Naomba kujua walipo waimbaji wa kwaya ya Ulyankulu Bara barabara ya 13

Ooh no, hope sahiv watakuwa wazee jamani
😭😭, niliwapenda sana, na nyimbo zao ni bomba mbaya
Kumbe wengi walikuwa nayo hii album aisee home nilikuwa dogo basi kila leo inapigwa hii album mbaka waislam wengi sana waliipenda kuna wimbo ulikuwa unaitwa ima nikuwa nayo hakikaa kwa mambo yatarajiwayo... Niliipenda sana kwakweli nilikuwa dogoo
 
Hii kwanya iliundwa na wakimbizi kutoka burundi waliokua wakiishi ulyankuru tabora, mwanzoni mwa miaka ya 2000 serikali iliwahamisha na kuwapeleka kambi za kigoma ikiwemo nduta, kanembwa na nyarugusu, baadhi walipata nafasi za kwenda ulaya, australia na amerika kupitia unhcr na wengine kurudi kwao burudi, nilikua nafanya biashara na baadhi yao na bado tunawasiliana hata baada ya kwenda majuu, huwa wananitumia hela nawanunulia bidhaa kama nguo, dagaa na vyombo vya nyumbani, unaweza kushangaa kusikia mtu yuko us ila ananunua nguo na vyombo afrika ila ndio hali halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasalimie mkuu, waambie Bushmamy pamoja na Bushdady bila kusahau bush's children wanawasilimia sana.

Pia sio mbaya ukitupia picha zao tuwaone walivyo hivi sasa 🤔🤔
 
Na sasa umeuacha Wokovu?
Aisee ni kweli,kujua hizo nyimbo lazima uwe kwenye familia ya utumishi au anamjua Mungu,enzi hizo nilikuwa nazunguka na mzee kwenye mikutano ya Injili,usiku kuanzia saa moja nawasha jenereta naweka tapes za hizo nyimbo halafu mida ya saa mbili mkanda wa Mateso ya Yesu au Samson & na delila tunaweka,l.

Basi watu wanajaa,pale kwenye mateso ya watu wanaanza kulia na kutubu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hiyo Album imetoka mwaka gani.?
Kinachofanya nizipende hizi nyimbo Mama alikua anapenda sana kuimba akiwa anatuogesha au akitwanga muhogo huo wimbo wa viumbe vyote. Kwaya nyingine ni ile ya kasulu waliimba Mke mwema..sijui wako wapi. Na wale wa Tabata waliimba sipati picha sijui walipotea wapi
View attachment 1404431
Mtoto mdogo sana ww kumbe....!!?
mm nimezaliwa wakati wa LEGCO Tanganyika
 
Mungu katuumba kwa mfano wake
Katutofautisha na vingine

Katutofautisha na wanyama
Wasio na akili
Katupa kujua mema mabaya
Ili.

Walimwengu wengine hawajui
Aliye mkombozi
Atakayerudi kuchukua
......
Ajabu Yao, akili walipewa hawakujua aliyewapa


Kwa viumbe vyote
Old is gold
Sent using Jamii Forums mobile app
👏👏👏👏
We mhenga kumbe?

Nyimbo nyingi za kwaya za zamani ni nzuri sana, huchoki kusikiliza.
 
Back
Top Bottom