Naomba kujuzwa, ile picha inayoonekana pale mwezini ni nini!!

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,973
27,209
Wakuu poleni na majukumu na harakati za hapa kazi tuu!!ni mda mrefu kidogo sikuwa hapa jukwaani kutokana na kazi!!vilevile niwatakie heri ya chrissmass na mwaka mpya! Namshukuru mungu nimerudi salama huko nilipokuwa!!katika pitapita zangu nimeulizwa hili swali nikashindwa kujibu maana mimi sio mtaalam wa hizi sayansi!!

Hivi ukitizama mwezi kwa makini pale kama kuna picha ya mtu anaonekana!!na ukitizama kwa haraka haraka unaweza ona kama kuna mtu kabeba mtoto mgongoni na kichwani kabeba mzigo wa kuni mara myingine hua kama kakaa anasukuma kitu kama wale wanawake wa kizamani wanasaga mahindi kwenye jiwe au mara inaonekana kama kuna mwanamke anatembea je!!!

Kuna ukweli wowote kuwa kuna picha au ni mtizamo wangu wa kifikra!!

Naomba wataalam wanifafanulie hilo!!
 
mwezi ni kama dunia hivi ilivyo kuna mabonde na milima kwahiyo ile reflection ya mwanga wa jua inasababisha vivuli baadhi ya sehemu na kutengeneza hizo image mnazoona na kwa coincendence tunaona kama mtu tukiwa wadogo walisema maria kambeba Yesu.
 
Unapoangalia mwezi au mawingu utapata taswira ya picha fulani, nikawaida sana, sasa nikwamba kila mtu anapata taswira yake anapoangalia vitu hivi , kwa mfano unaweza kuangalia wingu ukaona kama mtu ameshika jembe analima, au ukaona kikombe cha chai nk, hivyo hivyo kwenye mwezi pia unaweza ona mama amebeba kuni au ndoo au mtoto mgongoni au ukaona kondoo, hii inategemea mental yako inatengeneza picture gani kwa kile unacho kiona, ila sio kweli kwamba eti mwezin kuna mama kweli amebeba mtoto au kuni au ndoo , ni issue ya mental picture tu
 
What you see is what you get! Hiyo picha umeichora mwenyewe mawazoni mwako,kisha ukaibandika hapo kimawazo!na ukaiona jinsi ulivyotaka kuiona!
Lakimi mkuu mbona hiyo picha sio mimi tuu nimeiona kila umaemuuliza anakujibu jibu sawa na mwingine hilo hilo
 
Unapoangalia mwezi au mawingu utapata taswira ya picha fulani, nikawaida sana, sasa nikwamba kila mtu anapata taswira yake anapoangalia vitu hivi , kwa mfano unaweza kuangalia wingu ukaona kama mtu ameshika jembe analima, au ukaona kikombe cha chai nk, hivyo hivyo kwenye mwezi pia unaweza ona mama amebeba kuni au ndoo au mtoto mgongoni au ukaona kondoo, hii inategemea mental yako inatengeneza picture gani kwa kile unacho kiona, ila sio kweli kwamba eti mwezin kuna mama kweli amebeba mtoto au kuni au ndoo , ni issue ya mental picture tu
Mkuu vipi kwa mtizamo wako wewe unaona nini kuwa muwazi!!hapa tunafundishana!
 
Kila Watu na Imagination zake sasa Sijui wazungu Nao Watakuwa Wanaona Mwanamke amebeba Kuni.....
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Back
Top Bottom