kwenye keyboard hapa huwezi ku-explore kila kitu. nakushukuru kuwakilisha na umesomeka mkuu. pamoja sana
Miss Judith nadhani neno kufariki ni sahihi, huwezi kuweka neno kufa kama mbadala wa kufariki, mfano ukitaka sema kuwa fulani "kafa", ni sahihi kusema "fulani kafariki dunia" , japo hata neo kufa ni sahihi hasa kueleza tendo la kufariki!
Hapa nadhani sahihi ni ....ama....au... Neno aidha, lina maana na matumizi tofauti.10. aidha... au..., sahihi ni aidha,..../......au......
Glory to God
Hapa nadhani sahihi ni ....ama....au... Neno aidha, lina maana na matumizi tofauti.
Wataalamu wa kudadavua kiswahili hukubaliana kwa jambo hili: kiswahili cha bara hakifanani kwa kila kitu na kile cha visiwani ila vyote ni sanifu kulingana na sehemu. Mfano; markiti na soko, nyimbo na wimbo, afisi na ofisi,skuli na shule, jaa na jalala.... Ahsanteni sana kwa utulivu wenundugu yangu BAK yote ni sahihi na yana maana tofauti. swala linatokana na mambo ya ibada hasa ya kiislamu, kwa ibada za kikristu wanatumia sala zaidi lakini yote yana maana sawa au inayokaribiana na prayer/worship kwa kingereza. ila hilo la pili la "suala" linamaanisha " an isshue" kwa kiingereza na wingi wake ni masuala yaani issues. huo ndio usahihi wake na yapaswa kutumika hivyo kote bara na visiwani.
Glory to God
Dada Judith nakubaliana na wewe kwamba kila lugha ina kanuni zake za kisarufi. Aidha, nakubaliana na wewe kuwa watu wengi huchanganya matumizi ya maneno aidha..au kwa kudhani yana ufanano na maneno either ...or.. ya lugha ya kiingereza. Kama nilivyobainisha awali maneno ya kiswahili yanayotumika kwa kanuni ile ile ya kiingereza ya matumizi ya maneno either ...or.. ni ama....au....Kwa mfano:-mpendwa, kila lugha iliyosanifiwa ina kanuni zake za kisarufi. sarufi ya kiswahili na kiingereza ni tofauti. wengi wanatumia "aidha... au..." kwakufuatisha sarufi ya kiingereza ya ".... either... or...." ukitumia "aidha" hupaswi kutumia "au" pia ukitumia "au" huhitaji kutumia "ama". mifano ifuatayo inafafanua zaidi juu ya matumizi ya maneno haya:
1. aidha, mheshimiwa spika alinukuu kanuni ya 68 na kumzuia mh. lema kuzungumza
2. mh. spika alimtaka mh. lema kutoa ushahidi wa madai yake hayo au kufuta kauli yake
3. mh. spika alifafanua kuwa mh. lema anatakiwa kutoa ushahidi wake papo hapo ama atakabiliwa na azimio la bunge
NB:
wengine pia huchanganya na kusema mfano
a) "mh. spika alifafanua kuwa mh. lema anatakiwa kutoa ushahidi wake papo hapo ama sivyo atakabiliwa na azimio la bunge"
hayo nayo ni makosa. usahihi wake ni:
b) "mh. spika alifafanua kuwa mh. lema anatakiwa kutoa ushahidi wake papo hapo la sivyo akabiliwa na azimio la bunge"
nadhani tuko pamoja sasa
Glory to God
Nina swala kuhusu sarufi.
ipi ni sahihi ?
"The novel that she's writing":
1. "Riwaya anayoiandika"
2. "Riwaya anayoandika"
"the book she's reading":
1. "Kitabu anachokisoma"
2. "Kitabu anachosoma"
Yaani, if the subject is carrying out an action on the direct object, is it enough to just put the "o"- of reference (=yo, cho, etc.) in the verb or does the object infix (=yoi, choki, etc.) have to be there too?
It confuses me because i've seen people do both, it's like there's no correct rule and people just write what they want to write...
mazoea yanaweza kufanya maneno fulani yaonekane kuwa yanatumika kwa usahihi, lakini ukweli ni kinyume chake. mfano haya yafuatayo"
1. siyo, sahihi ni sio
2. ndiyo, sahihi ni ndio
3. ndio yeye, sahihi ni ndiye yeye
4. ndio wewe, shihi ni ndiwe wewe
5. ndio mimi, sahihi ni ndimi mimi
6. hichi, sahihi ni hiki
7. liwalo lote, sahihi ni lolote liwalo
8. onyesha, sahihi ni onesha
9. maonyesho, sahihi ni maonesho,
10. aidha... au..., sahihi ni aidha,..../......au......
11. siyo... wala...., sahihi ni si.... wala.....
12. kufariki, sahihi ni kufa
13. (fulani) anachechemea, sahihi ni (fulani) anachehechema/anachechemeka
14. shuka juu, sahihi ni shuka chini
15. toka nje, sahihi ni tokea nje/toka ndani
16. ukweli, sahihi ni kweli
17. uoga, sahihi ni woga
18. nk.
wengine mwaweza kuongeza ama kusahihisha.
wapendwa tukienzi kiswahili.
