msadapadasi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 504
- 62
kuhusiana na utofauti wa neno SWALI na SUALI ni hivi, hapa ni kwamba kuna umbo la ndani na umbo la nje mara zote umbo la nje ni vile linavyotamkwa wakati umbo la ndani ni kwa kuzingatia asili ya neno lenyewe, hivyo neno SWALI linatokana na neno la asili SUALA, lakini lugha ya kiswahili ina kanuni zake, kwa mfano, kanuni ya uyeyushaji ndiyo inatupatia neno SWALI, yaani'Kule visiwani pia wenzetu wanasema suali na sisi bara tunasema swali. Mfano: "sikulielewa suali lako" na "sikulielewa swali lako" neno lipi kati ya haya mawili ni sahihi.
U+A=WA yaani
S(U+A)LI=SWALI..
Hii ina maana kuwa wa-zanzibari wana wanapendelea kutumia na kutamka umbo la ndani la neno hilo wakati wa-bara (TZ) wanatumia umbo la nje katika kutamka.
UZIADA: Hata hivyo,kanuni hii hatuwezi kuitumia katika neno SUALA ili kupunguza utata utakaojitokeza mfn;
SWALA,yaweza kuwa ibada (worship), au myama wa porini jamii ya mbuzi, hivyo itabakia kuwa SUALA badala ya S(U+A)LA=(yaani)
SWALA.
NAWASILISHA...