Naomba kujuzwa changamoto za gari ya Toyota Alphard na aina zake

Model gani Alphard? Engine kubwa V6 au engine ndogo i4?

Crown na Alphard zipo class tofauti sana kufananisha. Alphard ni family car, Crown ni Midsize sedan.

Zote kwenye wese ni mbaya, ila spare utazipata ila sio kwa bei ndogo.

Ngoja nikuulize maswali ambayo yatasaidia wengine wakushauri gari zuri hapo?

1. Upo mkoa gani? Kama nje ya Mji izo gari zina ground clearance ndogo sana. Hazifai.

2. Matumizi yako ni yepi sana sana? Kama ni kwenda na kurudi tu kazini Crown itafaa ila kama kuna kubeba Sana mizigo mfano una duka basi Alphard.

3. Married with family au una mpango wa kua ba familia hivi soon? Kama una familia na watakua wanatumia (mnatumia) wote kwa Pamoja mara kwa mara, Alphard ni kubwa itafaa ila Crown ndogo seat ya nyuma mfano ukifunga seat ya mtoto mdogo haikai vema.

4. Kwa siku una utembezi wa kilometa ngapi? Kama kilometa nyingi izo chuma zinabwia sana wese. Jiandae kwa 7km/L.

5. Ushawahi kua na gari au ndio la kwanza? Kama ndio la Kwanza, izo sio chaguo sahihi
 
1.Nipo arusha

2.Nina familia

3.Matumizi yangu ni kwenda kazini na kurudi

4.Tutatumia kama usafiri wa familia

5.Ni mara yangu ya kwanza kumiliki gari

Sent from my SM-A145F using JamiiForums mobile app
Namba 3 na 4 vinapishana.

Kuna mtu alitaka kununua gari. Tukamshauri IST. Akauliza inaweza kufika kwetu Mwanza (anakaa Dar)?

Nikamuuliza, kwa mwaka unaenda kwenu Mwanza mara ngapi? Unakuta ni mara moja au asiende kabisa.

Kwanini ununue gari kisa kwenda nalo kwenu mara moja tu? Let say siku 10 hafu the rest siku 355 za mwaka zinakuumiza kwasababu sio matumizi ya iyo gari.

My point, Alphard utaitumia Jumatatu to Ijumaa kwenda nayo kazini hafu weekend ndio unatoka na familia (kanisani, masjid au out). Ila sio matumizi makuu.

Alphard ni gari kubwa sana, yaani boat. Na usitegemee matumizi ya mafuta yakawa mazuri. Sasa kwa matumizi yako sidhani kama ni gari sahihi.

Ila nashauri ungeanza na gari dogo (mfano Corolla family) au Wish, nayo ni kubwa.

Pendekezo kubwa kabisa ningeshauri ununue Toyota Raum.
 
Vuta premio ,huko kwingine utajuta,ninalo hapa crown natafuta mteja lina mwezi tu ila jasho la kwapa limenitoka,hili nijini tena la mguu mmoja
Haya magari ya engine kubwa mazuri pale unakua na safari ndefu, au mafuta kwako sio shida.

Kuna mzungu nilikutana nae sehemu sasa katika story akaniambia magari aliyonayo yeye na wife home kwao. Wana Ford zile truck F150, ana SUV nyingine, ana Mazda Miata (kaduchu sana haka kagari kana umbo kama BMW Z3), ila ana Toyota Prius 2nd generation.

Point yake, kila gari lina matumizi yake. kiwa na family trip au vacation anabeba SUV, weekend track days anatumia Miata ni sport car, akiwa anataka kuvuta mzigo (mfano camper au boat) au kununua vitu anatumia Ford, ila Prius ni daily car. Kwasababu ya fuel consumption.

Ila sasa sisi kutokana na vipato vyetu, unatakiwa uwe na gari ambalo litakidhi matumizi yooote.