Glory to God
nakubaliana nawe kuhusu kiswahili cha bara na visiwani. Lakini, kuhusu nyimbo na wimbo sikubaliani nawe. Wimbo ni umoja wakati nyimbo ni wingi. Kwa hiyo "wimbo wa JD ni mzuri sana". Nyimbo za JD ni nzuri sana" Hii dhana ya watu kusema "ile nyimbo yake niliipenda" ni uharibifu wa lugha. Hakuna upatanishon wa sarufi hapo (wingi na umoja). Nachukia sana watu wa redioni wanaposema hivyo.Wataalamu wa kudadavua kiswahili hukubaliana kwa jambo hili: kiswahili cha bara hakifanani kwa kila kitu na kile cha visiwani ila vyote ni sanifu kulingana na sehemu. Mfano; markiti na soko, nyimbo na wimbo, afisi na ofisi,skuli na shule, jaa na jalala.... Ahsanteni sana kwa utulivu wenu
Hapa nadhani sahihi ni ....ama....au... Neno aidha, lina maana na matumizi tofauti.
Nachelea kukubaliana nawe kwa kila kitu. Mf. ndiwe tayari limebeba ile dhana ya wewe ndani yake. Huwezi kusema ndiwe wewe utakuwa umerudia neno wewe mara 2. kwa hiyo ndio wewe ni sahihi pia likimaanisha ndiwe. Pili tokea nje unamaana tokea nje uelekee ndani, wakati dhana ambayo unataka kuizungumzia hapa ni elekea nje. toka ndani ni sahihi pia. Na pia kuna mengine machache ambayo sikubalini nawe hapo juu. Inaonekana wewe unatumia kiswahili cha lahaja fulani zaidi na utaipenda zaidi hiyo ukiamini ndicho sahihi.
Originally Posted by Omukuru
Miss Judith nashukuru umeleta huu mjadala mzuri kabisa. Pamoja na uzuri wa mjadala nina mashaka na usahii wa maana na matumizi ya baadhi ya maneno uliyoyaleta hapo juu.
Mimi nafahamu kwamba neno kama NDIMI tayari liko nafsi ya kwanza umoja. Linatokana na muungano wa kivumishi kitenzi-nomino thibitishi: NDIO na kiwakilishi nafsi MIMI
NDIO+WEWE = NDIWE
NDIO+HII/HIYO = NDIYO
Neno UKWELI liko sahii, na wingi wake ni KWELI. Maana inategemea sana
Nitarudi hapa jamvini kuendeleza uchambuzi na kuleta vielelezo na vyanzo vya maelezo yangu.
mazoea yanaweza kufanya maneno fulani yaonekane kuwa yanatumika kwa usahihi, lakini ukweli ni kinyume chake. mfano haya yafuatayo"
1. siyo, sahihi ni sio
2. ndiyo, sahihi ni ndio
3. ndio yeye, sahihi ni ndiye yeye
4. ndio wewe, shihi ni ndiwe wewe
5. ndio mimi, sahihi ni ndimi mimi
6. hichi, sahihi ni hiki
7. liwalo lote, sahihi ni lolote liwalo
8. onyesha, sahihi ni onesha
9. maonyesho, sahihi ni maonesho,
10. aidha... au..., sahihi ni aidha,..../......au......
11. siyo... wala...., sahihi ni si.... wala.....
12. kufariki, sahihi ni kufa
13. (fulani) anachechemea, sahihi ni (fulani) anachehechema/anachechemeka
14. shuka juu, sahihi ni shuka chini
15. toka nje, sahihi ni tokea nje/toka ndani
16. ukweli, sahihi ni kweli
17. uoga, sahihi ni woga
18. nk.
wengine mwaweza kuongeza ama kusahihisha.
wapendwa tukienzi kiswahili.
Glory to God
kufariki dunia ni nahau ikiwa na maana ya kutengana (separate) na dunia. neno fariki limetokana na neno faraka. hivyo mtu anayekufa anakuwa amefarakana (ametengana au kwa kingerza ame-separate) na dunia na ndiyo iasema "amefariki dunia". kwa hiyo neno sahihi ni kufa na kufariki dunia ni nahau inayokusudia kukata makali ya neno lenyewe. ni sawa na kusema fulani "anajamiiana" na fulani kwa lengo la kupunguza ukali wa neno halisi wakati neno lake sahihi linajulikana na kila mtu
sitosema sn hapa lkn tujiulize hiki kiswahili sanifu/sahihi kinaweza kutuvusha katika hili wimbi la utandawazi? je mwaonaje sasa JF iweze kuanzisha mtandao wakujifunza kiingereza kwa kutumia audios au vidios zitakazo wawezesha baadhi ya wenzetu wasioweza vizuri kujifunza?
hapo penye wino mkolezo, jibu langu ni: bila shaka !!