Naomba kujuzwa zaidi kuhusu Toyota Passo

homomorphism

Member
Feb 12, 2017
62
53
Naomba kujuzwa zaidi kuhusu Toyota Passo

Naomba kufahamu ubora na changamoto za Passo.

Passo.jpg

Picha: Toyota Passo
 
Naomba kufahamu ubora na changamoto za passo.
Gari dogo nje ndani pana. Kale ka cc990 mafuta kidogo na ac juu unapiga misele ya kutosha ika hakana nguvu na ukiwasha ac unasikia kabisa nguvu yapungua.

Kana tatizo la kugonga miguu so kama waishi mabondeni utakuwa unakatesa.

Kana baadhi ya vipuri bei kuliko hata alteza ila si vingi.

Kama mpenda misele hujali kusimangwa na unaishi town ni kagari kazuri kama kipato chako ni kidogo ili mradi usi kaover use.

Niliwahi kamiliki kwa miaka miwili nilikanunua kwa mhindi fulani nikaakaa nako miaka miwili zaidi ya services za kumwaga oil na kubadilisha brake pads sikuwahi pata changamoto labda ya kubadilisha engine mount.

Nami nikaja nikamuuzia mtu kwa pungufu ya milion 1.3 ya bei nliyokanunua.
 
Gari ni matumizi na matunzo yako mwenyewe. Hakuna gari mbaya ama rahisi kuharibika.

Ila kibongo bongo utaambiwa ni gari mbovu, haina nguvu, inasumbua, inagonga chini, ac yake haidumu. Hayo yote ni matokeo ya matunzo duni.

Utakuta mtu ana ki Passo na anakaa madongo kuinama kwenye mabonde na makorongo halafu anatarajia gari isigonge chini.

Mara ya kwanza kumiliki Passo ya cc990 piston 3 ilikuwa ni mwaka 2013. Niliinunua used ya Japan kupitia Durban, South Africa.

Niliiendesha kutoka Durban mpaka Dar bila tatizo lolote.

Niliileta maalum kwa ajili ya safari za mjini tu zaidi lami kwa lami.

Nilimuuzia rafiki yangu mwaka 2019 ikiwa full ac, haichemshi, haigongi wala kusumbua chochote.

Jamaa anaishi kimara Bonyokwa, baada ya miezi minne ile gari ilikuwa hata flyover ya Mfugale haina nguvu ya kupanda, yote sababu ya rough usage.

Narudia tena, gari ni matunzo.
 
Passo iliundwa kwa ajili ya wacheza golf kule Italy,waliweka order kiwandan kwa sababu ya kuingia navyo uwanjan, kuna mwaka kombe la dunia passo zilikuwa waz juu zilitumika kama machela uwanjan,

Sasa huku tz mtu anasafiri nako dar to mwanza au unakagongesha kwenye mashimo kataacha kufa, utunzaji wako ndio uzur wake, kasipige kaz sana ukakaover-dose
 
Back
Top Bottom