Ndioa maana tunavyonunua lazima tucheki sana sana.
-Fuel consumption na running costs. Gari ni appliance usitake ikutese kila siku wese la 20k.
-Matumizi. Imagine una gari ata siku mkisema familia mtoke wote, wengine itabidi wapakatane au wachukue Uber.
 
1.Nipo arusha

2.Nina familia

3.Matumizi yangu ni kwenda kazini na kurudi

4.Tutatumia kama usafiri wa familia

5.Ni mara yangu ya kwanza kumiliki gari

Sent from my SM-A145F using JamiiForums mobile app
Mimi ninayo Alphard mwaka wa 5 huu.. Ni nzuri sana.. Chukua cc 2360 usinunue yale yana kama pampa limeshuka mpaka chini noo.. Yale yanachakaa haraka bodi lake.
Hata bei yake daima ni chini kuliko Alphard Nyingine.
Suala mafuta ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko kiuchumi..
Inafaa sana ukitumia peke yako, familia au hata kikundi maana ina siti 8.
Viti vyake unavigeuza upande unaotaka.. Unaweza ukaweka kiofisi, ki conference, ki luxury, kubwa kuliko vile viti ni vitanda vizuri sana yaani ukikunjua unalala kama nyumbani tuu.
Ukiwa na safari au misibani au piknik huhitaji kutafuta lodge unaweza kulala kwa raha kabisa hata watu 3.

Ukikunja viti vya nyumba unabeba mzigo kama wa kirikuu na ukikunja na vya katikati ni balaa kirikuu haioni ndani, full tinted unapita unampungia mkono trafic.
Kwa uzoefu wangu ile gari ina matumizi mengi sana sana ni vile utakavyoamua au kutokana na mazingira ya wakati huo.

Huwezi juta hata siku moja kuwa Alphard.. Kwanza ni kubwa na pana sana mule ndani.. Dereva unakaa kwa nafasi na paa la juu bado lipo mbali huwezi gusa kwa kichwa.
Kwa nje linaonekana kama lipo chini lakini ndani lipo juu sana.

Kama ukinunua yale ambayo ground clearance yake ni ndogo.... Simpo tuu ni kwa mafundi wanakuwekea Spencer za inch moja moja au moja na nusu inakuwa juu vizuri.

Mimi napita nalo popote vumbi, au barabara nzuri, makorongo, mashimo popote, milima, au mabonde.

Service fuata oil sahihi ya engine 10w30 na gear box type iv.. Mengine kawaida.
 
Mimi naona kama pesa iko kiasi ni bora kuwa na Gari mbili moja ya injini ndogo kabsa na moja ya injini kubwa kwa ajili ya masafa.

Kusafiri safari na gari yenye injini ndogo ni mateso sanaaaa,lakini kuwa na gari ya injini ndogo kwa mizunguko ya kila siku mjini ni nzuri sana.
 
Mimi naona kama pesa iko kiasi ni bora kuwa na Gari mbili moja ya injini ndogo kabsa na moja ya injini kubwa kwa ajili ya masafa.

Kusafiri safari na gari yenye injini ndogo ni mateso sanaaaa,lakini kuwa na gari ya injini ndogo kwa mizunguko ya kila siku mjini ni nzuri sana.
Upo sahihi kabisa
 
kwa hapo angalia moyo wako unapenda nn, kuhusiana na mafuta eti kisa ununue ist au raum utajitesa crown athlete inatembea km 7-10km/l mjini ist mjini km10/l kwahyo inapishana kidogo tu. Na kuogopa kumiliki gari zuri kisa mafuta huo ni ujinga kwa maana hakuna gari isiyo kula mafuta kikubwa uwe na nidham kwenye uendeshaji kwa maana hata hyo ist au raum ukiwa una driving skills mbovu itakupa km 8/l. Kikubwa tunza gari na sio kila mahari kwasabab ww una gari bas unaenda nalo.
 
Back
Top Bottom