kabla ya mkopo.
Mkopo bila dhamana kwa vijana unapatikana Ulaya, china au uarabuni kwa vijana wao sababu ya mifumo yao
 
Tatizo la ajira nchini ni kubwa sababu ya ukosefu wa uwiano wa matumizi ya raslimali zilizopo na idadi ya vijana.Raslimali ni nyingi Sana kuliko idadi ya wasio na ajira ya kuzalisha.
 
Pesa zipo tele, nguvu Kazi ipo tele, masoko yapo tele, raslimali zimejaa tele.
Shida wakiacha ubinafsi, tatizo la ajira nchini ni historia.
 
Ndani ya miaka 3 jinsi ya kuleta maendeleo na kumaliza tatizo la ajira nchini.

1.Ondoa futa kodi zote za kuingiza magari ya mizigo na abiria nchini kodi yake utaipata mara mbili yake kupitia indirect tax.Kwenye mafuta,leseni za udereva,fine za traffic, parking fee,ushuru wa stand,spare za magari,leseni na vibali mbalimbali.Gari moja uajiri si chini ya vijana 3.

2.Toa ruzuku kwenye viwanda vya kuzalisha matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei trekta moja uajiri zaidi ya watu wanne.

3.Jenga schemes za umwagaliaji KILA kijiji upitapo mto pande zote mbili watu walime mwaka mzima ni aibu sana kwa maji ya mito kumwaga maji yake baharini badala ya mashambani.Soko la mazao nje ya nchi lipo tele

4.Jenga vyuo vya ujuzi kila kata kopesha vijana ujuzi baada ya kumaliza darasa la saba wakapate ujuzi wautakao.

Kukopesha vijana waende chuo kikuu kisha warudi mtaani kuendesha bodaboda na kuwa machinga ni upotevu Mkubwa Sana wa kodi zetu na kuongeza idadi ya masikini nchini.

5.Fungua mipaka watu wauze watakapo nje ya nchi kuna masoko tele.Legeza masharti ya vibali Ili export ikue.

Ni sekta mbili tu zingine takataka hazifikii kilimo na madini kwa kuajiri vijana wote nchini na kuongeza pato la taifa bila kutegemea kukopa na kukamua kodi wananchi.

6.Peleka KILA kijiji mashine za kutengeneza interlocking block na vigae Ili watz wote wajenge nyumba bora kwa gharama nafuu kabisa

Mjerumani kwa miaka 15 alituletea maendeleo makubwa Sana ccm imeshindwa nini kwa miaka 60,jibu ni ubinafsi ndo tatizo.
Tilioni moja ya kununulia ndege ingetosha kuajiri vijana milioni 12 nchi nzima,na ingezaaa mara tatu yake ndani ya mda mfupi.
 
Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.
 
Back
Top Bottom